TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,835
Binadamu tumeumbwa na ipo siku tutarudi kwa muumba wetu, hatujui ni usafiri gani utakaotufikisha yaani namna pumzi yetu itakavyotutoka. Ajali iliyotokea ya gari la Gongolamboto ni pigo kubwa kwa ndugu jamaa na marafiki, kuna familia imebaki ukiwa, kuna walioondokewa na waume, wake, watoto na marafiki zao. Tuombee roho zilizotangulia zifike salama na kupokelewa na muumba wetu. Majeruhi tuwaombe wapate nafuu na kuendelea na mapambano ya kujenga uchumi wa familia na nchi kwa ujumla.
Hivyo kampuni ya TAECO kwa pamoja tunaungana na ndugu zetu kuwapa pole na kuwatia nguvu kwa wafiwa wote na Majeruhi wote.
Mungu alitoa na Mungu ametwaa jina lake lihimidiwe daima, Amina
Mtenga Gerald
TAECO LTD