Salamu kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Passport za Tanzania zinakimbilia mikononi mwa wageni kupitia viongozi waandamizi na askari

Sijasoma yote Ila wewe jamaa inaonekana ni mzalendo kwerii kweriii.. kuna sehemu nilipita huko Kagera , wanyarwanda wamepata NIDA kibaoo, na wanajitambilisha kuwa wao ni watz wa kuzaliwa
Unajuaje kama ni wanyarwanda?watu wa mipakani kagera,Kyaka,mtukura,mlongo border au Karagwe,kwa kuwaangalia usoni,huwezi kuwatofautisha na raia wa nchi jirani.
Na inapokuja Swala la uraia kwanini watu wa kagera wanakuwa wahanga?kwanini wamasai,waluo,au wamakonde hawazungumziwi?hakuna tofauti kati ya mmasai wa TZ na Kenya
 
kwa kweli wewe ni mzalendo kweli kweli.rushwa katika nchi hii imetamalaki kweli kweli na si taasisi hizo tu ulizozitaja bali ziko nyingi.kagera ni sehemu tu ya mkoa ambao unao wageni wengi kweli kweli hata ukiwaangalia tu kwa sura zao utajua si watanzania.nenda kigoma mpaka maofisini wamejaa wageni kibao na hatujui huu mzaha watz utatupeleka wapi.ukiingia kwenye mabaa na maloji ya kageara wamejaa wakenya,watusi,warundi nk pia kigoma warundi wamekodi mpaka vyumba vya kulala wageni wanafanya biashara za ngono.nenda pia arusha wageni wamejaa.nchi hii rushwa imekithiri kweli kweli na mbaya zaidi wakubwa ndo mawakala wa hao wageni.kwa kweli ni kumwomba Mungu watu hao wawe na nia njema sababu huwezi kwenda mkoa wowote hapa nchini bila kuwakuta wageni na wengine wakishapenya mipakani wanakwenda moja kwa moja kujichanganya kwenye mikoa mikubwa kama dar,arusha,mwanza,nk.na watu hawa hutumia pesa nyingi kupata hizo huduma na kuna wanasheria wachache wanaoshirikiana na watu hawa ili kupata huduma hizo.Mungu ibaliki tanzania tuwe na wazalendo kama wewe.
 
Unajuaje kama ni wanyarwanda?watu wa mipakani kagera,Kyaka,mtukura,mlongo border au Karagwe,kwa kuwaangalia usoni,huwezi kuwatofautisha na raia wa nchi jirani.
Na inapokuja Swala la uraia kwanini watu wa kagera wanakuwa wahanga?kwanini wamasai,waluo,au wamakonde hawazungumziwi?hakuna tofauti kati ya mmasai wa TZ na Kenya
inawezekana hata wewe ni mgeni na si mtanzania.kiswahili kinakutambulisha kuwa wewe si mtanzania.kagera ni mojawapo ya mikoa victim kwa wageni.hizo sehemu unazozitaja tunazijua sana,kyaka,mutukula,karagwe kote huko wamejaa wageni.hata ukiwa zuzu namna gani lazima utawashitukia tu.njoo hapa bukoba mjini uone wageni walivojazana kwenye mahoteli,mabaa tena hata ukiwauliza wako very free kusema mm ni mganda,mnyarwanda nk na wala hawajifichi.nenda pale liquid,the mint,sky way,miembeni kuna wadada wanajiuza mchana kweupe na wengi wao ni wa nchi jirani hala wewe unakanusha nn.humu ndani tuko wengi na tunajua mengi na tumekutana na mengi ktk pita pita zetu.
 
Tanzania imezungukwa na maadui wengi kuliko marafiki, Tanzania imezungukwa na nchi zisizo na amani kama taifa letu. Ulinzi wa Tanzania upo mikononi mwetu Watanzania. Tusiposema hakuna atakayesema Kesho Wala Kesho kutwa. Nchi yetu imevamiwa Sana na wageni wanaotaka kuifanya nchi hii ni Mali Yao. Naamini nisipomwambia Kamishna Mkuu kuhusu Hali hii ntakua simsaidii, nisipomwambia Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Hali ilivyo mtaani may be wataingia wabaya nchini na wataishambulia nchi nakuumiza hata ndugu zangu naomba niseme. Yawezekana ninayoyasema anayajua au ni mapya kwake ila yatasaidia Taifa.

Kabla sijasema nikiri kwamba Mimi ni mtoa huduma za kisheria, Katika kutoa huduma za kisheria ndipo nilipokutana na haya nitakayoyaeleza hapa ambayo naamini yanamsaada mkubwa Kwa ulinzi wa nchi yetu,ulinzi wa afrika mashariki na ulinzi wa Dunia Kwa ujumla wake. Hivyo naomba anaposoma Kamishna Mkuu wa Uhamiaji basi asisome peke yake wasome Watanzania wengi na watakapoona visa vya aina hii waweze kuripoti wahusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria. Hizi ni true stori ambazo zimepita mikononi mwangu na mikononi mwa watoa huduma ya kisheria wengine, hakuna aliyechukulia serious au kama walichukulia serious basi awakufikisha ujumbe panapohusika.
Kati ya mwaka 2015 Hadi Sasa nimetoa huduma Kwa wateja wengi nikianzia Mwanza, nikaenda Mbeya, nikahamia Dar na Sasa nipo Kilimanjaro. Kupitia huduma hizo naomba kueleza madhara ya huduma hizi kwa Taifa letu na kwa Mataifa mengine
1. Huduma ya utoaji wa kiapo Cha kuzaliwa: Hii huduma inatolewa na Mawakili wengi na ni huduma ipo kisheria lakini huduma hii usipoifanya Kwa uadilifu madhara yake ni makubwa sana. Mwaka 2016 alifika mteja anatafuta kiapo kwangu, Mteja huyo alikua na maneno machache Sana ya kiswahili na mengi ya kiingereza, alikua anatafuta kiapo Kwa ajili ya pasipoti; nilipomhoji kuhusu majina yake,majina ya wazazi na majina ya watakao shuhudia kiapo alionekana dhahiri kwamba anatunga majina hivyo kumtilia mashaka. Nilipombana zaidi na kumweleza umuhimu wa kusema ukweli alikiri yeye ni raia wa Kenya ila amakuja nchini kufuatilia pasipoti, familia waliyofikia wakiwa watu wanne wanawasaidia kupata pasipoti na kwamba wenzake wote wamepata yeye amekwama kiapo. Nilikataa kumpa huduma na kumwacha aondoke Kisha kuwasilisha taarifa zake na za Ndugu zake ambao alidai wanapasipoti Uhamiaji ya karibu nisingependa kutaja jina; baada ya kuwasilisha taarifa zile nakuchukua namba za simu za afisa Kwa ajili yakupeana taarifa zaidi nilikuja kubaini kwamba kesi Ile imeingiliwa na watu flani wakubwa wanaofanya kazi wizara ya mambo ya ndani hivyo suspects wakapata mtetezi kutoka juu. Kwanini nimeandika hii stori, nimeandika baada ya kukutana na Mteja yuleyule aliyekiri kwangu kwamba ni raia wa Kenya Uhamiaji Dar es salaam akiwa anafuatilia siyo pasipoti mpya tu bali anabadilisha apewe ya kielekroniki. Kibaya zaidi treatment yake ilikuwa ni VIP kwa sababu wakati wengine tunasubiri yyeye aliingia Moja Kwa Moja nakukamilisha huduma nikasikia anaelekezwa kwenda Kurasini means ana mtandao mkubwa. Nilitamani kuwajulisha maafisa wawe makini lakini nilisita kukwamishwa mimi yeye akapita na sikupenda kujipnyesha kwake. Kwa tafsiri nyingine yupo mtumishi wa serikali aliyezuia huyu bwana kuchunguzwa uraia wake, yupo wakili aliyemtengenezea kiapo na wapo Watanzania nyuma yake waliojitolea kumpokea na kuruhusu atumie majina ya familia Yao. Lakini je wakati haya yanafanyika nani anajua dhamira za wageni hawa kutafuta pasipoti za Tanzania? Kwanini wabadili majina? Wana athari gani kwa kesho ya Tanzania? Kamishna tulindie nchi yetu simu zenu wakubwa wakati mwingine zinapeperusha wahalifu

