Salamu kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Passport za Tanzania zinakimbilia mikononi mwa wageni kupitia viongozi waandamizi na askari

Nishawahi kutana na jamaa Warundi huko ughaibuni, wana passport za bongo na wanazitumia kuzamia Canada na Australia kama wakimbizi...
 
Passpot ya Tz inatakiwa sana na nchi nyingi za africa kwa kuwa ina free visa nchi nyingi watu wengi wanafanya uhalifu halafu wakikamatwa wanaonekana wanatoka Tz lkn kiuhalisia si Tz mzee Magu kajitahd sana kuwaondoa hawa lkn sasa wanarudi tena upyaaa....
Hapa mleta mada anasema 2016 ,2018 si ndio Mzee magu alikuwepo au ?
 
Sio passport tuu na utoaji vyeti vya kuzaliwa uangaliwe kwa umakini.
 
Nchi imekuwa ya hovyo sana,, Ujamaa pia unapelekea haya,,,Watu wanaoneana huruma wanashindwa kufuata sheria za nchi...

Kuanzia Rais ni corrupted, mawaziri,, wanakwaya wa ndugai hadi mtendaji wa kijiji....

Uzalendo umebakia wa wachache sana ambao wakiongea wanaitwa wametumwa na mabeberu...
 
Watu wengi wanaotafuta passport ya nchi ingine ni kwamba hawana sababu ya kihalali. Mfano mtu anataka kuzamia Ulaya au canada kama msomali atatafuta pasi ya kitanzania.

Wapo wa yemen na syria wanakuja wanaoa wanatafuta pasi sababu labda wana historia ya criminal ili wapate urahisi wa movement, wengine wanawekeza hapa ili wapate unafuu wa kumiliki hata ardhi inabidi watafute pasi ya kibongo.

Sasa hivi hata waturuki wameshtuka Tanzania nchi nzuri kuwekeza na kuoa wana opt kuomba uraia na kupata mkoba wa hapa.
 
Sijasoma yote Ila wewe jamaa inaonekana ni mzalendo kwerii kweriii.. kuna sehemu nilipita huko Kagera , wanyarwanda wamepata NIDA kibaoo, na wanajitambilisha kuwa wao ni watz wa kuzaliwa

Kuna mambo usiyojua kuhusu eneo unalolizungumzia. Toka mwaka 1959 katika vita ya kiraia, waliingia Tz na kupatiwa hifadhi. Baada ya hapo JK Nyerere aliwapa uraia. Hao ni watoto wa raia na wamezaliwa Tz. Kuongea lugha ya kinyarwanda Tz sio hoja.

Birthright gives one a citizenship! Na sio sheria ya nchi hii tu bali makubaliano ya kimataifa.
 
Tz ina chagamoto kubwa zenye athari moja kwa moja kwa mtu wa hari ya chini kama mkulima machinga mama tilie kuliko hi ya wa arabu na Wahidi kupewa passport, na hili limetokea kwa sabb raia wa kawaida wame wekewa masharti magumu kupewa passport na hawana pesa hiyo 200,000 ni nyingi, wale wa hindi wa somali na wa arabu wengi hawana shida ya kukaa hapa wa natumia Tz kama gateway to Europe America baada ya pass zao za nchi zao kua rejected na hizò nchi za ulaya ,......usijindaganye kwamba huu mchezo haujulikani na top leaders ata waziri wa mambo ya ndani anaujua vizri na ni chazo cha mapato, hauna athari kwa raia wa kawaida ni faida kwa viongozi na serikali kupata mapato,.....wivu na ignorance ndo shida kwetu tulioshindwa maisha, mgejua watanzania hapa jneburg wanao miliki pass za bila kufuata masharti. Wa Tznia wanao ishi Kenya na pass za kenya ndo usiseme, sema tu nchi nyingi kuchukulia wa tz kama under dogs sio tishio kiuchumi kwasabb ya kukosa mitaji na elimu, neenda Rwanda utakutana na Wtanzania kibao na pass za uko, DRC wengi wapo na pass za congo uganda ndo basi shamba la bibi.
Mbona kuna Watanzania kibao tu wana passport za Sweden,Canada,UK and etc kwa kujifanya wakimbizi wa Nchi za jirani zao, sisi wakijifanya Watanzania tunalia Uzalendo.Hii issue nadhani ni ya duniani kote sema kwetu tatizo ni rushwa ikimewe.
 
Tukubaliane kwamba kuanzia ofisi ya Waziri mwenye dhamana ya Uraia Hadi chini Kuna shida. Mimi Kuna mtoto flani Binti mdogo raia wa Rwanda amekamatwa Kwa utapeli huko Rwanda nadhani alimtapeli Mme wake kiasi kikubwa Cha fedha, sijui ilikuwaje nikasikia amekimbilia Tanzania na amekamatwa Tena kwa kukutwa na pasipoti ya Rwanda. Juzi nimekuja Dar nikiwa njiani kwenda Afrika Kusini katika kupiga stori na watu flani tukawa tunajadili udhaifu wa serikali. Mtu mmoja nadhani ni wakili au huyu Binti anamahusiano naye akatoa barua ya Siri kwenye simu yake ambayo imeandikwa kwa Kamishna wa Uhamiaji nakala akapewa huyo Binti, barua hiyo Ukikisoma hata kama ujaenda shule na huna uelewa wa masuala ya utawala utajiuliza mara kadhaa Waziri amesukumwa na Nini kuandika Ile barua. Hiyo barua inaonyesha kilikuwa na kesi mahakamani serikali dhidi ya mtuhumiwa, baada ya kuonekana atashindwa akaenda kwa Waziri na Mhe. Waziri akampa barua ya kumtamka yeye ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
Najua Mamlaka hii anayo Waziri lakini huyu Binti sidhani kama Uhamiaji wamewahi hata kuhojiana naye kumjua. Pili haya mambo ya Waziri kutoa uraia Kwa wageni bila taratibu yanawafanya wageni kuja na kughushi nyaraka kama ulivyosema hapo na wakikamatwa wanamlilia Waziri wanapewa Uraia. Kibaya zaidi Waziri anamamlaka makubwa sana, hivyo tunapowalaumu watendaji ipo mifano pia ya viongozi wa kisiasa kuchangia uharibifu wa usalama wetu

Lakini pia tujikimbushe namna Viongozi Hadi wanafikia nafasi kubwa ndipo wanabainika siyo Watanzania. Lakini pia ukienda Kurasini watu wa bara Hindi kama ulivyosema wanapitiliza Kwa kamishna, wasomali ma waharabu the same so Nadhani kitendo Cha viongozi wa juu kutoa huduma kunazuia kuchukuliwa hatua. Lakini hizo pasipoti restricted nimewahi kusoma sheria hazipo, ila viongozi wameziweka kwa ajili ya kuwapa wenye fedha utanzania. Hakuna mqeusi atapewa hizo pasipoti.

Tujadili usalama na wachukulie haya mambo serious
Ipo siku hii nchi itaongozwa na mkongo kwa ujinga kama huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tz ina chagamoto kubwa zenye athari moja kwa moja kwa mtu wa hari ya chini kama mkulima machinga mama tilie kuliko hi ya wa arabu na Wahidi kupewa passport, na hili limetokea kwa sabb raia wa kawaida wame wekewa masharti magumu kupewa passport na hawana pesa hiyo 200,000 ni nyingi, wale wa hindi wa somali na wa arabu wengi hawana shida ya kukaa hapa wa natumia Tz kama gateway to Europe America baada ya pass zao za nchi zao kua rejected na hizò nchi za ulaya ,......usijindaganye kwamba huu mchezo haujulikani na top leaders ata waziri wa mambo ya ndani anaujua vizri na ni chazo cha mapato, hauna athari kwa raia wa kawaida ni faida kwa viongozi na serikali kupata mapato,.....wivu na ignorance ndo shida kwetu tulioshindwa maisha, mgejua watanzania hapa jneburg wanao miliki pass za bila kufuata masharti. Wa Tznia wanao ishi Kenya na pass za kenya ndo usiseme, sema tu nchi nyingi kuchukulia wa tz kama under dogs sio tishio kiuchumi kwasabb ya kukosa mitaji na elimu, neenda Rwanda utakutana na Wtanzania kibao na pass za uko, DRC wengi wapo na pass za congo uganda ndo basi shamba la bibi.
Haujaeleleweka au unamaanusha urahis wa kupata passport ni kila nchi wanamagummashi na sio tz pekee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa anaitwa Juma yupo hapo Uhamiaji Kurasini ana Vanguard Nyekundu, hii ndiyo kazi yake ameajiri vijana mtaani kabisa wanadeal na hao wageni Wasomali, Wahindi na waarabu, jamaa ana hela sana kwa sasa anajenga ghorofa kubwa sana kibaha.
 
Mbona kuna Watanzania kibao tu wana passport za Sweden,Canada,UK and etc kwa kujifanya wakimbizi wa Nchi za jirani zao, sisi wakijifanya Watanzania tunalia Uzalendo.Hii issue nadhani ni ya duniani kote sema kwetu tatizo ni rushwa ikimewe.
Watanzania tulio wengi ni limbukeni ushamba na uzalendo wa kinafiki, huu ni mchezo dunia nzima na inchi zinazo eleweka kama US UK FR CND SA wageni wengi wana manipulate system zao na kupata passport bila kupigiwa kalele sembuse hapa kwetu hapa 3rd world country, wanatumia hapa tu kama exit door kutafuta rizki nje ni wachache wana opt kuka hapa milele hi nchi yetu ni shida raha na utajili viko kwenye nadharia havionekani.
 
Tanzania imezungukwa na maadui wengi kuliko marafiki, Tanzania imezungukwa na nchi zisizo na amani kama taifa letu. Ulinzi wa Tanzania upo mikononi mwetu Watanzania. Tusiposema hakuna atakayesema Kesho Wala Kesho kutwa. Nchi yetu imevamiwa Sana na wageni wanaotaka kuifanya nchi hii ni Mali Yao. Naamini nisipomwambia Kamishna Mkuu kuhusu Hali hii ntakua simsaidii, nisipomwambia Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Hali ilivyo mtaani may be wataingia wabaya nchini na wataishambulia nchi nakuumiza hata ndugu zangu naomba niseme. Yawezekana ninayoyasema anayajua au ni mapya kwake ila yatasaidia Taifa.

Kabla sijasema nikiri kwamba Mimi ni mtoa huduma za kisheria, Katika kutoa huduma za kisheria ndipo nilipokutana na haya nitakayoyaeleza hapa ambayo naamini yanamsaada mkubwa Kwa ulinzi wa nchi yetu,ulinzi wa afrika mashariki na ulinzi wa Dunia Kwa ujumla wake. Hivyo naomba anaposoma Kamishna Mkuu wa Uhamiaji basi asisome peke yake wasome Watanzania wengi na watakapoona visa vya aina hii waweze kuripoti wahusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria. Hizi ni true stori ambazo zimepita mikononi mwangu na mikononi mwa watoa huduma ya kisheria wengine, hakuna aliyechukulia serious au kama walichukulia serious basi awakufikisha ujumbe panapohusika.
Kati ya mwaka 2015 Hadi Sasa nimetoa huduma Kwa wateja wengi nikianzia Mwanza, nikaenda Mbeya, nikahamia Dar na Sasa nipo Kilimanjaro. Kupitia huduma hizo naomba kueleza madhara ya huduma hizi kwa Taifa letu na kwa Mataifa mengine
1. Huduma ya utoaji wa kiapo Cha kuzaliwa: Hii huduma inatolewa na Mawakili wengi na ni huduma ipo kisheria lakini huduma hii usipoifanya Kwa uadilifu madhara yake ni makubwa sana. Mwaka 2016 alifika mteja anatafuta kiapo kwangu, Mteja huyo alikua na maneno machache Sana ya kiswahili na mengi ya kiingereza, alikua anatafuta kiapo Kwa ajili ya pasipoti; nilipomhoji kuhusu majina yake,majina ya wazazi na majina ya watakao shuhudia kiapo alionekana dhahiri kwamba anatunga majina hivyo kumtilia mashaka. Nilipombana zaidi na kumweleza umuhimu wa kusema ukweli alikiri yeye ni raia wa Kenya ila amakuja nchini kufuatilia pasipoti, familia waliyofikia wakiwa watu wanne wanawasaidia kupata pasipoti na kwamba wenzake wote wamepata yeye amekwama kiapo. Nilikataa kumpa huduma na kumwacha aondoke Kisha kuwasilisha taarifa zake na za Ndugu zake ambao alidai wanapasipoti Uhamiaji ya karibu nisingependa kutaja jina; baada ya kuwasilisha taarifa zile nakuchukua namba za simu za afisa Kwa ajili yakupeana taarifa zaidi nilikuja kubaini kwamba kesi Ile imeingiliwa na watu flani wakubwa wanaofanya kazi wizara ya mambo ya ndani hivyo suspects wakapata mtetezi kutoka juu. Kwanini nimeandika hii stori, nimeandika baada ya kukutana na Mteja yuleyule aliyekiri kwangu kwamba ni raia wa Kenya Uhamiaji Dar es salaam akiwa anafuatilia siyo pasipoti mpya tu bali anabadilisha apewe ya kielekroniki. Kibaya zaidi treatment yake ilikuwa ni VIP kwa sababu wakati wengine tunasubiri yyeye aliingia Moja Kwa Moja nakukamilisha huduma nikasikia anaelekezwa kwenda Kurasini means ana mtandao mkubwa. Nilitamani kuwajulisha maafisa wawe makini lakini nilisita kukwamishwa mimi yeye akapita na sikupenda kujipnyesha kwake. Kwa tafsiri nyingine yupo mtumishi wa serikali aliyezuia huyu bwana kuchunguzwa uraia wake, yupo wakili aliyemtengenezea kiapo na wapo Watanzania nyuma yake waliojitolea kumpokea na kuruhusu atumie majina ya familia Yao. Lakini je wakati haya yanafanyika nani anajua dhamira za wageni hawa kutafuta pasipoti za Tanzania? Kwanini wabadili majina? Wana athari gani kwa kesho ya Tanzania? Kamishna tulindie nchi yetu simu zenu wakubwa wakati mwingine zinapeperusha wahalifu

2. Nikiwa Arusha nilikuta kesi Moja ofisini ambayo wahusika walioomba msaada wa kisheria walikuwa Dar es salaam. Katika kuwasikiliza nilipobaini ukweli nilijitoa bila kusema Kwanini nimejitoa. Story Yao Kwa ufupi ipo hivi; Wana asili ya Somalia, baba na mama waliingia nchini miaka ya 1970 wakiwa na pasipoti za Somalia. Walipokelewa na kaka Yao ambaye pia alikuwa Msomali. Miaka ya 1980 wenyeji wao wakafanikiwa kupata pasipoti za Tanzania na kwenda Ulaya. Wao pia wakatafuta pasipoti na kupata pasipoti lazima wawe na cheti cha kuzaliwa. Nilisikitika kusikia waliweza kupenyeza rupia wakapata vyeti vya kuzaliwa wazazi na watoto kipindi hicho hicho wakiwa tayari wanaishi kwa karatasi za kufanya kazi za uhamiaji. Baadaye walifanikiwa kupata pasipoti na watoto wao, nusu wakaenda ulaya na nusu wakabaki Tanzania. Mwaka 1995 Mzee wao akakamatwa Kwa Tuhuma za kugushi na kujipatia nyaraka( means yupo mtu aliwatonya Uhamiaji kwamba familia Ile siyo Watanzania) wakapanchi wakafunga uchunguzi bila uchunguzi. Siku wanakabidhiwa kwangu nakueleza stori hii ndipo nikabaini mambo yafuatayo.
I. Familia hii tayari ilishaingiza nchini ndugu zao wengi na wote kupitia cheti cha kuzaliwa Cha mwaka 1980+ wamefanikiwa kujitanabaisha kama wazaliwa wa Tanzania. Kila wakitaka cheti wanatoa copy vile vyeti vya awali na kuambatisha Kisha RITA wanatoa vyeti kama wazaliwa wa Tanzania. Kwanini wakieleza ukweli? Ni kwa sababu katika Tuhuma zilizokuwa zinawakabili tayari mamlaka za uchunguzi zilikuwa na ushahidi wote kwamba familia nzima ilikuwa siyo Watanzania. Jambo jema zaidi ni kwamba taarifa hizi zilitokana na mgogoro wa familia hivyo wao hoja Kwa mwanasheria haikuwa kupingana na ukweli wa serikali Bali walitaka mwanasheria asaidie kufifisha ushahidi na wasichunguzwe Wala uraia wao kuguswa Bali waendelee kutambulika kama Watanzania. Naamini wapo wanasheria wengi wanakutana na kesi za aina hii ambazo ni wazi zinaonyesha nchi ipo Miko mwa wageni na tumekuwa tukizishughulikia kwa lengo lakupata Fedha na tunashiriki kuzima uchunguzi. Hawa watu tunajua malengo Yao? Kesho wamekulipa ukajenga ghorofa uone ipo siku watalipua ghorofa ukiwa ndani na familia Yako? Watanzania tusidharau Utanzania wetu, tuulinde.
Ii. Kupitia kesi hii nilibaini wapo wageni wametoroka mapigano Somalia nakuja Tanzania kujificha , Ili wasisumbuliwe wanautafuta utanzania wa magumashi ambao ndio huu wakurithishana makaratasi ya kuzaliwa ambayo nilipouliza cheti chakuzaliwa kinacost shs ngapi nikaambiwa wakala anapewa laki Hadi laki na nusu na wakati mwingine Kwa mfano familia hii Ina mtu maalumu ofisi za RITA anayepokea na kushughulikia. Kikubwa kinachofanyika wageni wanaachwa nyumbani Kwa sababu wakihojiwa watabaonika.
III. Kupitia stori za familia hii nilibaini ni rahisi Sana kwa mgeni mwenye fedha kupata kitambulisho Cha NIDA, wakipata cheti cha kuzaliwa wenyeji wao wanakwenda serikali za mtaa wanaandikiwa barua kisha wakienda NIDA wanapata ID ndani ya muda mfupi Sana. Wakati huo yupo mtanzania wakuzaliwa asikilizwi na apewi huduma. Kamishna sijui kama mbinu hizi unazijua na unajua zinavyochezwa.
iv. Nini kilitokea, Wakati kesi hii inaletwa tusaidie kudefend wakiomba istop kwenda mahakamani na wasivuliwe uraia na baada ya kujitoa kwa kuogopa kushiriki uharamia huu; zile pasipoti zilifutwa lakini sijui sheria ipoje, pasipoti zilizofutwa siyo za familia Bali ya mmoja aliyekuwa analalamikiwa Sana ila sasa waliofuta wakatoa kitu kinatwa restrictions passport Kwa miaka minne kupisha uchunguzi. Lakini baadaye kidogo wale waliobaki wakaendelea kupewa electronic Passport na yule aliyezuiwa aliomba tumwandikie kitu flani baada ya muda amepewa Tena electronic Passport. Naomba hapa Kamishna Mkuu uwasaidie Watanzania ni nani anayepewa pasipoti ya Tanzania? Hii kesi kwa upande wangu na namna ilivyofikiswa kwetu ilitutisha na nakumbuka one of our wakili ilibidi afike uhamiaji kuuliza madhara ya wakili kutoa huduma Kwa kutengeneza nyaraka Kwa watu kama Hawa ambao wanakiri wazi na nyaraka zipo wazi kwamba siyo Watanzania lakini wanataka bargaining wasipokonywe Uraia; lakini alitaka kujua ni katika mazingira Gani Raia wa Kigeni anapewa restrict pasipoti? Lakini pia tulichanganywa na Nani mhamaji haramu? Hii kesi imenifanya niandike kumwomba Kamishna Jenerali awaangalie watendaji wake, Hali ya Dunia hasa nchi maskini ipo hatarini na tishio kubwa la usalama ni binadamu. Hao maafisa wa chini wanapotoa hizi restric pasipoti wadhibitiwe, maana kila kesi ya mwenye pesa zinaishia aidha anatamkwa raia au anafutiwa pasipoti ya miaka kumi na kupewa ya muda kidogo na baada ya muda anaonga anapewa tena pasipoti kama Mtanzania. Kwa mawakili wenzetu kesi kama hizi vuteni mpunga lakini hakiiisheni mnachosaidia ni huyu mgeni kuishi kihalali au mtaftieni huyo mgeni nauli arudi kwao.


3. Kesi ya mwisho; kuna watu wanaomba msaada wa kisheria kama wakimbizi hasa kutoka huko Yemen na kwingine: Hawa watu mnashughulika nao baada ya mwaka wakiwa wanafuatilia ukimbizi unasikia wana pasipoti za Tanzania. Kwanini pasipoti za Tanzania wanasema wanakwenda Ulaya na pasipoti ya Tanzania ni dili. Nadhani hapa nchini zipo familia zinapokea wa siria na wayemeni na watu wa bara Hindi nakujifanya ni ndugu zao. Hii mbinu nafuatilia zaidi kwa sababu watu hawa sijakutana na anayetaka huduma ya nyaraka ila naaamini mawakili wenzangu wanakesi kama hizi wameletewa watengeneze nyaraka au kuthibitisha cheti ni Tru copy. Lakini uhamiaji si mnahoji, mnajua kwamba watu wanapachikwa kwenye familia? Kamishna Mkuu hapa napo fanyia utafiti ni vipi watu Hawa wanapata pasipoti? Mgeni ni mkimbizi lakini anapata pasipoti.

4. Kamishna Mkuu, Jambo nililolipenda kuhusu viongoozi wenzako lakini nilikuja kubaini mbinu hii inatumika vibaya; ukifika ofisi ya Kiongozi wa uhamiaji ukajitambulisha nakulalamikia Jambo hatua zinachukuliwa fasta, mwanzo kabla sijafunguka macho ilikuwa tukipata kesi tunakwenda Kwa wakubwa kuizima. Wakati nashighulikia kesi ya wasomali ndipo nikagundua huu ukarimu unaambatana na mlungula wakati mwingine. Siku Moja mmoja wa wateja kwenye kesi hiyo alitakiwa kwenda kuhojiwa na hakutaka kutoa maelezo it was around may, 2018. Alimpigia simu bwana mmoja jina tunalihifadhi akiomba msaada asihojiwe, what happened agent claimed apewe Milioni arobaini kuzima mahojiano, and finally alifanikiwa na ndipo masuala ya restric yalipozaliwa. Hivyo huu ukarimu wa watendaji waandamizi pls usiandamane na Rushwa, kama wanakarimu kwa kupewa rushwa bora wasikarimu.

Mwisho; ntaandika majina ya wahusika wote ambao naamini nimewahi kuwahudumia ila wana viashiria vya ugeni , ntakutumia pia hizo restric pasipot number uangalie ni namna gani kesi hii itasiadia kurise awareness kwa watendaji wako na kuwataadharisha kwamba ulimwengu huu umebadilika. Nimesoma south Africa naelewa namna corruption na tamaaa za watendaji zilivyopelekea kinachoutwa ubaguzi wa karne. Viongozi walikalia kutoa huduma mwisho wakasau kuwachuja wanaowapa huduma. Tuombe Mungu miongoni mwa hawa niliowaeleza wasiwe na nia mbaya, lakini wapo wangapi wanacheza na RIta ,NIDA, UHAMIAJI NA MIPAKANI kwa kutumia mbinu hizi?

Tuilinde Tanzania ,tuache Rushwa.
Ukarimu unaanzia nyumbani. Weka hapa majina na passport zao zote huyo kamishna atayachukua hapahapa na jamii itapaza sauti kuanzia hapa. Pia yapeleke twitter, Facebook e.t.c kule pia kuna maofisa wa serikali wanaoweza kuchukua hatua. Tunataka tanzania salama japo tutapigwa mnada.
 
Back
Top Bottom