Salamu Zangu Kwako Nape Nnauye

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,429
1,045
Salaam zangu zikufikie Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg. Nape Nnauye. Salamu hizi zinaambatana na pongezi za dhati kwa ukimya wako uliosaidia kuwepo kwa utulivu katika chaguzi za ndani ya chama zinazoendelea na kuelekea ukingoni kwa ushwari wa kupongezwa. Matarajio yangu ni kuwa Nape utakuwa umetambua kwa kiasi gani matamshi, matamko na mabandiko yako katika mitandao ya kijamii huathiri sana michakato, sura ya chama na huweka sifongo katika siasa za makundi ndani ya chama.

Ni ushauri wangu kuwa chama kijihoji kama kinaweza kukutumia (Nape) katika nafasi nyingine yenye mahitaji ya vipawa na sifa ulizonazo ili kuendeleza utulivu huu. Niweke wazi, ninakufagilia sana Nape kwa jinsi ulivyosimama kuhesabiwa miongoni mwa Watanzania wachache waliomnyooshea Lowassa kidole na kumwambia kuwa "wewe ni FISADI" bila kupiga ukope wala kumung'unya maneno. Na kubwa zaidi katika hili la Lowassa wewe ni kijana wa pekee uliyebaki na msimamo madhubuti bila kuyumba wala kuyumbishwa. Lakini ninatofautiana nawe katika maeneo mbalimbali na kubwa likiwa ni katika tafsiri halisi ya neno na matendo yanayomaanisha UZALENDO wa kweli.

Nakutakia utendaji mwema na wa mafanikio makubwa zaidi katika majukumu yako.
 
Hivi kwa nini Nape Nnauye akiacha kuanzisha mijadala kwenye mitandao ya kijamii (kwa jina halisi) na kupotea kwenye mainstream media kunakuwa na utulivu ndani ya ccm?
 
Last edited by a moderator:
. Niweke wazi, ninakufagilia sana Nape kwa jinsi ulivyosimama kuhesabiwa miongoni mwa Watanzania wachache waliomnyooshea Lowassa kidole na kumwambia kuwa "wewe ni FISADI" bila kupiga ukope wala kumung'unya maneno. .
kaka unampongeza au unampalia mkaa...
 
kaka unampongeza au unampalia mkaa...
Nampongeza kwa dhati kabisa maana lile ni jabali la ufisadi na ndani ya nchi inayoitwa Tanzania ni wachache sana ambao wameweza kusimama kuliambia wewe ni mwizi na fisadi na wakadumu kutetea kauli na misimamo yao. Nape Nnauye ni mmojawao. Amewashinda hata viongozi wa dini waomtetemekea na kuruhusu madhabu za Mungu wetu kunajisiwa kisa mali na pesa?! Ukiona hadi Mzee Mengi kakubali Lowassa aanze kupata coverage ya kutosha kwenye vyombo vya IPP kubali tu kuwa Lowassa anatisha!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom