Katika nchi za kiafrika mara nyingi siasa za upinzani huanzia mjini na kusambaa kwa kasi ndogo kuelekea kijijini. Lakini kwa Tanzania kwa hivi sasa hali ni tofauti sana. Nimekuwa vijijini kanda ya ziwa kwa mwezi na wiki kama mbili kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na nimerejea mjini tayari kwa kibarua jana. Nilchoona kijijini, naweza kusema subirini kishindo kikuu miaka hii miwili ya uchaguzi.
Kijijini watu wanafungua misingi ya chama bila usimamizi wa mtui yoyote, wana fomu zinaozoonyesha msingi unatakiwa kuwaje basi. Nimeshiriki kuungua misingi zaidi ya 50 na kukaa vikao vya ndani zaidi ya 40. Watu wanachaguana na kuwekeana marengo ya kujenga chama kwa kushona bendera zao wenyewe. Wanashona mavazi ya chama wao wenyewe.
Viongozi na wanachama wa Ccm kujiunga Chadema siyo story tena, story ni kwamba serikali haitangazi uchaguzi mdogo ili wamalize hasira zao. Ndugu zangu vijijini akina mama wako mstari wa mbele ktk mapambano, mfano jimbo la Kyerwa kuna vikundi vya akina mama wa Chadema zaidi ya hamsini. Wanachangiana fedha wananunua sare za chama na kuinuana kiuchumi. Wana kaulimbiu yao inasema "Chadema guma, abakazi tuliyo" yaani Chadema msiwe na wasi wasi wanawake tuko nyuma yenu!
Udini uko mjini, kijijini hakuna habari kama hiyo. Nimeshiriki kufungua tawi ambalo viongozi saba ni waislamu kati ya 10, kumbuka maeneo ya kanda ya ziwa waislamu ni wachache sana. Kwa sababu ya hali ya miundombinu nililazimika kupanda pikpiki muda mwingi, lakini kila nilipotaka usafiri kwa kazi ya chama sikukodi wala kuweka mafuta. Muda wote niliambiwa pikipiki zipo kwa kazi ya chama.
Changamoto waliyo nayo kubwa ni kadi za chama, maana nimeona watu zaidi ya 100 ambao wamerudisha kadi za Ccm zaidi ya miezi miwili lakini hawajapata kadi za Chadema. Nimejaribu kuwasiliana na viongozi wa kanda ya ziwa magharibi lakini nako nikaambiwa kuna tatizo kubwa la upatikanaji vifaa vya chama. Natajaribu kuwasiliana na mkurugenzi wa uenezi nimpe hali hii.
Asanteni!