MO11
JF-Expert Member
- Mar 23, 2014
- 18,857
- 38,605
Ni mwaka sasa umepita tangu niifute namba yako kwenye simu yangu
Japo juzi juzi umenitafuta ila sio kupitia namba yangu kupitia kwa ndugu yangu habari nikazipata nikamwambia achana nae
Kiukweli baada ya kuniambia kichwa changu hakikukaa sawa ndo nikajua bado upo moyoni mwangu na kichwani ila mikononi mwangu haupo
Nikikumbuka tulivyokuwa pamoja japo kwa kipindi kifupi ulikaa sana moyoni kuliko yeyote yule nilikupenda kweli sijawahi kupenda hivi hata ile nyimbo yetu niliifuta siitaki tena kuisikia picha zako nikafuta ila kukufuta moyoni nimeshindwa nasikitika kwa kweli
Sijui nilipokosea nahisi uliniona mtoto nilipokuwa nakuimpress ndo tatizo
Kwa kweli nilikupigia simu tukaongea nachoshukuru hukuniuliza mimi nani ulinijua japo nimebadili namba kwa ajili yako ila sauti yangu umeikumbuka sijui unawaza nini huko ulipo
Ila nahisi utakuwa unafuraha umempata mwengine labda mrefu kuliko mimi hensam boi na mweupe au labda ana hela kunizidi
Mimi bado nipo vile vile mcheshi as always nikiwa na buku mfukoni nitakupa mia 9 mia iliyobaki nitakudanganya ya kukwangulia vocha
Nilipanga tutazunguka sehemu nyingi ila mpaka nikizipata ukachoka ahadi zangu
Ni mimi uliyeukodi moyo wangu kwa kipini chako puani
Mr H