Salamu za mwaka mpya: Jinsi gani tutaweza kujaribu kujipanga na mwaka ulioanza na kwa wengine utakaoanza

Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
3,974
4,733
mara nyingi tumezoe kusoma salamu za mwaka mpya kutoka kwa watu maarufu sana. safari hii basi tusome za kwetu ikiwa ni kushauriana ni kwa jinsi gani tutaweza kujaribu kujipanga na mwaka ulioanza na kwa wengine utakaoanza nadhani mmenielewa. kwangu kubwa napenda kuchangia zaidi kuhusu bajeti ya familia ambayo iwe kiini cha tafakari ya jinsi tutakavyoenda. katika kuangalia hili tutaangalia maeneo makubwa kama ifuatavyo:-
  1. matumizi muhimu (basic needs) hapa tunaangalia matumizi makubwa matatu
    1. chakula - hapa ni muhimu kujua kwa siku tunatumia kiasi gani kwa chakula cha familia hii ni pamoja na matumizi ya maji na kwa ushauri ili kupunguza bili za maji ni bora maji yasitumike moja kwa moja toka bombani bali yakingwe kwanza ndipo yatumike. na pia bomba la nje linaweza kuondolewa matumizi yote ya maji yakatoka ndani ili kuongeza mazoezi kwa wanafamilia lakini pia zoezi hili linapunguza bili kwa kiasi kikubwa kuna familia niliwashauri watumie maji badala ya kukinga bili ikapungua zaidi ya nusu.
    2. malazi-tunahitaji kutenga kodo kwa ajili ya nyumba na wale wenye nyumba waanze kutenga fedha ya kodi kulingana na nyumba wanayoishi ili kufikiria kuwekeza kwa kiasi wanachosave kwa kukaa kwao lakini kwa wale tusio na nyumba tuanze kufikiria ni kwa jinsi gani tuanze kujipanga kwa ujenzi kwa hali yoyote ile.
    3. mavazi- do! ile hali ya wanaume kuendelea kutolewa nguo zao kwenye kabati linaweza kuendelea lakini wake zetu punguzeni kununua nguo au mgawe baadhi ya nguo watu mmekaa na nguo miaka saba na hamzivai wakati wako wasio nazo. ni muhimu tukatengeneza bajeti kwa ajili ya mavazi kwa familia nzima
  2. matumizi muhimu lakini si ya lazima
    1. hakuna mtu anayeweza kufa kwa kukosa kwenda shule, lakini mtoto asiposoma jipange kumuhudumia mpaka mwisho wa maisha yako lakini tegemea kupata magonjwa msiyotegemea kama sukari na shinikizo la damu kwa stress za watoto.
    2. wageni na marafiki- wageni tunawapenda lakini mwaka huu mkija msikae sana kama mlivyokaa miezi mitatu mwaka uliopita na kizuri zaidi mlirudi mara tatu do! hivyo ni vyema tuanze kutengeneza bajeti kwa ajili ya wageni angalau tutegemee wageni wa kuishi si kwa zaidi ya siku tano na tunaweza kuwa na wageni 20 watakao kaa siku hizo na kila mgeni tukamkarimu kwa 7,000/- si haba. Pia mwaka huu hatukatazi msioe au msilewe ila michango yenu ya harusi mtutaarifu mapema na ikiwezekana msituweke kwenye kamati bora tuwape michango ya kawaida na muandae party simple nyingine fanyeni yenu sio kutulewesha na kutuweka kwenye kamati na mkala mpaka ada za watoto na matokeo yake tukalipa kwa malalamiko haikuji akilini michango tunalipa 2,000,000/- ada tunalipa laki saba kwa malalamiko.
  3. matumizi ya maendeleo ni muhimu na haya tunaweza kuyagawanya katika sehemu mbili
    1. matumizi ya samani za ndani na matengenezo-mhn! wake zetu mmeanza tena yaani sofa hazina hata miaka miwili mnataka tuzibadilishe? hapana mwaka huu tuanze msingi tufanye tuu marekebisho dia ila tununue kitanda kingine kwakuwa mtoto wetu wa kiume kakua si busara kuendela kulala na mdada wa kazi asije akajifunza halafu akaharibu.
    2. ni vizuri kufikiria kuanza ujenzi hata kwa kusafisha kiwanja na kununua matofari machache
baada ya kumaliza kuangalia jinsi gani tutatumia sasa ni vyema tuangalie ni kwa jinsi gani tutafadhiri bajeti ya hapo juu katika hili ni kuangalia vyazo vya mapato kama vinakidhi matumizi hapo juu na kama hayakidhi nini kifanyike? kwa kawaida viko vyanzo vifuatavyo tulivyovizoea kwa kufadhiri bajeti:-
  1. mshahara- kwa wale mnaofanya kazi mshahara unaweza kufadhiri karibu 52% ya bajeti ya familia lakini wake zetu msiwe wakali mwaka huu huwa hatuongi mshahara ila mruhusu asilimia 40% kugharamia kazi na refresher kiasi kwa bia mbili tu na nyama choma sio mnakaza kupita kiasi mbona ninyi saloon kila siku hatuwafuatilii muwe ladhi pia tukiwalipia wanawake wengine lunch kwakuwa hata nyie wako wanaume wenzetu wananunua lunch kwa ajili yenu na wala hawana nia mbaya kwenu na sio wapenzi wenu japo hamsemi kwetu ila tunavumila tu kwa kuwa tembo hashindwi kwenda kwa mkonga wake tutunzieni heshima hasa kipindi hiki tulichohamia Dodoma msijiongeze kupita kiasi.
  2. mikopo- hii ni pamoja na mikopo ya mishahara ambayo inaweza kutumika kwa ujenzi na uwekezaji wa familia siweze kueleza zaidi kwa kuwa wengi hamtaki kusoma vitu virefu.
  3. uwekezaji- hapa tuwe makini katika kuchagua, kupanga na kusimamia na ikiwezekana tuyajue haya kabla ya kuanza uwekezaji wa moja kwa moja muhimu tukazingatia simple business plan na ikiwezekana hata kama tukisaidiwa kutengeneza tuweze kuitafsiri ili tusianguke kibiashara.
  4. misada kwa ndugu na marafiki- tupo kutegemezana ifike wakati jirani akitoka kwao akikuletea mihogo tuione inathamani kwa kuwa anaweza kuwa amechangia zaidi ya 3,000/- kwa chai ya asubuhi sasa wakifanya mara 20 wamekuwezesha kiasi gani.
  5. kuokota na bahati nasibu- yapi si mfumo rasmi lakini ukitokea lazima tuweke kwenye matumizi.
ili kufanikisha hili ni muhimu tuanze matumizi ya diary na ikiwezekana tuwe na diary tatu ofisini kwa kazi za mwajiri, binafsi, na kwa familia ili kutunza kumbukumbu kwa uaminifu.
nisiwachoshe sana zaidi ni kuwatakia heri ya mwaka mpya wenye furaha huzuni zisiwe kwenu na kila aina ya uchungu iondoke kwenu mkono wa MUNGU ukawe juu yenu si kwa ajiri ya asra yake bali kwa huruma na utetezi wake kwa kuwa sikio lake sio zito lisisikie maombi yenu.
 
Back
Top Bottom