Salamu kwa PENGO, MALASUSA na mufti mkuu!!

Hofu zilizopandikizwa ndani ya watu ndizo zilizorahisisha utawala wa wakoloni kudumu miongoni mwa jamii ya kiafrika. Ndugu zangu tusiogope viongozi wa dini bali tumuogope MUNGU. Kwani ni nani asiyejua jitihada za Lowasa kujisafisha kwa mgongo wa dini? Mi ningekua kiongozi wa dini hata nisingemkaribisha kwenye maswala ya dini kwa sababu bado hajajibu kashfa ya richmond na hivyo pesa aliyo nayo ni najisi na inachafua madhabahu ya mungu. Viongozi wa dini waache njaa kali kwani lowasa kwa sasa anatuhumiwa ni mwizi na hajajibu tuhuma. Arudishe kwanza alivyoiba ndipo labda asamehewe,. la sivyo yeye bado ni mtumishi wa shetani.
 
kuna watu wanadhani ukiwa muumini hutakiwi kufikiri, yaani unaacha inteligence nje unaingia kanisani kama debe tupu!!!unatakiwa kumtumikia Mungu kwa akili zako zote sio kwa liframe la mwili tu. viongozi wa dini wanatakiwa kuwa kwenye msitari, akipinda tu mpigieni kelele ajirekebishe sio kumuogopa. tuliwaacha akina KILAINI wanabwabwaja ooh chaguo la Mungu Chaguo la MUNGU wapi bwana weee? sasa hivi cha moto tunakiona na yeye kanyamaza kimya, angekuwa msitaarabu angesema/angewithdraw statement yake kabla ya 2010 general election kuwa alikosea kumsemea MUngu uongo na watu wanaomuamini sana wangefanya uamuzi wa busara sasa kumchagua mtu anayefaa. halafu wengine wanataka tuendelee kunyamaza. kuna viongozi wa dini ktk makanisa madogo madogo haya wamekuwa mashetani kabisa...wanatoa rushwa kama kawaida, kaulizeni morogoro mtajulishwa ukweli. hawana utofauti na wachungaji wanaosema neno la Mungu limehamia kwenye mti hivyo watu waanze kuabudu miti ili wapone magonjwa(loliondo)...tusipowasema mbona watakuja kuchoma moto miumini isiotaka kutumia akili! this timeTunamuambia LOwassa and company kuwa hatudanganyiki!!!!hakuna cha 6 wala kelango wala mwamwembe na mwenzao ole something..so long as wako ccm they are not clean . tumewafahamisha kwa vitendo KIRUMBA na KIWIRA na Ole sendeka amekiona hukohuko ARUMERU east. sasa matumbo moto kwa maana jimbo la Ole sendeka bado tunahesabu liko wazi,la Ole medeye liko wazi, la Nagu, la Dk wa biashara moshi vijijini.....baadaye tutamalizia upande wa huku Same n.k....vijana wako vyuo vya mafunzo sasa hivi wakitoka huko ni moto kuliko Joshua Nassari. mark my words
 
Mtoa maada,uyasemayo ni kweli kw namna fulani lakini kuna askofu katika gazeti la mwanahalisi la jumatano ya leo limweka wazi msimamo wa Pengo kuwa hakubaliani na Lowasa kutumika katika kanisa.
 
Hofu zilizopandikizwa ndani ya watu ndizo zilizorahisisha utawala wa wakoloni kudumu miongoni mwa jamii ya kiafrika. Ndugu zangu tusiogope viongozi wa dini bali tumuogope MUNGU. Kwani ni nani asiyejua jitihada za Lowasa kujisafisha kwa mgongo wa dini? Mi ningekua kiongozi wa dini hata nisingemkaribisha kwenye maswala ya dini kwa sababu bado hajajibu kashfa ya richmond na hivyo pesa aliyo nayo ni najisi na inachafua madhabahu ya mungu. Viongozi wa dini waache njaa kali kwani lowasa kwa sasa anatuhumiwa ni mwizi na hajajibu tuhuma. Arudishe kwanza alivyoiba ndipo labda asamehewe,. la sivyo yeye bado ni mtumishi wa shetani.

Tatizo hapa ni either kutojua mafundisho ya dini hasa kikristo yanayohubiri UPENDO na MSAMAHA! pamoja na kuwa EL ana skendo mbalimbali au tuhuma nafikiri sio sababu ya viongozi kumfungia milango, kumbuka Yesu hakuja kwa ajili ya waliowasafi ila wenye dhambi wapate kutubu na kuungama or ukosefu wa elimu ya biblia kwani kuhusu matamasha ya makanisa hata Yesu alihudhulia matamasha yaliyokuwa na wadhambi kama makahaba na watoza ushuru hadi walimkaribisha nyumbanimwao kumbuka ZAKAYO!

Nachokiana hapa ni baadhi watu humu wanaojiita magreat thinker kuwa na tabia za MASADUKAYO NA MAFARISAYO! sikubaliani na siasa za EL ila sikubaliani na watu wanataka kuaminisha watu kuwa huyu jamaa anabebwa na viongozi wa dini!

Hii ingeleta maana kama Pengo, Malasusa au Issa bin Simba walishasimama kwemye mimbari zao na kusema EL ni msafi ametakaswana kanisa au msikiti wao vinginevo kila mtu aangalie nini ni nini na nani ni nani katika ujenzi wa taifaletu! mie najua maaskofu waliowengi hususani waliotajwa humu wanajua CCM na wanaCCM ni nini!
 
Tatizo hapa ni either kutojua mafundisho ya dini hasa kikristo yanayohubiri UPENDO na MSAMAHA! pamoja na kuwa EL ana skendo mbalimbali au tuhuma nafikiri sio sababu ya viongozi kumfungia milango, kumbuka Yesu hakuja kwa ajili ya waliowasafi ila wenye dhambi wapate kutubu na kuungama or ukosefu wa elimu ya biblia kwani kuhusu matamasha ya makanisa hata Yesu alihudhulia matamasha yaliyokuwa na wadhambi kama makahaba na watoza ushuru hadi walimkaribisha nyumbanimwao kumbuka ZAKAYO!
Unakosea sana unapomlinganisha EL na makahaba na watoza ushuru!! Yesu alikuwa anawaambia watoza ushuru wauze vyote walivyonavyo, waache vyote wamfuate. Sasa EL kahujumu uchumi wa Taifa na bado anataka kuendelea kujijenga kisiasa. Ni dhambi kubwa kumtetea Lowasa. Halafu yesu aliwafuata na wala wao hawakufanya kinafiki kama Lowasa anavyowarubuni hawa wa sasa. Yesu hakufuata wenye dhambi waendelee kuishi na dhambi bali alitaka watubu na kuanza maisha mapya ya utakatifu.
 
Back
Top Bottom