Rugby Union
JF-Expert Member
- Nov 21, 2012
- 402
- 248
Kama ID inavyojieleza.
Utambulisho huu unastahili hasa jukwaa la Michezo, ila kwa itifaki ya JF imebidi niuweke huku.
Rugby ni moja kati ya michezo ya nguvu na kasi zaidi unaochezwa na wachezaji 15 kila timu, kila timu ikijaribu kufika na mpira kupita nusu ya wapinzani kwenye eneo la kufungia. Mpira wake ni kama huo hapo kwenye avatar yangu... (nitakuja na maelezo kamili kwenye uzi wake)
Mchezo huu umeanza kuchezwa humu nchini miaka ya 1950, wakati huo Tanganyika ikiwa chini ya Uingereza, mechi ya kwanza ikiwa kati ya Tanzania na Kenya ambapo Kenya walishinda kwa matokeo ambayo hayajawahi kufahamika.
Tanzania Rugby Union ndio chama kinachoongoza mchezo huu hapa nchini, kikiwa na makao yake makuu huko Arusha na mechi za timu ya taifa (pia inafahamika kama Twigas) huchezwa kwenye viwanja vya Friedkin Recreational.
TRU ina usajili kamili wa CAR, shirikisho la rugby barani Afrika na ina usajili wa muda wa Bodi ya Rugby duniani (International Rugby Board) na iko katika mchakato wa usajili wa kudumu, malengo yake ikiwa ni kushiriki michezo ya Olimpiki mwaka 2016 mjini Rio de Janeiro.
Hembu tukomee hapo kwa sasa... Nitajitahidi kujibu maswali yenu, na kwa ufafanuzi zaidi tukutane Jukwaa la Michezo.
Nikaribisheni...