Salamu kutoka Rugby Union

Rugby Union

JF-Expert Member
Nov 21, 2012
402
248
Kama ID inavyojieleza.

Utambulisho huu unastahili hasa jukwaa la Michezo, ila kwa itifaki ya JF imebidi niuweke huku.

Rugby ni moja kati ya michezo ya nguvu na kasi zaidi unaochezwa na wachezaji 15 kila timu, kila timu ikijaribu kufika na mpira kupita nusu ya wapinzani kwenye eneo la kufungia. Mpira wake ni kama huo hapo kwenye avatar yangu... (nitakuja na maelezo kamili kwenye uzi wake)

Mchezo huu umeanza kuchezwa humu nchini miaka ya 1950, wakati huo Tanganyika ikiwa chini ya Uingereza, mechi ya kwanza ikiwa kati ya Tanzania na Kenya ambapo Kenya walishinda kwa matokeo ambayo hayajawahi kufahamika.

Tanzania Rugby Union ndio chama kinachoongoza mchezo huu hapa nchini, kikiwa na makao yake makuu huko Arusha na mechi za timu ya taifa (pia inafahamika kama Twigas) huchezwa kwenye viwanja vya Friedkin Recreational.

TRU ina usajili kamili wa CAR, shirikisho la rugby barani Afrika na ina usajili wa muda wa Bodi ya Rugby duniani (International Rugby Board) na iko katika mchakato wa usajili wa kudumu, malengo yake ikiwa ni kushiriki michezo ya Olimpiki mwaka 2016 mjini Rio de Janeiro.

Hembu tukomee hapo kwa sasa... Nitajitahidi kujibu maswali yenu, na kwa ufafanuzi zaidi tukutane Jukwaa la Michezo.
Nikaribisheni...
 
nadhani huu uzi utasaidiana sana bidada Ad kuufanikisha huu mchezo kufahamika..
 
ni mchezo mzuri sana na ni maarufu sana hapa Arusha ila kwakweli sina mwili wa huu mchezo .
 
ni mchezo mzuri sana na ni maarufu sana hapa Arusha ila kwakweli sina mwili wa huu mchezo .

Mwili wala sio tatizo, unaweza kucheza nafasi ya kati ambayo haihitaji nguvu kubwa kama front row.
Cecil Afrika wa Springboks Sevens hana mwili mkubwa kivile, lakini ni mmoja kati ya wachezaji mahiri duniani.
 
Rugby Union

Unakaribishwa!

Good job.

Ahsante ndugu.
Lazima watu wajitolee kuliko kuishia kulaumu kila yanapotokea matokeo mabovu. Mimi sipo TRU wala kwenye klabu yoyote ya rugby, na kama wengi wetu mchezo huu pia ni kitu kigeni kwangu, kuanzia sheria na structure yake duniani na huku nchini.
Naamini kwa kushirikiana na wadau wengine na GT's tutaupeleka mbele angalau kufikikia kiwango cha wenzetu Kenya na Uganda.
 
Last edited by a moderator:
Nimeitazama video ya Tanzania rugby katika youtube. It was very refreshing. Natumai Tanzania ilete standards za rugby juu ndipo tuwe na michuano baina ya timu za Afrika mashariki aka Bamburi series. Muhimu ni kuanzisha rugby katika mashule.

Miaka michache iliyopita kulikuwa na timu nzuri sana ya tanzania schools katika michuano ya safari sevens. Sijui walipotea wapi. mwaka huu ni Rwanda schools iliyo fanya miujiza na kufika fainali ya safari sevens katika U19 category.

Tupatie updates za Tanzania rugby katika uzi huu.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom