Salamu za ACT-Tanzania kwa vyama vyote vya siasa Nchini

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
608
1,540
View attachment 162796
SOTE NI WATANZANIA

Ndugu Viongozi wa vyama vya siasa nchini, wanachama wa vyama mbali mbali vya siasa nchini, wadau mbali mbali wa siasa nchini na watanzania wote kwa ujumla; tunapenda kuwasalimu kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi!

Chama cha ACT-Tanzania kinapenda kuwapa salamu hizi kufuatia wasi wasi ambao umekuwa ukioneshwa na baadi ya Viongozi wa vyama vya siasa, wanachama wao na hata washabiki wao juu ya ujio wa Chama kipya cha ACT-Tanzania.Kumekuwa na wimbi la baadhi ya watu kutoka vyama kadhaa vya kiaisa kulalamika kwamba eti chama cha ACT-Tanzania kimekuja kuwamaliza kisiasa.

Chama cha ACT-Tanzania kinapenda kutuma salamu kwa vyama vyote vya siasa nchini na wanachama wao kwamba; Chama cha ACT-Tanzania hakijaja Kuvimaliza vyama vyao wala kupambana na mtu yeyote wala chama chochote cha siasa nchini, bali kimekuja kupambana na matatizo sugu yanayomkabili mtanzania kupitia misingi, falsafa na itikadi zake.ACT-Tanzania imeanzishwa katika misingi yake yenyewe, Inajijenga katika misingi yake yenyewe,Itajiimarisha katika misingi yake yenyewe, Itatembea katika misingi yake yenyewe, Itasimama katika misingi yake yenyewe na kama ni kuanguka; basi itaanguka kwa kutokusimamia misingi yake yenyewe.Uwepo wa ACT-Tanzania hautegemei wala hautatagemea uwepo wa vyama vingine au operesheni za vyama vingine.Kwa lugha nyingine ni kwamba uwepo wa ACT-Tanzania hautategemea matukio bali misingi yake yenyewe.

Hata hivyo, kwa kuwa lengo kuu la ACT-Tanzania ni kupambana na matatizo sugu yanayomkabili mtanzania ambayo bado yanasumbua sana na kuleta machungu katika maisha ya watu, ili kuleta unafuu na furaha katika maisha ya mtanzania; lengo hili litafikiwa kwa ukamilifu wake kwa chama kupewa mamlaka ya kuiongoza nchi.Mamlaka hayo yatatoka kwa wananchi watakaoikubali misingi itikadi na falsafa za chama.Kwa kuwa katika uchaguzi chama kinachoshinda ni kimoja, ni wazi kwamba ACT-Tanzania itakaposhinda; vyama vingine vyote vitabaki kuwa vyama vya upinzani wakati ACT-Tanzania ikisimamia itikadi yake na ikitekeleza sera zake lakini hii haimaanishi kwamba ACT-Tanzania imekuja kuvipoteza vyama hivyo katika sura ya siasa za Tanzania! kwani hilo sio lengo la msingi la ACT-Tanzania.

Kadhalika tunafahamu kwamba kutokana na ubora wa falsafa, misingi na itikadi za ACT-Tanzania, Uwajibikaji,uwazi na uadilifu wa viongozi wa chama tulionao na tutakaokuwa nao, wanachama wengi kutoka vyama vyote nchini, watakuwa wakijiunga na ACT-Tanzania makundi kwa makundi.Hata hivyo hiyo haitakuwa inamaanisha kwamba tuna uadui na vyama wanakotoka wanachama hao.Tutafanya nini sasa! katika hali hiyo ndipo tunaposisitiza kwamba itatupasa tuwe na uvumilivu wa kisiasa.Tunawashauri wale watakaoona kwamba chama chetu kinafanya vizuri, wasitujengee uadui bali watuunge mkono au watuvumilie tu.

Kuhusu watu wanaotumia mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari kudai kwamba wao ni wana ACT-Tanzania, na chama hiki kimekuja kupambana na watu fulani fulani, nao wanasema kwa niaba ya chama! na watu wanaotunga habari na kudai zimesemwa na viongozi wakuu wa chama kwamba ACT-Tanzania imekuja kwa lengo kuu la kuua vyama vya watu fulani,Tunawaomba watanzania muwasamehe kwani kuna siku watajua kwamba wanachokifanya si sahihi na wakarudi kwenye njia ya ukweli na ustaarabu.

Mwisho, ACT-Tanzania kupitia Ofisi yake ya Mawasiliano na Uenezi, Inajenga na itaendelea kuimarisha mahusiano na vyama vyote nchini kwa kadiri itakavyowezekana kwani chama kinaamini kwamba sote ni watanzania na zaidi ya hapo sote ni watu.Chama kinakaribisha na kinapokea ushauri wowote kutoka kwa yeyote bila kujali chama chake, kitaupitia na kuuchambua na kila itakapoonekana unafaa, utafanyiwa kazi.Chama kiko tayari kushirikiana na yeyote anayependa ushirikiano katika mambo mema na yenye tija kwa taifa.ACT- Tanzania bado ndio chama kidogo zaidi nchini, hivyo badala ya kukiogopa; ni bora kukishika mkono ili kuimarisha demokrasia.Kadhaalilika Chama kupitia Ofisi ya Mawasiliano na uenezi, kitajenga na kuimarisha uhusiano na vyama mbali mbali duniani hasa vile vyenye muelekeo wa "Mrengo wa Kati Kushoto".

Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa ajili ya taifa la leo na kesho.

ACT- Tanzania ..............Taifa kwanza!,

Mabadiliko na uwazi...........Chukjua hatua!

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uenezi ya Dar es Salaam leo tarehe 05/06/2014.

Ni halmashauri ya kichwa chako wewe mwenyewe ndio yenye wasiwasi kama huo!! ACT is a non starter; ACT was still born. yaani kilikufa kabla ya kuzaliwa; RIP ACT
 
Katibu Mkuu wa ACT Samson Mwigamba amekiri ujio wa Muungano wa UKAWA umevuruga malengo ya chama chake.

Mwigamba amesema lengo kubwa la chama chake ni kuwaunganisha wananchi na kuwaeleza ubovu wa chama kikuu cha upinzani nchini Chadema.
 
kwa hiyo hamtaki aseme?
 
chadema imeshakufa mpaka ndoa na hiyo haina jipya ikivunjika cdm kwishinei inabaki act jamaa wako vizr mtaongea sana.mfa maji?.......?
 
Watanzania na hasa chadema acheni uoga ACT - Tanzania ndo kwanza wanajipanga ili waanze kufanya siasa nyinyi mnaweweseka, jamani mnaogopa kitoto kichanga. Tuwasubiri waje kwenye jamii tuwahoji mbona tunaanza kuwasemea. Fanyeni siasa acheni uzushi na ufitini.
 
Hiki chama ni kweli kitavuruga baadhi ya vyama lakini pia kitasaidia kuviimarisha vingine zaidi.

Mfano mzuri ni namna chama hiki kilivyosaidia kukiimarisha chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kwa kujitwika mzigo wa kuwachukua wanachama ambao walifukuzwa kwenye chama hicho kwa sababu za kihaini au usaliti uliopita kipimo.

Kwa wale wasiofahamu,samsoni mwigamba ambaye ni mmoja wa viongozi wa chama hiki,alibainika kuwa na hurka ya kisaliti na undimilakuwili misri ya nyoka mwenye vichwa viwili kwa kuwasifia viongozi wa chama ndani ya vikao wakati huo huo akipost maandiko ya kuwakashifu viongozi hao hao kwenye mitandao ya kijamii hasa jukwaa hili.kitendo hicho cha kishenzi kilipelekea akatandikwa makofi kama mtoto mdogo na mbunge tata wa arusha mjini bwana godbless lema a.k.a ngumi mkononi.

Hivyo hofu inayozungumzwa ni ya kweli kabisa,hasa kutoka chama cha mapinduzi ambako tayari kuna hofu ya kukosa pesa ya kujiendesha kutoka kwenye mashirika ya uma,baada ya kiongozi mwandamizi wa ACT kufungua kampuni mbili za gombe na leka ambazo zimeonyesha kuwa na weredi wa hali ya juu katika kujipatia mamilioni ya fedha kutoka kwa mashirika ya uma kwa ajiri ya kuendeshea chama hicho.

Hivyo si kweli kwamba chama hiki kina niA nzuri kwa vyama vingine.
 
Watanzania na hasa chadema acheni uoga ACT - Tanzania ndo kwanza wanajipanga ili waanze kufanya siasa nyinyi mnaweweseka, jamani mnaogopa kitoto kichanga. Tuwasubiri waje kwenye jamii tuwahoji mbona tunaanza kuwasemea. Fanyeni siasa acheni uzushi na ufitini.
waache wakalie kujipanga tu, wakati wenzao wanasonga mbele...
 
kwa nn nyie msijiunge na UKAWA basi ijulikane ni wapinzani au mjiunge na CCM mjulikane ni serikali...

View attachment 162796
SOTE NI WATANZANIA

Ndugu Viongozi wa vyama vya siasa nchini, wanachama wa vyama mbali mbali vya siasa nchini, wadau mbali mbali wa siasa nchini na watanzania wote kwa ujumla; tunapenda kuwasalimu kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi!

Chama cha ACT-Tanzania kinapenda kuwapa salamu hizi kufuatia wasi wasi ambao umekuwa ukioneshwa na baadi ya Viongozi wa vyama vya siasa, wanachama wao na hata washabiki wao juu ya ujio wa Chama kipya cha ACT-Tanzania.Kumekuwa na wimbi la baadhi ya watu kutoka vyama kadhaa vya kiaisa kulalamika kwamba eti chama cha ACT-Tanzania kimekuja kuwamaliza kisiasa.

