Salamu nyingi tunazowasalimia wale tuliopoteana kwa muda huwa zinawaumiza pasipo sisi kujua

Ebu nipe mbinu jinsi ya kulijibu hilo swali maana huwa natamani kuchapa watu vibao nashindwa ni ndugu zangu wakubwa tu wanavoniuliza kuhusu kuhusu kuolewa kama mimi ndiye mzee mtaa mzima, i hate it
hayo maswali yanakera sana..mi nilimpa mtu jibu hilo mbele ya kadamnasi, kwahiyo hata wale ndugu zangu wenye viherehere wametulia tuliiii...I hate it too..!
 
Me nawajibugi kaa chini usubiri maana ukisimama utaumwa miguu kwa kusubiri, baada ya hapo nakwambia nisikilize kwa makini usirudie kumuuliza mtu swali kama hilo hujui mtu anapitia nini kwa wakati huo, kumuuliza swali kama hilo unamuongezea machungu na unaweza sababisha mtu akukosee adabu au akutukane,

Kuna siku tuko kwenye sherehe tuko na dada mmoja hajaolewa na ilikua send off ya mdogo ake imagine akaja mmama anamwambia enhee flani we unaoelewa mdogo wako ndo huyo anaolewa yaan unaona kabisa mtu ananyong’onyea anaumia moyoni sikuamuacha salama yule mama
Huyo mama adhabu yake anyolewe nywele kwa chupa...
 
Back
Top Bottom