Mwanga Lutila
JF-Expert Member
- Nov 10, 2016
- 3,954
- 12,913
Salamu za kumsalimia mtu na kuanza kumuuliza unafanya kazi gani, umeo/umeolewa au unawatoto wangapi? Nilishaziacha baada ya siku moja kuonana na Classmate ambaye hatujawahi kuonana kwa zaidi ya miaka 10 na nilisikia alishaolewa muda mrefu, nikaanza kumuuliza vip una watoto wangapi sahizi ? Alinijibu kwa huzuni sana "bado sijabarikiwa" niliyaona maumivu moyoni mwake kwa jinsi alivyonijibu.
Nafsi yangu ilinisuta kwanini nimemuuliza?
Ninaandika nimeona mtu anasalimiana hivyo na mwenzie waliopoteana kitambo, swali la una watoto wangapi lilionekana kumuumiza kwa jinsi alivyojibu.
Tukikutana na wenzetu hizi salamu hazna maana.
Zinabakia kuwa maumivu tu na kujiona kama wapo nyuma wamechelewa maisha.