Salamu za wana-Chadema wa vijijini kwenu wana-Chadema wa mjini!

Kaguta

JF-Expert Member
Jan 31, 2013
414
225
Katika nchi za kiafrika mara nyingi siasa za upinzani huanzia mjini na kusambaa kwa kasi ndogo kuelekea kijijini. Lakini kwa Tanzania kwa hivi sasa hali ni tofauti sana. Nimekuwa vijijini kanda ya ziwa kwa mwezi na wiki kama mbili kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na nimerejea mjini tayari kwa kibarua jana. Nilchoona kijijini, naweza kusema subirini kishindo kikuu miaka hii miwili ya uchaguzi.

Kijijini watu wanafungua misingi ya chama bila usimamizi wa mtui yoyote, wana fomu zinaozoonyesha msingi unatakiwa kuwaje basi. Nimeshiriki kuungua misingi zaidi ya 50 na kukaa vikao vya ndani zaidi ya 40. Watu wanachaguana na kuwekeana marengo ya kujenga chama kwa kushona bendera zao wenyewe. Wanashona mavazi ya chama wao wenyewe.

Viongozi na wanachama wa Ccm kujiunga Chadema siyo story tena, story ni kwamba serikali haitangazi uchaguzi mdogo ili wamalize hasira zao. Ndugu zangu vijijini akina mama wako mstari wa mbele ktk mapambano, mfano jimbo la Kyerwa kuna vikundi vya akina mama wa Chadema zaidi ya hamsini. Wanachangiana fedha wananunua sare za chama na kuinuana kiuchumi. Wana kaulimbiu yao inasema "Chadema guma, abakazi tuliyo" yaani Chadema msiwe na wasi wasi wanawake tuko nyuma yenu!

Udini uko mjini, kijijini hakuna habari kama hiyo. Nimeshiriki kufungua tawi ambalo viongozi saba ni waislamu kati ya 10, kumbuka maeneo ya kanda ya ziwa waislamu ni wachache sana. Kwa sababu ya hali ya miundombinu nililazimika kupanda pikpiki muda mwingi, lakini kila nilipotaka usafiri kwa kazi ya chama sikukodi wala kuweka mafuta. Muda wote niliambiwa pikipiki zipo kwa kazi ya chama.

Changamoto waliyo nayo kubwa ni kadi za chama, maana nimeona watu zaidi ya 100 ambao wamerudisha kadi za Ccm zaidi ya miezi miwili lakini hawajapata kadi za Chadema. Nimejaribu kuwasiliana na viongozi wa kanda ya ziwa magharibi lakini nako nikaambiwa kuna tatizo kubwa la upatikanaji vifaa vya chama. Natajaribu kuwasiliana na mkurugenzi wa uenezi nimpe hali hii.

Asanteni!
 
kajansi

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
485
0
Mungu akubariki mwanetu! wewe ndo umenipa faraja ya mwaka mpya nawajua sana hao wakwe zangu! nilipata bahati ya kulala pale usiku mmoja kwenye hotel ya fisadi katagila! wapambanaji ni wengi sana. Nitawasiliana na viongozi wa kanda hapa Mwanza tuone jinsi ya kusaidia vifaa kama kadi viwafike. Asante sana, waiyuka no mwaka.
 
Furuguti jr

Member
Jul 2, 2012
43
95
hakika chadema ni mpango wa Mungu makamanda hamna kukata tama
inatia moyo sana kuona tumeingia kwenye ngome kuu ya adui CCM
Big up makamanda
 
celincolyn

JF-Expert Member
Dec 17, 2013
243
0
Katika nchi za kiafrika mara nyingi siasa za upinzani huanzia mjini na kusambaa kwa kasi ndogo kuelekea kijijini. Lakini kwa Tanzania kwa hivi sasa hali ni tofauti sana. Nimekuwa vijijini kanda ya ziwa kwa mwezi na wiki kama mbili kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na nimerejea mjini tayari kwa kibarua jana. Nilchoona kijijini, naweza kusema subirini kishindo kikuu miaka hii miwili ya uchaguzi.

Kijijini watu wanafungua misingi ya chama bila usimamizi wa mtui yoyote, wana fomu zinaozoonyesha msingi unatakiwa kuwaje basi. Nimeshiriki kuungua misingi zaidi ya 50 na kukaa vikao vya ndani zaidi ya 40. Watu wanachaguana na kuwekeana marengo ya kujenga chama kwa kushona bendera zao wenyewe. Wanashona mavazi ya chama wao wenyewe.

Viongozi na wanachama wa Ccm kujiunga Chadema siyo story tena, story ni kwamba serikali haitangazi uchaguzi mdogo ili wamalize hasira zao. Ndugu zangu vijijini akina mama wako mstari wa mbele ktk mapambano, mfano jimbo la Kyerwa kuna vikundi vya akina mama wa Chadema zaidi ya hamsini. Wanachangiana fedha wananunua sare za chama na kuinuana kiuchumi. Wana kaulimbiu yao inasema "Chadema guma, abakazi tuliyo" yaani Chadema msiwe na wasi wasi wanawake tuko nyuma yenu!

Udini uko mjini, kijijini hakuna habari kama hiyo. Nimeshiriki kufungua tawi ambalo viongozi saba ni waislamu kati ya 10, kumbuka maeneo ya kanda ya ziwa waislamu ni wachache sana. Kwa sababu ya hali ya miundombinu nililazimika kupanda pikpiki muda mwingi, lakini kila nilipotaka usafiri kwa kazi ya chama sikukodi wala kuweka mafuta. Muda wote niliambiwa pikipiki zipo kwa kazi ya chama.

Changamoto waliyo nayo kubwa ni kadi za chama, maana nimeona watu zaidi ya 100 ambao wamerudisha kadi za Ccm zaidi ya miezi miwili lakini hawajapata kadi za Chadema. Nimejaribu kuwasiliana na viongozi wa kanda ya ziwa magharibi lakini nako nikaambiwa kuna tatizo kubwa la upatikanaji vifaa vya chama. Natajaribu kuwasiliana na mkurugenzi wa uenezi nimpe hali hii.

Asanteni!
Hii imekaa vizuri tukaze moyo makamanda. Hivi suala la Zitto limefikia wapi? Tunataka liishe mapema kitu kitambae!!!!!!!!!!!!!!!
 
shumanice

Member
Jul 21, 2011
62
95
Hilo unalosema kamanda ni sahihi kabisa, udini, ukabila, ukanda na mengine kama hayo yapo hapa jamvini tu labda na mijini kidogo sana (dsm). Kwa huku kanda ya ziwa mijini na vijijini watu wameshatambua nini wanataka. Cha msingi ni makamanda kufanya kazi kama mchwa (hata kwa kujitolea ikibidi) kukisaidia chama kuweza kufikia malengo. Naamini ukifanya mawasiliano na viongozi wa kanda tatizo hili kitatatuka tu......CDM for development
 
Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,842
2,000
Vijijini ndiyo kwenye maficho ya magamba kama ni hivyo maficho ya magamba yameshavamiwa na huu ndio utakuwa mwisho wa magamba.
 
m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,374
2,000
Umesema kweli tupu kamanda,hata mimi nilienda huko Bunda kijiji cha KAMKENGA na baadaye xmas nikawa kwa babu NAMBAZA,pote kuna changamoto ya kadi hadi wazee kwa kutojua wananiagiza nikirudi mjini niwatumie kadi za uanachama wa CDM.watu wameamka kweli na wanasubiri uchaguzi tu hasira yao waifikishe! KWA SASA CDM NDIYO HABARI YA VIJIJINI!
 
TOFU

JF-Expert Member
Aug 26, 2012
573
250
2015 Chadema wachukua nchi..!!
Belive Me..!!
Godbless Chadema
 
Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
4,945
1,500
Kurugenzi CDM,

Huu uzi mmeuona? tatizo nini, maana hata mimi nimepita viijij vingi bendera za cdm ama zimezeeka au hakuna. Sasa issue ya kadi pia. Pls tafuteni suluhisho ya jambo ilo.
 
SIMBA45

JF-Expert Member
Oct 1, 2012
574
0
Ongera kamanda na kazi ya kujitolea ya kujenga chama.. mungu akubarik kwa mema unayoyafanya kuwakomboa watanzania........
 
spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,533
2,000
Kanda ya ziwa wala usiwe na hofu, Yani usiwe na harara!!!!

Kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu Chadema itapeta sana tu.

Subiri tuone, maana watu hawahtaji kampeni tena.

Washafanya maamuzi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom