Salamu kwa Mjomba

Said S Yande

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
874
637
MJOMBA #SALAMU

Katika nyakati Kama hizi mjomba tunakumisi sana kwani ulitufahamu vyema. Na hata tulipoandamana hukutupiga mawe au risasi Bali ulituita tuongee hatimaye tupate mwafaka.
.
#Mjomba Tulikutania, ukawa mtani wetu hata shemeji zako ukawapa neno lenye busara nyingi ndani yake. Pale ulipoona hamna namna ulisema wazi japo hukusema "msemakweli Ni mpenzi wa Mungu"
.
#MJOMBA, wewe uliamini kuwa #CHAKULA NI #BORA KULIKO #RELI. hukuchukua chakula chetu ukajengea bwawa la maji Bali ulitupa unga nao watoto na wazee wetu wakashiba.
.
#MJOMBA, kila ulichosema ulitimiza. Wala haukuwa kigeugeu. Pale wanao tulipokuomba #MKATE ULITUPA MKATE NA SIYO AHADI HEWA kila mwaka. Mjomba ulikataa kufananisha tonge la ugali na kiatu Cha mguuni. Ni wewe uliyeamini kwamba GIZA NA MWANGA HAZIWEZI KUCHANGANYWA. Tena ulisema KAMWE good and bad can't be confused.
.
#MJOMBA kweli ulienda sawa na JK wa kwanza kwamba WATU Ni MUHIMU KULIKO NCHI YENYEWE kwani hakuna nchi bila watu. Lakini pia hukuacha kutufundisha kutumia rasilmali kwa matumizi endelevu ili vitukuu vyetu vifurahie maisha Kama sisi.
.
#MJOMBA tunakuomba utupe Siri . Hivi Ni kweli nchi haina shamba? Kwani mjomba wewe ulikuwa unatoa wapi chakula ulichotugawia wakati mmoja wetu alipokumbwa na njaa?
.
#NDUGUMJOMBA ILE #MISHAHARA uliyokuwa unaongeza unaipata wapi?? Au wewe hukuhangaika na ujenzi wa nchi ndiyo maana ukawa na pesa za kutosha?? Wazee wetu watangulizi nao watuambie mbinu waliyotumia ili nasi tuishi bila ngoja ngoja iumizayo matumbo...
.
#NACHELEA KUKUITA MJOMBA, YAFAA TUSEME WEWE NI BABA AMBAYE ULIJUA KUWAPA WANAO VIPAWA VYEMA. NA PIA ULIJUA KUTENGANISHA #MGONGO NA #TUMBO kwamba haviwezi KUCHANGANYWA.
.
Mungu aendelee kukuweka MJOMBA

NAenda Msoga
 
yebaba
IMG_20190502_004338.jpg
 
Kikwete aliposema mtanikumbuka, alikuwa anajua chaguzi la mrithi wake atakuwaje, ndio maana akamchagua JPM kuliko wasomi wote
 
Jiwe aliandaliwa kuchukua nafasi bila yeye mwenyewe kujua...mjomba alijua na ndo maana alituonea huruma
 
Back
Top Bottom