2. Nikiwa Arusha nilikuta kesi Moja ofisini ambayo wahusika walioomba msaada wa kisheria walikuwa Dar es salaam. Katika kuwasikiliza nilipobaini ukweli nilijitoa bila kusema Kwanini nimejitoa. Story Yao Kwa ufupi ipo hivi; Wana asili ya Somalia, baba na mama waliingia nchini miaka ya 1970 wakiwa na pasipoti za Somalia. Walipokelewa na kaka Yao ambaye pia alikuwa Msomali. Miaka ya 1980 wenyeji wao wakafanikiwa kupata pasipoti za Tanzania na kwenda Ulaya. Wao pia wakatafuta pasipoti na kupata pasipoti lazima wawe na cheti cha kuzaliwa. Nilisikitika kusikia waliweza kupenyeza rupia wakapata vyeti vya kuzaliwa wazazi na watoto kipindi hicho hicho wakiwa tayari wanaishi kwa karatasi za kufanya kazi za uhamiaji. Baadaye walifanikiwa kupata pasipoti na watoto wao, nusu wakaenda ulaya na nusu wakabaki Tanzania. Mwaka 1995 Mzee wao akakamatwa Kwa Tuhuma za kugushi na kujipatia nyaraka( means yupo mtu aliwatonya Uhamiaji kwamba familia Ile siyo Watanzania) wakapanchi wakafunga uchunguzi bila uchunguzi. Siku wanakabidhiwa kwangu nakueleza stori hii ndipo nikabaini mambo yafuatayo.
I. Familia hii tayari ilishaingiza nchini ndugu zao wengi na wote kupitia cheti cha kuzaliwa Cha mwaka 1980+ wamefanikiwa kujitanabaisha kama wazaliwa wa Tanzania. Kila wakitaka cheti wanatoa copy vile vyeti vya awali na kuambatisha Kisha RITA wanatoa vyeti kama wazaliwa wa Tanzania. Kwanini wakieleza ukweli? Ni kwa sababu katika Tuhuma zilizokuwa zinawakabili tayari mamlaka za uchunguzi zilikuwa na ushahidi wote kwamba familia nzima ilikuwa siyo Watanzania. Jambo jema zaidi ni kwamba taarifa hizi zilitokana na mgogoro wa familia hivyo wao hoja Kwa mwanasheria haikuwa kupingana na ukweli wa serikali Bali walitaka mwanasheria asaidie kufifisha ushahidi na wasichunguzwe Wala uraia wao kuguswa Bali waendelee kutambulika kama Watanzania. Naamini wapo wanasheria wengi wanakutana na kesi za aina hii ambazo ni wazi zinaonyesha nchi ipo Miko mwa wageni na tumekuwa tukizishughulikia kwa lengo lakupata Fedha na tunashiriki kuzima uchunguzi. Hawa watu tunajua malengo Yao? Kesho wamekulipa ukajenga ghorofa uone ipo siku watalipua ghorofa ukiwa ndani na familia Yako? Watanzania tusidharau Utanzania wetu, tuulinde.
Ii. Kupitia kesi hii nilibaini wapo wageni wametoroka mapigano Somalia nakuja Tanzania kujificha , Ili wasisumbuliwe wanautafuta utanzania wa magumashi ambao ndio huu wakurithishana makaratasi ya kuzaliwa ambayo nilipouliza cheti chakuzaliwa kinacost shs ngapi nikaambiwa wakala anapewa laki Hadi laki na nusu na wakati mwingine Kwa mfano familia hii Ina mtu maalumu ofisi za RITA anayepokea na kushughulikia. Kikubwa kinachofanyika wageni wanaachwa nyumbani Kwa sababu wakihojiwa watabaonika.
III. Kupitia stori za familia hii nilibaini ni rahisi Sana kwa mgeni mwenye fedha kupata kitambulisho Cha NIDA, wakipata cheti cha kuzaliwa wenyeji wao wanakwenda serikali za mtaa wanaandikiwa barua kisha wakienda NIDA wanapata ID ndani ya muda mfupi Sana. Wakati huo yupo mtanzania wakuzaliwa asikilizwi na apewi huduma. Kamishna sijui kama mbinu hizi unazijua na unajua zinavyochezwa.
iv. Nini kilitokea, Wakati kesi hii inaletwa tusaidie kudefend wakiomba istop kwenda mahakamani na wasivuliwe uraia na baada ya kujitoa kwa kuogopa kushiriki uharamia huu; zile pasipoti zilifutwa lakini sijui sheria ipoje, pasipoti zilizofutwa siyo za familia Bali ya mmoja aliyekuwa analalamikiwa Sana ila sasa waliofuta wakatoa kitu kinatwa restrictions passport Kwa miaka minne kupisha uchunguzi. Lakini baadaye kidogo wale waliobaki wakaendelea kupewa electronic Passport na yule aliyezuiwa aliomba tumwandikie kitu flani baada ya muda amepewa Tena electronic Passport. Naomba hapa Kamishna Mkuu uwasaidie Watanzania ni nani anayepewa pasipoti ya Tanzania? Hii kesi kwa upande wangu na namna ilivyofikiswa kwetu ilitutisha na nakumbuka one of our wakili ilibidi afike uhamiaji kuuliza madhara ya wakili kutoa huduma Kwa kutengeneza nyaraka Kwa watu kama Hawa ambao wanakiri wazi na nyaraka zipo wazi kwamba siyo Watanzania lakini wanataka bargaining wasipokonywe Uraia; lakini alitaka kujua ni katika mazingira Gani Raia wa Kigeni anapewa restrict pasipoti? Lakini pia tulichanganywa na Nani mhamaji haramu? Hii kesi imenifanya niandike kumwomba Kamishna Jenerali awaangalie watendaji wake, Hali ya Dunia hasa nchi maskini ipo hatarini na tishio kubwa la usalama ni binadamu. Hao maafisa wa chini wanapotoa hizi restric pasipoti wadhibitiwe, maana kila kesi ya mwenye pesa zinaishia aidha anatamkwa raia au anafutiwa pasipoti ya miaka kumi na kupewa ya muda kidogo na baada ya muda anaonga anapewa tena pasipoti kama Mtanzania. Kwa mawakili wenzetu kesi kama hizi vuteni mpunga lakini hakiiisheni mnachosaidia ni huyu mgeni kuishi kihalali au mtaftieni huyo mgeni nauli arudi kwao.

3. Kesi ya mwisho; kuna watu wanaomba msaada wa kisheria kama wakimbizi hasa kutoka huko Yemen na kwingine: Hawa watu mnashughulika nao baada ya mwaka wakiwa wanafuatilia ukimbizi unasikia wana pasipoti za Tanzania. Kwanini pasipoti za Tanzania wanasema wanakwenda Ulaya na pasipoti ya Tanzania ni dili. Nadhani hapa nchini zipo familia zinapokea wa siria na wayemeni na watu wa bara Hindi nakujifanya ni ndugu zao. Hii mbinu nafuatilia zaidi kwa sababu watu hawa sijakutana na anayetaka huduma ya nyaraka ila naaamini mawakili wenzangu wanakesi kama hizi wameletewa watengeneze nyaraka au kuthibitisha cheti ni Tru copy. Lakini uhamiaji si mnahoji, mnajua kwamba watu wanapachikwa kwenye familia? Kamishna Mkuu hapa napo fanyia utafiti ni vipi watu Hawa wanapata pasipoti? Mgeni ni mkimbizi lakini anapata pasipoti.

4. Kamishna Mkuu, Jambo nililolipenda kuhusu viongoozi wenzako lakini nilikuja kubaini mbinu hii inatumika vibaya; ukifika ofisi ya Kiongozi wa uhamiaji ukajitambulisha nakulalamikia Jambo hatua zinachukuliwa fasta, mwanzo kabla sijafunguka macho ilikuwa tukipata kesi tunakwenda Kwa wakubwa kuizima. Wakati nashighulikia kesi ya wasomali ndipo nikagundua huu ukarimu unaambatana na mlungula wakati mwingine. Siku Moja mmoja wa wateja kwenye kesi hiyo alitakiwa kwenda kuhojiwa na hakutaka kutoa maelezo it was around may, 2018. Alimpigia simu bwana mmoja jina tunalihifadhi akiomba msaada asihojiwe, what happened agent claimed apewe Milioni arobaini kuzima mahojiano, and finally alifanikiwa na ndipo masuala ya restric yalipozaliwa. Hivyo huu ukarimu wa watendaji waandamizi pls usiandamane na Rushwa, kama wanakarimu kwa kupewa rushwa bora wasikarimu.

Mwisho; ntaandika majina ya wahusika wote ambao naamini nimewahi kuwahudumia ila wana viashiria vya ugeni , ntakutumia pia hizo restric pasipot number uangalie ni namna gani kesi hii itasiadia kurise awareness kwa watendaji wako na kuwataadharisha kwamba ulimwengu huu umebadilika. Nimesoma south Africa naelewa namna corruption na tamaaa za watendaji zilivyopelekea kinachoutwa ubaguzi wa karne. Viongozi walikalia kutoa huduma mwisho wakasau kuwachuja wanaowapa huduma. Tuombe Mungu miongoni mwa hawa niliowaeleza wasiwe na nia mbaya, lakini wapo wangapi wanacheza na RIta ,NIDA, UHAMIAJI NA MIPAKANI kwa kutumia mbinu hizi?

Tuilinde Tanzania ,tuache Rushwa.
Kuna mmoja tuliambiwa sio Mtanzania,jamaa kigogo akasema ni mtanzania,akapata ubunge,akawa naibu waziri na kuwa waziri kamili
 
Nishawahi kutana na jamaa Warundi huko ughaibuni, wana passport za bongo na wanazitumia kuzamia Canada na Australia kama wakimbizi...
SWALI LA UFAHAMU;
Hawa wageni wanapotoka nchi zao wanakuwa na passport za huko kwao. Na wakati wa kusafiri wanapita airport zaidi ya moja ambako hukaguliwa fingerprints. Sasa swali langu ni kwanini isiwe rahisi kuwakamata hapo airport wakiwa na passport mpya zenye majina mapya kwasababu fingerprints hazibadiliki? Kwani anapoweka kiganja kukaguliwa fingerprints si itajitokeza rekodi yake ya zamani alivyopita?
 
Mbona kuna Watanzania kibao tu wana passport za Sweden,Canada,UK and etc kwa kujifanya wakimbizi wa Nchi za jirani zao, sisi wakijifanya Watanzania tunalia Uzalendo.Hii issue nadhani ni ya duniani kote sema kwetu tatizo ni rushwa ikimewe.
SWALI LA UFAHAMU;
Hawa wageni wanapotoka nchi zao wanakuwa na passport za huko kwao. Na wakati wa kusafiri wanapita airport zaidi ya moja ambako hukaguliwa fingerprints. Sasa swali langu ni kwanini isiwe rahisi kuwakamata hapo airport wakiwa na passport mpya zenye majina mapya kwasababu fingerprints hazibadiliki? Kwani anapoweka kiganja kukaguliwa fingerprints si itajitokeza rekodi yake ya zamani alivyopita?
 
Tz ina chagamoto kubwa zenye athari moja kwa moja kwa mtu wa hari ya chini kama mkulima machinga mama tilie kuliko hi ya wa arabu na Wahidi kupewa passport, na hili limetokea kwa sabb raia wa kawaida wame wekewa masharti magumu kupewa passport na hawana pesa hiyo 200,000 ni nyingi, wale wa hindi wa somali na wa arabu wengi hawana shida ya kukaa hapa wa natumia Tz kama gateway to Europe America baada ya pass zao za nchi zao kua rejected na hizò nchi za ulaya ,......usijindaganye kwamba huu mchezo haujulikani na top leaders ata waziri wa mambo ya ndani anaujua vizri na ni chazo cha mapato, hauna athari kwa raia wa kawaida ni faida kwa viongozi na serikali kupata mapato,.....wivu na ignorance ndo shida kwetu tulioshindwa maisha, mgejua watanzania hapa jneburg wanao miliki pass za bila kufuata masharti. Wa Tznia wanao ishi Kenya na pass za kenya ndo usiseme, sema tu nchi nyingi kuchukulia wa tz kama under dogs sio tishio kiuchumi kwasabb ya kukosa mitaji na elimu, neenda Rwanda utakutana na Wtanzania kibao na pass za uko, DRC wengi wapo na pass za congo uganda ndo basi shamba la bibi.

