Salamu zangu ziwafikie Viongozi wote

MGANGA MCHAWI

Senior Member
Oct 15, 2015
199
393
Nimekua nikifuatilia hotuba na mahojiano ya baadhi ya Viongozi wa kiserikali na vyama vya siasa wakitoa mitazamo yao kuhusu swala la ukosefu wa ajira na utatuzi wake.
Kwanza niwapongeze kwa kukubali kuwa ajira ni janga la taifa sio la Tanzania tu bali ni dunia kwa ujumla.
Katika kutatua tatizo hili viongozi wengi wamekuwa wakiwalaumu vijana kuwa wameshindwa kuwa wabunifu na wamekuwa wavivu kujiajiri kutokana na Elimu walioipata.

Baadhi ya viongozi wamefikia hata hatua ya kushangaa kwamba inakuaje kijana mwenye shahada anashindwa kujiajiri?Wamejaribu kuwa "insipire" vijana wajiajiri kwa kutoa mifano ya baadhi ya waliofanikiwa kimaisha kwa kujiajiri.Wengine wamefikia hatua ya kuelezea historia ya maisha yao waliyopitia hadi wamefika walipo ili mradi tu waweze kueleweka kwa kile wanachoshauri.
Ukweli ni kwamba hakuna asiependa kuwa na maisha mazuri hasa kwa sisi vijana ila wengi tunakosa njia ya kuyapata hayo maisha mazuri.Na wengi wanapenda kujiajiri ila wanakosa msingi wa kujiajiri.

Viongozi wanapotoa suluhisho la tatizo a ajira ni vizuri kwanza wajiveshe viatu vya kijana mwenye hali duni yule aliyesoma kwa tabu bila mkopo na akiwa na majukumu ya kuwasaidia ndugu zake, hapo ndipo mtatoa suluhisho zuri ambalo litawajumuisha vijana wote.

Lazima tukubaliane kwamba viongozi wetu wengi ni wale ambao hawajawahi kuangaika swala la ajira.Wengi walikuwa wanaajiriwa moja kwa moja toka vyuoni au wameishi katika mfumo rafiki wa baada ya kuhitimu shule tu wakapata ajira rasmi. Hawajui tabu ya kuzunguka na bahasha ya kaki kwenye ofisi za wahindi. So wanashindwa kuvaa uhusika wa tatizo la ajira na pia wamekosa ubunifu wa kutatua swala la ajira.


Mfano, kiongoz unaposema vijana wakajiajiri katika kilimo lazima ujiulize; Je wataipataje ardhi kwa ajili ya kilimo? Kuna Mazingira rafiki ya vijana kupata ardhi? Upatikanaji wa pembejeo ni wa uhakika? Na watazpata kwa masherti rafiki kwa kijana alietoka shuleni?
Kuna vijana wengine wamekulia kwenye nyumba za kupanga na familia zao hazijawai hata miliki kiwanja.

Pia lazima Viongozi waelewe kuwa wanaolalamika ajira wengi ni wale wenye hali duni ya ufukura kabisa sio wale waliokuwa na uhakika wa milo mi3 kwa siku.Ni wale waliokabiziwa wadogo zao wa kuwasomesha kabla hata hawajamaliza kidato cha sita.

Kingine lazima waelewe swala la ajira linahusisha vijana wenye kiwango cha elimu tofauti.Lazima wagawe vijana katka makundi matatu
1)Wenye elimu ya chini( Darasa la 7 hadi form 4)
2)Wenye elimu ya kati (form 6 hadi diploma)
3) Elimu ya juu ( 1st degree na zaidi)
Kwa hiyo utatuzi wao ni lazima ulenge makundi yote matatu au watafute namna ya kuwezesha kundi moja ili liwasaidie kundi lingine.

Ikumbukwe kwamba serikali yeyote ina wajibu wa kutoa ajira kwa raia wake.
Na ina uwezo wa kutoa ajira either "direct" au "indirect".
Direct ni serikali yenyewe kuajiri raia wake wenye uhitaji wa ajira na indirect ni serikali kuandaa mazingira rafiki ya raia wake kuajiriwa kwenye sekta binafsi au kujiajiri wenyewe.

Ukweli ni kwamba serikali haiwezi kuajiri wahitaji wote wa ajira. Njia pekee ni kuweka mazingira ya vijana kuweza kuajiriwa na sekta binafsi au kujiajiri.
Tatizo viongozi wetu wanatoa suluhisho ambalo haliwezi kutumika katika dunia halisi ya vijana wengi.

USHAURI WANGU.
1)Serikali iandae sheria (kama haipo) ya kudhibiti makampuni toka nje au wazawa kuajiri raia wa kigeni kwa kazi zinazoweza fanywa na watanzania au kama ipo basi waisimamie ipasavyo kwani tumeshuhudia kazi nyingi zinazoweza kufanywa na wazawa zikifanywa na watu toka nje.
2)Kuimarisha sekta binafsi.Ili kutatua tatzo la ajira ni lazima serikali iimarishe sekta binafsi kwa kuweka mazingira mazuri ya kibiaashara na uwekezaji
3)Kuandaa utaratibu wa vijana kupata mikopo kwa masherti nafuu.Masherti ya mikopo si rafiki kwa vijana wengi.Wengi hawana mali zisizohamishika ambazo ndio kigezo kikubwa kwenye sekta nying za fedha.
4) Kuboresha sekta ya kilimo nchini kwa kuandaa mazingira mazuri ya upatikanaji wa ardhi, maji na pembejeo za kilimo kwa vijana.
5) Kuongeza shule na vyuo vya ufundi.
6) Kurasimisha sanaa kama kazi rasmi.
Serikali lazima itambue sanaa kama njia mojawapo ya vijana kujiajiri.Iweke mazingira ya vijana kuweza kunufaika na sanaa.Iweke mazingira rafiki ya wasanii kupata maeneo ya kufanyia kazi/kuibua vipaji na kuviendeleza pia kutangaza vipaji vyao.
Iandae sheria itakayobana watumiaji wa kazi za wasanii kuwalipa wasanii wa kazi hizo.
...........ongeza hapa nyingine.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom