Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,591
- 58,819
UCHAGUZI TANZANIA 2010
Jumuiya ya watanzania ugiriki inapenda kuitumia fursa ya uchaguzi uliofanyika 31/11/2010 kuelezea machache yafuatayo:
Jumuiya ya watanzania ugiriki inapenda kuitumia fursa ya uchaguzi uliofanyika 31/11/2010 kuelezea machache yafuatayo:
- Inatubidi watanzania popote tulipo tupongezane kwa kujikuta tunaendelea kupata maraisi kwa njia ya kura tangu tulipoungana 1964.Si siri kwamba mabalaa yanayotokea katika nchi za wenzetu wakati wa uchaguzi HAKUNA HATA MMOJA ANGEPENDA YATUTOKEE NCHINI KWETU.
- Busara na ushujaa uliotumiwa na viongozi wetu walioshindwa kuchaguliwa na wakaamua haraka kuwapongeza walioshinda ni dalili ya wazi kwamba TUNAPIGA HATUA KUELEKEA MBELE.
- Tunaelewa vizuri kwamba bado kutakuwa na wengine wataolaumu na kutuhumu kwamba uchaguzi ulikuwa na makosa na hata ulaghai, lakini hoja hizi haziwezi kuvunja ukweli usiopingika kwamba uchaguzi ulimalizika bila mabalaa makubwa yanayotokea katika nchi za wenzetu.HAKUNA kitu kilicho kamili duniani.Hata uchaguzi wa awamu ya pili ya GEORGE BUSH ulikuwa na matatizo na kasoro.Ni vizuri tuanze kujijengea ile hali ya kuangalia mengi mazuri na kuyapuuza mabaya machache.
- Mwisho, watanzania kuwa na vyama tofauti ni hatua nzuri kuelekea katika demokrasi. Isipokuwa itasikitisha na kukatisha tamaa kama watanzania tutakuwa tunafuata chama fulani na kuwaona wale wengine wasiokuwa katika chama chetu kama ni maadui.Hali hii itaturudisha nyuma na inatubidi sote kwa pamoja tuipige vita.