Hivi hawa maadui wengi wanaotuzunguka ni kina nani? Toka Nikiwa mdogo nasikia tu maadui wengi wametuzunguka kila Kona ila cha ajabu hao maadui zetu wapo busy kujenga nchi zao.
 
Kuna jamaa anaitwa Juma yupo hapo Uhamiaji Kurasini ana Vanguard Nyekundu, hii ndiyo kazi yake ameajiri vijana mtaani kabisa wanadeal na hao wageni Wasomali, Wahindi na waarabu, jamaa ana hela sana kwa sasa anajenga ghorofa kubwa sana kibaha.
Tuwafichue tu huyo jumaa sio mzalendo ni adui wa Taifa anadumaza usalama wa Taifa ashughulikiwe kwa namna inayofaa
 
Hivi hawa maadui wengi wanaotuzunguka ni kina nani? Toka Nikiwa mdogo nasikia tu maadui wengi wametuzunguka kila Kona ila cha ajabu hao maadui zetu wapo busy kujenga nchi zao.
Hizo ni propaganda za nchi za kiujamaa kujaza raia wao hofu wakati wenyewe wanaendelea kugawana nchi na familia zao, hi tz masikini sanaa kwandamwa na kila jirani wetu, wakati Ky Rw Ug SA zibabwe wamesha tupiku kitambo.
 
Tz ina chagamoto kubwa zenye athari moja kwa moja kwa mtu wa hari ya chini kama mkulima machinga mama tilie kuliko hi ya wa arabu na Wahidi kupewa passport, na hili limetokea kwa sabb raia wa kawaida wame wekewa masharti magumu kupewa passport na hawana pesa hiyo 200,000 ni nyingi, wale wa hindi wa somali na wa arabu wengi hawana shida ya kukaa hapa wa natumia Tz kama gateway to Europe America baada ya pass zao za nchi zao kua rejected na hizò nchi za ulaya ,......usijindaganye kwamba huu mchezo haujulikani na top leaders ata waziri wa mambo ya ndani anaujua vizri na ni chazo cha mapato, hauna athari kwa raia wa kawaida ni faida kwa viongozi na serikali kupata mapato,.....wivu na ignorance ndo shida kwetu tulioshindwa maisha, mgejua watanzania hapa jneburg wanao miliki pass za bila kufuata masharti. Wa Tznia wanao ishi Kenya na pass za kenya ndo usiseme, sema tu nchi nyingi kuchukulia wa tz kama under dogs sio tishio kiuchumi kwasabb ya kukosa mitaji na elimu, neenda Rwanda utakutana na Wtanzania kibao na pass za uko, DRC wengi wapo na pass za congo uganda ndo basi shamba la bibi.
Shida kuna watu wanaamini dunia nzima ni Tz.Ukenda Zambia,RSA Malawi na nchi nyingi tu utakutana na Watanzania kibao wanamiliki National ID na Passport za nchi hizo. Na unakuta mtu mwingine anamiliki ID zote mbili yaani za Tanzania na Nchi aliyopo. Haya mambo hayapo Tz tu.Nina ndugu wako nje wanamiliki Passport na Vitambulisho vya huko.Haya mambo ni dunia nzima sio Tz pekee sema ukiwa Tz unaweza sema haya mambo yapo Tz tu.
 