Chama cha ACT-Tanzania kinapenda kutuma salamu kwa vyama vyote vya siasa nchini na wanachama wao kwamba; Chama cha ACT-Tanzania hakijaja Kuvimaliza vyama vyao wala kupambana na mtu yeyote wala chama chochote cha siasa nchini, bali kimekuja kupambana na matatizo sugu yanayomkabili mtanzania kupitia misingi, falsafa na itikadi zake.ACT-Tanzania imeanzishwa katika misingi yake yenyewe, Inajijenga katika misingi yake yenyewe,Itajiimarisha katika misingi yake yenyewe, Itatembea katika misingi yake yenyewe, Itasimama katika misingi yake yenyewe na kama ni kuanguka; basi itaanguka kwa kutokusimamia misingi yake yenyewe.Uwepo wa ACT-Tanzania hautegemei wala hautatagemea uwepo wa vyama vingine au operesheni za vyama vingine.Kwa lugha nyingine ni kwamba uwepo wa ACT-Tanzania hautategemea matukio bali misingi yake yenyewe.

Hata hivyo, kwa kuwa lengo kuu la ACT-Tanzania ni kupambana na matatizo sugu yanayomkabili mtanzania ambayo bado yanasumbua sana na kuleta machungu katika maisha ya watu, ili kuleta unafuu na furaha katika maisha ya mtanzania; lengo hili litafikiwa kwa ukamilifu wake kwa chama kupewa mamlaka ya kuiongoza nchi.Mamlaka hayo yatatoka kwa wananchi watakaoikubali misingi itikadi na falsafa za chama.Kwa kuwa katika uchaguzi chama kinachoshinda ni kimoja, ni wazi kwamba ACT-Tanzania itakaposhinda; vyama vingine vyote vitabaki kuwa vyama vya upinzani wakati ACT-Tanzania ikisimamia itikadi yake na ikitekeleza sera zake lakini hii haimaanishi kwamba ACT-Tanzania imekuja kuvipoteza vyama hivyo katika sura ya siasa za Tanzania! kwani hilo sio lengo la msingi la ACT-Tanzania.

Kadhalika tunafahamu kwamba kutokana na ubora wa falsafa, misingi na itikadi za ACT-Tanzania, Uwajibikaji,uwazi na uadilifu wa viongozi wa chama tulionao na tutakaokuwa nao, wanachama wengi kutoka vyama vyote nchini, watakuwa wakijiunga na ACT-Tanzania makundi kwa makundi.Hata hivyo hiyo haitakuwa inamaanisha kwamba tuna uadui na vyama wanakotoka wanachama hao.Tutafanya nini sasa! katika hali hiyo ndipo tunaposisitiza kwamba itatupasa tuwe na uvumilivu wa kisiasa.Tunawashauri wale watakaoona kwamba chama chetu kinafanya vizuri, wasitujengee uadui bali watuunge mkono au watuvumilie tu.

Kuhusu watu wanaotumia mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari kudai kwamba wao ni wana ACT-Tanzania, na chama hiki kimekuja kupambana na watu fulani fulani, nao wanasema kwa niaba ya chama! na watu wanaotunga habari na kudai zimesemwa na viongozi wakuu wa chama kwamba ACT-Tanzania imekuja kwa lengo kuu la kuua vyama vya watu fulani,Tunawaomba watanzania muwasamehe kwani kuna siku watajua kwamba wanachokifanya si sahihi na wakarudi kwenye njia ya ukweli na ustaarabu.

Mwisho, ACT-Tanzania kupitia Ofisi yake ya Mawasiliano na Uenezi, Inajenga na itaendelea kuimarisha mahusiano na vyama vyote nchini kwa kadiri itakavyowezekana kwani chama kinaamini kwamba sote ni watanzania na zaidi ya hapo sote ni watu.Chama kinakaribisha na kinapokea ushauri wowote kutoka kwa yeyote bila kujali chama chake, kitaupitia na kuuchambua na kila itakapoonekana unafaa, utafanyiwa kazi.Chama kiko tayari kushirikiana na yeyote anayependa ushirikiano katika mambo mema na yenye tija kwa taifa.ACT- Tanzania bado ndio chama kidogo zaidi nchini, hivyo badala ya kukiogopa; ni bora kukishika mkono ili kuimarisha demokrasia.Kadhaalilika Chama kupitia Ofisi ya Mawasiliano na uenezi, kitajenga na kuimarisha uhusiano na vyama mbali mbali duniani hasa vile vyenye muelekeo wa "Mrengo wa Kati Kushoto".

Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa ajili ya taifa la leo na kesho.

ACT- Tanzania ..............Taifa kwanza!,

Mabadiliko na uwazi...........Chukjua hatua!

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uenezi ya Dar es Salaam leo tarehe 05/06/2014.

Watanzania na hasa chadema acheni uoga ACT - Tanzania ndo kwanza wanajipanga ili waanze kufanya siasa nyinyi mnaweweseka, jamani mnaogopa kitoto kichanga. Tuwasubiri waje kwenye jamii tuwahoji mbona tunaanza kuwasemea. Fanyeni siasa acheni uzushi na ufitini.

Hatuna muda na hivyo vyama vya mifukoni vinavyoanzishwa katika misingi ya kilaghai! Act ni tawi la ccm lililoanzishwa na wasaliti wa mabadiliko kwa lengo la kuendelea kuchuma mapesa toka ccm!
 
Back
Top Bottom