Salamu za Uhuru: Rais Magufuli asamehe wafungwa 4,477. Aagiza pesa za sherehe ya Uhuru zijenge hospitali Dodoma. Awataka watanzania wachape kazi

VITA YA KIUCHUMI NI NGUMU KULIKO ILE YA KUDAI UHURU
 
Nampongeza Sana Mhe. Rais kwa matumizi sahihi ya rasilimali za Taifa.
Kwa kitendo kutoadhimisha sherehe hizo kwa desturi iliyozoeleka kuanzia 1961 ameokoa fedha nyingi sana zikiwemo gharama za mizinga, kusafirishaji wa zana na askari, tafrija n.k.
Hongera sana kwa uamuzi huo wa busara na hekima. Kama ikiwezekana sherehe hizo ziwe zinafanyika kila baada ya miaka mitano. Kila mwaka zitengwe fedha Na kupelekwa kwenye mradi mahsusi kwenye mikoa mbalimbali.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atatoa salamu za kumbukumbu ya miaka 57 ya Uhuru kuanzia saa 9:00 Alasiri leo Desemba 07, 2018. Fuatilia matangazo kupitia Televisheni,Radio na mitandao ya kijamii.

Source:Msemaji wa Serikali

---
"Nimeagiza fedha zilizokuwa zitumike kwa ajili ya uhuru, zitumike kujenga hospitali kubwa mjini Dodoma itakayoitwa Uhuru hospital" - Rais Magufuli

"Ninatoa msamaha kwa Wafungwa 4477 kwenye kumbukumbu za maadhimisho haya ya miaka 57 ya Uhuru" - Rais Magufuli

"Nawatakia Watanzania wote tusherehekee miaka 57 ya Uhuru kwa amani na furaha tele. Tuendelee kuchapa kazi, tuendelee kulijenga Taifa letu" - Rais Magufuli

Tunasherekea uhuru gani, kama tu kukuosoa tunaenda jela?
 
Tunasitisha sherehe za kumbukumbu ya Uhuru eti kubana matumizi !!
Mbona tunafuja mabilioni kwa. Chaguzi za hovyo za marudio za ubunge na madiwani ?
Tuache unafiki.....
 
Baada ya salamu hii Jiwe kabakisha sherehe moja ya mwakani baada ya hapo salamu za sherehe za uhuru za mwaka 2020 atatoa Mh. Bernard Camilius Membe
 
VITA YA KIUCHUMI NI NGUMU KULIKO ILE YA KUDAI UHURU
Wewe una akili mbovu sana! kwani aliyeusambaratisha uchumi wa Nchi hii nani? Kila tatizo mnasingizia vita ya uchumi! Siku hizi kila mara utasikia "vita ya uchumi" mara "uchumi wa kati" mara "wia ini ze raiti traki" pumbavu kila siku mnahadaa watu. Membe ndiyo dawa yenu mbwiga nyie
 
Tunasitisha sherehe za kumbukumbu ya Uhuru eti kubana matumizi !!
Mbona tunafuja mabilioni kwa. Chaguzi za hovyo za marudio za ubunge na madiwani ?
Tuache unafiki.....
Sijawahi kuona serikali ya kinafiki Kama hii ya Jiwe
 
Back
Top Bottom