Salamu kwenda kwa baba wa kaya aliyetangulia mbele ya haki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salamu kwenda kwa baba wa kaya aliyetangulia mbele ya haki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Jan 26, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwako baba wa kaya,
  Salaam nyingi zikufikie,sisi wajukuu zako tu wazima tunapumua japokuwa hatuna uhakika wa siku moja katika mchakato wetu wa kutafuta riziki.Tunakukumbuka kwa mengi,kiasi cha kuweka hotuba zako mara kwa mara japokuwa hatutekelezi kwa vitendo kwani aliyekwenda amekwenda.Tumekuwa mabingwa wakutoa mifano kwa nukuu zako japo hatutembei ndani ya maneno yako.Vipi hali ya uko ulipo,je ni kweli umetuandalia makao?

  Hali ya kaya kwa sasa baba inatisha sana,nakuita baba japokuwa wewe ni babu,ila kutokana na sifa lukuki ulizotunukiwa wakati wa uhai wako na maono uliyokuwa nayo juu ya mstakabali wa kaya yetu unastahili kuitwa baba wa kaya.Hali ya maisha imekuwa ngumu kupita maelezo, wanakaya wenzako uliotuacha tunaishi chini ya dola moja.Matendo ya kujinyonga yamekuwa si kwa wenzetu wa Iringa tu bali kila kona watu wanatumia ujasiri wa Mkwawa kuliko kupambana na adui yetu mkuu maisha magumu.Mpe salamu nyingi sana tena mshirikishe kwa kumwambia salamu toka huku kwenye kaya yetu ni kuwa uzalendo aliotuachia tumeushindwa,tunawakaribisha wakoloni kuchukua ardhi yetu na rasilimali zetu bure bila hata jasho,tukiimba kuwa ni wawekezaji waliokuja kuikomboa kaya yetu.

  Ule mfumo wa elimu uliotuachia,umepotea hauna tija katika kaya yetu,ila tumepiga hatua kidogo tuna shule za shina ambazo hazina miundo mbinu ya elimu.Mwambie Mh Kabeho,kilichobaki kwa sasa katika elimu ni vurugu tupu.Elimu imekuwa biashara tena wanatumia msemo usemao" if you think education is expensive try ignorance".Hata zile shule za kaya ulizotuachia tukajifunia siku hizi zimekuwa historia tu.Wakubwa kama ulivyokuwa ukipenda kuwaita, watoto wao wanasoma ng'ambo,wanaandaliwa kuwa wakuu wa kaya utaratibu ambao haukuuwacha.

  Rushwa ndani ya kaya imekithiri kwa kiwango ambacho haijawahi kutokea,hakuna wakukemea.Naamini ikitokea ukarudi ghafla unaweza usipelekwe tena kwa wakoloni kufia huko,utakufa hapa hapa kwenye kaya yetu kwa hofu juu ya wana kaya wako.watendaji wa kaya wanawaogopa wa rushwa ambao siku hizi tunawaita mafisadi, wanasema wakiwakamata nchi itatetereka kiuchumi.Siku hizi ukiiba mali ya umma unaambiwa urudishe bila hata riba,wakati juzi mtoto mmoja wa mwanakaya mwezetu aliiba kuku akafungwa miaka saba.

  Wale maadui zetu(makaburu) upande wa kusini mwa kaya yetu, tuliwaimba vibaya na kusema maneno mabaya juu yao,kwa nyimbo tulipokuwa JKT na mashuleni ndo leo wameshikilia uchumi wa kaya yetu.Nakukumbuka kwani siku mmoja ulitahadharisha juu ya kuuzwa kwa kila kitu ndani ya kaya tena ukasema waache watoto watasoma na kupata elimu ya kutosha kuendesha rasilimali hizo, lakini maneno yako yalipuuzwa mara tu ulipotwaliwa.Mshukuru sana muumba maana bila hekima yake ya kukuchukua mapema, ungegongwa na gari na kupata ulemavu ambao ungekusumbua sana hasa ukizingatia tuna mgomo mkubwa wa madaktari.

  Migomo kila sehemu ndani ya kaya,kama kuna laana uliotuachia wajukuu zako tunaomba utusamehe,maana fikra zetu kwa sasa zimefika kikomo.Kila idara ndani ya kaya inagoma,wakuu wa kaya wapo lakini masikio wametia pamba.Cha ajabu hata kile chama hatamu ndani ya kaya nacho kimeacha misingi na madhumuni ya chama,kwa sasa si chama cha wakulima na wafanyakazi kama falsafa yako ilivyoamini.Kwasasa ni chama cha wenye minoti na taama ya kutumia dhamana ya madaraka watayopata kuchumia matumbo yao hali iliyopelekea ugomvi ndani ya chama kushika hatamu.Huwezi amini hata mwanafunzi wako uliyemchapa kiboko kimoja tu wakati anasoma,naye alipata uwendawazimu aw kujilimbikizia mali mwezi mmoja tu mara baada ya safari yako ya mwisho.Hata yule jamaa uliyemwita boys two men eti naye amekuwa mkuu wa kaya,kinachofanyika mauzauza matupu.

  Kuna vyamai ulivicha vikiwa na nia ya kushika madaraka ya kaya,lakini mpaka leo hii havijafanikiwa japokuwa vinajitahidi lakini ikifika wakati wa kuchaguana vinadai vinachakachuliwa,msemo huu wakati unaondoka hakuwepo,ina maana vinaibiwa kwa kutumia lile lile geshi letu la borisi uliotuachia.Ila kikubwa ambacho wanakienzi mpaka leo ni ule utaratibu uliotuachia wa kulindana hata kama umeharibu, isipokuwa wameongezea kauli mbiu moja inayosema waacheni wazee wapumzike

  Baba wa kaya naomba leo niishie hapa muda hautoshi ningekujuza mengi juu ya kaya yako uliyoiacha ambayo kwa sasa imepoteza heshima mbele ya kaya zingine.Mabwana wakubwa uliokuwa unawapinga kiasi cha kuwa na msimamo wa kaya yetu kutofungamana na upande wowote sasa hawana tena upinzani,wanaidhihaki kaya yetu eti imekuwa Matonya kama vile tunatoka vitani.Msalimie sana Rashidi mwambie sasa hivi, tekenolojia imeongezeka ndani ya kaya yetu,tunaagiza yebo yebo badala toka China,tumeacha utamaduni aliotuachia wa kuvaa matairi ya gari.Wasalime wote bila kumsahau Amiri Jamal mwambie nafasi yake imeshikiliwa na mwana morogoro mwenzake aliye prove failure.Na mwisho kabisa mkuu wa kaya hii kwasasa, hajui kwanini wanakaya wake ni masikini wakati kaya imezungukwa na rasilimali nyingi

  Wako mjukuu
   
Loading...