Salamu zangu za haki kwa Mhe Raisi JK (wapi? ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya?) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salamu zangu za haki kwa Mhe Raisi JK (wapi? ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya?)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kimboka one, Feb 8, 2012.

 1. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mhe rais wangu,nimeona nikupe salamu zangu hizi,mimi ambaye ni mtanzania wa chini kabisa baada ya kuona mambo yanakwenda kombo ili hali sisi watanzania wakawaida kwa imani kubwa tulikuamini na kukutuma ukafanye maisha yetu kuwa bora maana ulituambia utafanya kwa amri mpya,nguvu mpya na kasi mpya,kwa hakika kipindi chako cha siku 100 ulifanya vizuri nasi tukaamini kuwa kweli Mungu amekupa hekima ya kutimiza ahadi zako na kiapo chako.

  Lakini kadri siku zilivyo sogea nahisi Mungu alianza kujitenga nawe hata ukapata hofu kabisa ya kutamka tena ARI MPYA, NGUVU MPYA NA KASI MPYA. Mhe raisi sina maana ya kukusimanga au kukudhihaki hapa ila kukumbusha roho nyingi za Watanzania ambazo ziko mikononi mwako na sasa zinataabika.

  Kwa kukosa matibabu(migomo ya madaktari)
  Kukosa elimu kwa viwango vinavyatakiwa(migomo baridi ya waalimu)
  Kukosa sehemu walau kidogo ya rasilimali walizopewa na Mungu wao(madini,viumbe wa maji,milima na mbuga za wanyama na mali chungu mzima)
  Kukosa utulivu na amani ya kweli
  Na mengine mengi yanayowataabisha.

  Mhe raisi wangu najua ni vigumu kufanya maamuzi magumu kama wengi wanavyoshauri kwani wanaokukosea ni maswaiba wako wakubwa na watoto zao au wake zao na mashemeji wao.

  Lakini leo naomba nikueleza kuwa huku Tanzania ambako wewe ni vigumu kufika hali ilivyo.kwani hapa ninaamini kupitia watu wako unaweza kupata ujumbe huu. Watanzania wamekuchoka kiasi cha kutamani nchi yao ambayo ni maarufu kwa kisiwa cha amani itawaliwe na raisi dikteta au itawaliwe na jeshi.

  mkuu kwa ufipi watanzania waliokuchagua 2005, siyo wa leo hali ni mbaya sana kwani wanajua kila kitu unachofanya hapo magogoni,hii ni kutokana na uhuru uliyowapa wa kujadili. Ushauri wangu,bado unaweza kufanya jambo kuwatuliza wabunge wa CCM ambao wewe unajua hali ilivyo lakini pia wananchi ambao wanahasira sana na serikali yako.

  1. kubali kuvunja uhusiano na maswaiba zako kwa heshima ya taifa.
  2. kubali kufanya kazi na watu ambao si marafiki zako ambao ni wachapakazi.
  3. usiogope watu watendakazi wazuri kama Magufuli,Mwanri na wengi,kwa kuhofia umaarufu wako kupungua.
  4. kubali wakati mwengine kupishana na mataifa ya ughaibuni kwa manufaa ya nchi yako.
  5. kubali na kiri umewakosea watanzania na kufungua ukurasa mpya.
  6. kubali kuvunja baraza la mawaziri haraka iwezekanao kwa kuweka pembeni watu ambao ni tatizo nawe unajua,kubali kulegeza shingo yako mkuu. Kwa kufanya hayo utanusuru mgomo wa madaktari na mgomo mkubwa unakuja wa WALIMU.

  Pia utarejesha heshima yako na imani yako wa watanzania na tena kudhubutu kusema tena ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya kwa kujiamini na kifua mbele.

  Kadhali utapata kustaafu kwa heshima na kunusuru wakina riz wasizomewe kila watakapo pita kwa watanzania kwa kukumbuka machungu aliyosababisha baba yao. Mimi ni mtanzania wa kawaida sana lakini nisiye na chuki na CCM kwani ninajua ccm ubaya wake ni watu na kama akipatikana mtu wa kusafisha hali itakuwa safi tu,tena sina shaka na vyama vya upinzani hata kidogo,kwani mawazo yao ni mazuri na pale wanapokushauri usipuuze ata kidogo tena tenga muda wa kutosha kusikiliza na kusoma hotuba zao mbadala na bajeti zao bungeni pengine utajifunza jambo.

  Mwisho nakutakia kazi njema na utekelezaji wa haya na mengine ambayo watanzania wengine wataweka hapa chini.

  Tafadhali wadau tumshauri raisi wetu ili apate nafasi ya kujisahihisha na msianze kutukana au kuweka ushabiki wa vyama vyenu.
   
 2. M

  Madodi Senior Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 181
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  rais kihiyo kuwahi kumuona ktk maisha yangu
   
Loading...