SWALI LA UFAHAMU;
Hawa wageni wanapotoka nchi zao wanakuwa na passport za huko kwao. Na wakati wa kusafiri wanapita airport zaidi ya moja ambako hukaguliwa fingerprints. Sasa swali langu ni kwanini isiwe rahisi kuwakamata hapo airport wakiwa na passport mpya zenye majina mapya kwasababu fingerprints hazibadiliki? Kwani anapoweka kiganja kukaguliwa fingerprints si itajitokeza rekodi yake ya zamani alivyopita?
Ukiwa na pesa utajua hakuna kinachoshindikana. Nenda Kenya,Zambia,Malawi,South au Mozambique utakutana na watanzania kibao wana passport za nchi hizo na Tz.Mkuu haya mambo kama hujawahi toka nje ya Tz unaweza ona ni ya ajabu sana na kusema ni Tz tu kuna magumashi.
 
Shida kuna watu wanaamini dunia nzima ni Tz.Ukenda Zambia,RSA Malawi na nchi nyingi tu utakutana na Watanzania kibao wanamiliki National ID na Passport za nchi hizo. Na unakuta mtu mwingine anamiliki ID zote mbili yaani za Tanzania na Nchi aliyopo. Haya mambo hayapo Tz tu.Nina ndugu wako nje wanamiliki Passport na Vitambulisho vya huko.Haya mambo ni dunia nzima sio Tz pekee sema ukiwa Tz unaweza sema haya mambo yapo Tz tu.
Viongozi wetu wana tupumbaza ili tuwe na fikra kwamba dunia nzima inawaza Tz tu, wakati hi ni nchi masikini raia wengi wa Tz wako nje wana tabika na kibaya zaidi lugha ya kiingereza inatupiga chenga tunatabika mara mbili, na viongozi wetu hawataki kulitambua, raia wakigeni wanao kuja na kutumia pass ya tz ni wachache kuliko sie watz tunao vamia na kuomba haki zetu kwenye nchi za wenzetu,.......
 
Wengi hawajui haya.Wakiona mtu ambaye sio mtanzania kapewa passport basi wanaamini hili jambo ni la Tz tu.Nakubaliana nawe kuwa watanzania wengi wako nje na wanaishi kiharamu kuliko wageni waliopo Tz.
 
Alafu mm nashangaa hapa bongo mtu anakaa zaidi ya miaka 20 lakini akiomba uraia analetewa magumashi mengi

Na bongo ubaya wetu asylum system haipo kabisa ukidakwa mpakan hata ujitetee vp ww ni muhamiaji haram

Jela miaka 2 then unakuwa deported
 
Viongozi wetu wana tupumbaza ili tuwe na fikra kwamba dunia nzima inawaza Tz tu, wakati hi ni nchi masikini raia wengi wa Tz wako nje wana tabika na kibaya zaidi lugha ya kiingereza inatupiga chenga tunatabika mara mbili, na viongozi wetu hawataki kulitambua, raia wakigeni wanao kuja na kutumia pass ya tz ni wachache kuliko sie watz tunao vamia na kuomba haki zetu kwenye nchi za wenzetu,.......
Wengi hawajui haya.Wakiona mtu ambaye sio mtanzania kapewa passport basi wanaamini hili jambo ni la Tz tu.Nakubaliana nawe kuwa watanzania wengi wako nje na wanaishi kiharamu kuliko wageni waliopo Tz.
 
Ukiwa na pesa utajua hakuna kinachoshindikana. Nenda Kenya,Zambia,Malawi,South au Mozambique utakutana na watanzania kibao wana passport za nchi hizo na Tz.Mkuu haya mambo kama hujawahi toka nje ya Tz unaweza ona ni ya ajabu sana na kusema ni Tz tu kuna magumashi.
Ila hujajibu swali langu
 
Passpot ya Tz inatakiwa sana na nchi nyingi za africa kwa kuwa ina free visa nchi nyingi watu wengi wanafanya uhalifu halafu wakikamatwa wanaonekana wanatoka Tz lkn kiuhalisia si Tz mzee Magu kajitahd sana kuwaondoa hawa lkn sasa wanarudi tena upyaaa.
Mzee magu alikua anafanya kazi uhamiaji???
 
75 Reactions
Reply
Back
Top Bottom