Salamu za David Kafulila siku ya Mei Mosi duniani

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
363
557
Nimependa kutoa maoni yangu eneo moja kuhusu maslahi ya wafanyakazi leo.

Wafanyakazi wa tanzania wanaumizwa sana katika kodi kuliko wafanyakazi wa nchi zote za afrika mashariki

Wastan wa kodi ya mfanyakazi Tanzania ni 18%, Uganda11%, Kenya 6.8%, Burundi 10.3 %na Rwanda 5.6%. ( global tax comparison report 2014-WB)

Wastani wa kodi ya mfanyakazi duniani kwa mujibu wa ripoti hiyo ni 16.2%. Kwa takwimu hizi sio tu kwamba wastani wa kodi ya mfanyakazi Tanzania ni kubwa kuliko nchi yoyote Afrika Mashariki bali ni zaidi ya wastani wa kodi ya mfanyakazi duniani.

Ikumbukwe chama tawala Tanzanja asili yake ni harakati za wafanyakazi na wakulima wadogo na ndio tafsiri ya alama ya jembe na nyundo kwenye bendera ya CCM. Hivyo ni aibu chama kilichoasisiwa na wafanyakazi leo kinaongoza kunyonya wafanyakazi kwa kodi kubwa kuliko nchi yoyote afrika mashariki.

Nashauri wafanyakazi waombe CCM iondoe nembo ya nyundo kwenye bendera yake kwani ni kejeli kwa wafanyakazi. CCM kwasasa ipo kwa maslahi ya wafanyabiashara wakubwa wasio waaminifu. Hao ndio wanafaidi uchumi kwa misamaha ya kodi na ukwepaji mkubwa wa kodi.

Ni maoni yangu kwamba kodi ya mshahara inapaswa kushuka kwa 50%. Itoke 18%mpaka9% wastani kwa kuanzia.

Kwa mujibu wa taarifa za TRA mwaka jana, tukishusha kodi hiyo kutoka wastani wa 18-9% tutapoteza mapato kiasi cha 704billion.

Ni maoni yangu kwamba mapato hayo yanaweza kufidiwa kwa kutekeleza sheria ya kodi ya majengo ambayo mpaka sasa utekelezaji wake ni 3% na tunakusanya 25billioni. Hii maana yake tukiteleleza kwa 100% tutakusanya zaidi ya 800billion.

Nawatakia heri wafanyakazi wote Tanzania siku hii muhimu.

David Kafulila(MB)
 
kujifanya una uchungu na wafanyakazi, mbona ulikuwa unachukua posho ya makalio ilihali bado mna perdiem hukusema kitu?
 
Back
Top Bottom