SALAMU Mpya za CHAMA CHA MAPINDUZI ( Zaweza kutumiwa hata na wapinzani) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SALAMU Mpya za CHAMA CHA MAPINDUZI ( Zaweza kutumiwa hata na wapinzani)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtaka Haki, Mar 25, 2012.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa tumekatishwa tamaa kuwa ni KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI kufanya mapinduzi ya kweli yenye lengo la kuweka hali sawa kwa faida ya taifa.

  Na imekuwa wazi kuwa NI NGUMU FIKRA ZA MWENYEKITI za kuvua gamba kutimia. Hata zikitimia kule kusua sua kwenye kufanya maamuzi ya haki ya kujisafisha kumeleta aibu juu ya udhati wa FIKRA HIZI. Gamba lililokuwa limesemekana lingevuliwa ndani ya kipindi kifupi limekuwa gamba la KOBE.
  UFISADI umeshinda na zimeendelea kuwa ngumu fikra za mwenyekiti wangu kwa sababu kansa ya rushwa imeshakuwa ni kawaida na sidhani kama ana watu wa kutosha wanaomuunga mkono ndani ya chama juu ya kuupinga ufisadi. Huu ungekuwa ni wakati wa kuchukua ushauri wa Lowassa kuwa maamuzi yafanyike hata kama yataweza kuwa sio the best.

  Kama hata suala la RADA na ushahidi mkubwa uliokuwa umetolewa bado imeshindikana kufanya lolote basi nimekatishwa tamaa.
  Siasa ya UJAMAA na kujitegemea imegeuzwa na wapenda rushwa na ufisadi kuwa SIASA YA UNYAMA NA KUJITEGEA. Kama nilivyowahi kuwasikia baadhi ya watu wakiita.
  Watu wanafanyiana visa na mitego. Rushwa aliyekuwa adui wa HAKI sasa amekuwa rafiki wa viongozi wa Siasa.

  NI KIGUMU KUCHUKUA MAAMUZI, NI NGUMU KUONA KUWA DAWA NI KUWACHUKULIA HATUA WAHALIFU NA KUSIMAMISHA HAKI. HAKI IKITOWEKA AMANI INATOWEKA. NI NGUMU SIASA YA unyama na kujitegea inayoendelezwa. Wengi wamenaswa katika siasa ya kujitegea sasa inaendelea siasa ya KUNYAMAA NA KUJIMEGEA.
  KIWIRA,
  TANGOLD
  EPA,
  NDEGE YA RAISI
  RADA,
  TAFADHALI ongezea

  HIVYO SALAMU MPYA NI KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI - Wanaitikia KIGUMUUU
  Ni Ngumu fikra za mwenyekiti za kuvua Gamba ni Ngumuuuuuuuu - ni kama gamba lenyewe.
  Ni Ngumu siasa ya Unyama na Kujitegea Ni ngumuuuuuuu - Tuliowategea na kuwafanyia unyama wamepeta.
  Ni ngumu siasa ya Kunyamaa na Kujimegea - Ni Ngumuuuuuuuu - wapinzania wanatuchachafya na waliokosa kumegewa wanatusaliti.
  KWA HIYO ACHANENI NA CHAMA CHETU kina wenyewe tafuteni chenu.
   
 2. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sawa kaka....
   
 3. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Hivi CCM kipo kwa maslahi ya nani ?
  Kama ni genge la mafisadi na vibaraka wa wanyonyaji basi ijulikane wazi.
  Wananchi hawana sauti wala thamani.
  Wananchi wamekufa na mifugo yao na mazao yao kwenye migodi ya dhahabu na kuachiwa mashimo, wamekufa mgomo wa madaktari, mpaka sasa hospitali hazina vifaa, wananchi wanaendelea kufa kwa bidhaa feki, ufisadi, na udhalimu wa vyombo vya dola.
  Nape, Hivi CCM kipo kwa maslahi ya nani ?
  Wana JF, Hivi CCM kipo kwa maslahi ya nani ?
   
 4. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
   
 5. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Nchi yetu inazingatia utawala wa sheria, tuhuma ambazo hazina ushahidi hata kama ni za kweli haziwezi kumtia mtuhumiwa hatiani, labda iwe nchi ya kidikteta. mafisadi wachache hawatoshi kuwajumuisha atu wote ndani ya Chama na Serikali na kubadilisha salamu ya Chama hasa ukizingatia kuwa tayari wengi wao wameshakaa pembeni na kukiacha chama kisonge mbele.
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
   
 8. g

  glojos88 Member

  #8
  Mar 26, 2012
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kwa kuwa nchi inazingatia utawala wa sheria. Watuhumiwa wangepelekwa kwenye vyombo vya sheria. Hivyo kama watu wanatuhumiwa na hakuna lolote linafanyika hadi Uingereza waone kuna kesi ya kujibu huoni kuna kitu kimepunguka?
   
 9. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I agree, utawala wa sheria hauwaachi watuhumiwa na kusema hakuna ushahidi. Unaposema hakuna ushahidi wakati unayesema sio chombo cha sheria huko ndiko kukiuka utawala wa sheria. Mahakama na polisi ndio wenye haki ya kudai ushahidi.
   
 10. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM ipo kulinda maslahi ya walioweza kuiba na kuharibu uchumi wa nchi hii.
   
 11. g

  glojos88 Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salamu hizi zianze kutumika Leo Kwenye mkutano wa Shukrani USA river
   
 12. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadharia yake imeonekana.
   
 13. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,183
  Likes Received: 1,184
  Trophy Points: 280
  unamfaham mmiliki wa dowans lakini?
   
Loading...