Salama ya Tanzania: CCM ifutwe!!

CCM ifutwe?

  • Total voters
    31
Kamende

Kamende

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2008
Messages
415
Likes
6
Points
0
Kamende

Kamende

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2008
415 6 0
Ninaandika hoja yangu hii nikiwa makini vya kutosha baada ya kuchuja kwa undani ukweli na chanzo cha matatizo ya nchi yetu kwa leo.

Ninakumbuka kwa kiasi kuwa enzi za siasa ya chama kimoja Tanzania ilikuwa imelemaa kutokana na mfumo wenyewe kwamba isingewezekana hata kidogo kutoa mawazo yanayokinzana na imani, mwelekeo na msimamo wa chama tawala. Kibaya zaidi ingehesabiwa kuwa uhaini endapo ungetofautiana na Mwenyekiti wa chama.

Mwaka 1992 tukatangaza kuingia katika siasa za mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Lengo kubwa likiwa ni kuongeza demokrasia, uwazi na uwajibikaji.

Siasa ya vyama vingi ilimaanishwa kuifanya serikali iliyoko madarakani kuongoza wakiwa makini wakihofia kuwa kosa lolote lingeweza kuwaondoa madarakani. Kwa imani hii yeyote atakayekuwa madarakani atakuwa makini kwa kuhofia kuwa mzaha wowote utamnyima kuendelea kushika dola siku zijazo.

Kwa bahati mbaya sana Tanzania ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa CCM iliyokuwa madarakani wakati huo iliendelea na mamlaka yake na nguvu zake nyingi ilizokuwa nazo. Wakati vyama vingine vinazaliwa vikiwa vichanga na masikini kabisa viliikuta CCM ikiwa chama kikubwa chenye mtandao nchi nzima, mali nyingi sana na uzoefu mkubwa wa kujikita katika utawala.

Hii ni kusema kwamba Tanzania iliingia kwenye mfumo wa vyama vingi kama kiini macho tu. Serikali iliyokuwa madarakani kwa wakati ule kwanza kwa kutambua na kushangilia ujuzi mdogo wa mambo ya siasa kwa wananchi wake na kwa kutumia mabavu ilipoka demokrasia kwa lengo la kuihakikishia CCM uhakika wa kukaa madarakani milele kutokana na kuweka tofauti kubwa ya kiuwezo baina yake na vyama vingine vya siasa.

Kwa kosa hili sasa haiwezekani kuwalazimisha viongozi kutii kiapo chao cha utii kwa utumishi wao. Wanajua wazi kuwa hali ya kupingwa itaendelea kwa maneno tu na wala hakuna jinsi ambavyo kitatokea chama kingine kikaweza kuitoa CCM madarakani. Hawana hofu ya kuondolewa madarakani kwa nini wawajibike kwa wananchi?

Katika hila zao ili waweze kuiibia nchi wanavyotaka, mafisadi wamefanikiwa kuwekeza kwa nguvu nyingi CCM na kuiimarisha ili ividhoofishe vyama vingine na kubakia yenyewe imara lakini kwa sharti la kutokuzuia wizi wa mafisadi hao.

Sasa tunapozungumzia nguvu ya CCM kuwa kubwa sana dhidi ya vyama vingine tunazungumzia fursa ya wezi (mafisadi) kupora kwa nguvu sana mali za Tanzania.

Kama Tanzania inataka kupona dhidi ya wizi na uporaji unaoendelea leo basi ni lazima turudi kujadili upya na kwa umakini tuone kanuni za kuingia kwenye siasa za vyama vingi vya siasa.

Hata hivyo ni lazima sheria itumike kuifuta CCM kwani kutokana na ulaghai wake wa kujibakizia mali zote ambazo wananchi walivuna kwa pamoja walipokuwa katika mfumo wa chama kimoja cha siasa.

Sababu ya pili ya kuifuta CCM ni kutokana na chama chenyewe kuwa maficho ya mafisadi na ya kwamba haiwezekani kukiachanisha chama hicho na mafisadi.

Sababu ya tatu ya kuifuta CCM ni kuwa kutokana na chama hicho kukubuhu kwa rushwa kwenye kila kitu kinachofanya basi vita ya rushwa haiwezi kufanikiwa nchini. Kwa kuwa tumetangaza kuwa rushwa ni adui mkubwa wa nchi hii na kwa kuwa nguvu kubwa ya CCM inatokana na matumizi makubwa ya rushwa basi njia pekee ya kuinusuru nchi dhidi ya rushwa ni kuifuta CCM.

Sababu ya nne ya kuifuta CCM ni kutokana na kuwafanya watanzania wengi hata vijana kuishi maisha ya kutegemea upendeleo. CCM ni chama ambacho watu hujiunga ili kupata manufaa fulani. Kwa hiyo watu wote wasiopenda kujibidiisha, hujiunga na chama hicho. Sasa ili kuwafanya watanzania hasa vijana kuwa na tabia ya kuwajibika na kujibidiisha basi ni lazima tufyeke kichaka kinachowavutia watu wavivu (CCM)

Sababu ya tano ya kuifuta CCM ni ili kuifanya demokrasia iweze kufanya kazi. CCM ni kikwazo kikubwa cha demokrasia. Kila siku CCM inabuni mbinu za kuvihujumu vyama vingine na kupunguza fursa za watanzania za kukemea uovu. Wanafanya hivyo kwa kutumia nguvu ambazo wanazo tayari. Na kwamba kwa kweli hawaoni aibu hata kidogo kutumia fedha za nchi kuihujumu nchi. Nakiri kuwa CCM haiwezi kuacha hii tabia ya kuhuni. Dawa pekee ni kuifuta.

Zipo sababu zingine nyingi sana za kuifuta CCM, Hatua hii ni ya kizalendo yenye nia ya kuikomboa nchi yetudhidi ya uduni ambao inao na inaendelea kuwa nao kutokana na uwepo wa CCM.

Hapa mtandaoni nawakaribisha sana tujadili hoja hii na kuiboresha, ili kuinusuru nchi yetu. Najua watanzania hatuthubutu kujadili kufutwa kwa CCM. Huu ni mkakati wao mmojawapo pia. Wamewafanya watanzania waamini kuwa maana ya uongozi ni kutawaliwa na CCM. Kumbe huku ndiko kuimaliza nchi yetu.

Hatuwezi kuthubutu kuiondoa CCM madarakani kama hatuthubutu hata kujadili kuifuta kwa makosa ya wazi kabisa ambayo imefanya.

Sitanyamaza: hadi CCM ifutwe!!
 
M

MiratKad

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2008
Messages
294
Likes
0
Points
0
M

MiratKad

JF-Expert Member
Joined May 2, 2008
294 0 0
Kuna kila sababu CCM ni lazima kifutwe. Kufanya hivyo kutawasambaratisha Mafisadi. Na uwezekano ni mkubwa tutapata Wabunge wanao wajibika sio haya mabubu yanayosinzia bungeni.
 
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
9,913
Likes
8,198
Points
280
Mag3

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
9,913 8,198 280
Kuna kila sababu CCM ni lazima kifutwe. Kufanya hivyo kutawasambaratisha Mafisadi. Na uwezekano ni mkubwa tutapata Wabunge wanao wajibika sio haya mabubu yanayosinzia bungeni.
Sababu nyingine ni CCM kuendeleza juhudi zake za kibaguzi miongoni mwa wananchi ndani na nje ya nchi kwa kisingizio cha itikadi. Hii siasa ya ubaguzi wa itikadi lazima ipigwe vita kwa kukifuta chama hiki.

Kwa ndani wananchi wanabaguliwa kwa kutengwa kutoka utotoni hadi uzeeni. Kuna watoto wa CCM, vijana wa CCM, wanawake wa CCM na Wazazi wa CCM na jumuiya hizi zote zimeandikwa rasmi kama jumuiya za kitaifa.

Huko nje mabalozi wetu hutumiwa na CCM kuwabagua na kuwatenga vijana wa kitanzania walioko masomoni kwa kuanzisha matawi ya CCM.

Haya makundi si siri kuwa yanafaidika kwa kiwango fulani kwani yako above the law. Jumuiya ya MAFISADI wa CCM pamoja na kuwa haijaandikishwa rasmi lakini malengo na matendo yake tayari tunayashuhudia. Tusiwape nafasi ya kujiimarisha - hivyo hivi vikundi navyo vifutwe.
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
80,573
Likes
117,662
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
80,573 117,662 280
Kuna kila sababu CCM ni lazima kifutwe. Kufanya hivyo kutawasambaratisha Mafisadi. Na uwezekano ni mkubwa tutapata Wabunge wanao wajibika sio haya mabubu yanayosinzia bungeni.
Matatizo yetu mengi sasa hivi yanasababishwa na hiki chama cha mafisadi. Kibaya zaidi ni kwamba wenyewe wameridhika kabisa na wala hawafanyi juhudi zozote za kukirudishia hadhi chama hicho.
 
Pundamilia07

Pundamilia07

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2007
Messages
1,433
Likes
12
Points
135
Pundamilia07

Pundamilia07

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2007
1,433 12 135
Ninaandika hoja yangu hii nikiwa makini vya kutosha baada ya kuchuja kwa undani ukweli na chanzo cha matatizo ya nchi yetu kwa leo.

Ninakumbuka kwa kiasi kuwa enzi za siasa ya chama kimoja Tanzania ilikuwa imelemaa kutokana na mfumo wenyewe kwamba isingewezekana hata kidogo kutoa mawazo yanayokinzana na imani, mwelekeo na msimamo wa chama tawala. Kibaya zaidi ingehesabiwa kuwa uhaini endapo ungetofautiana na Mwenyekiti wa chama.

Mwaka 1992 tukatangaza kuingia katika siasa za mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Lengo kubwa likiwa ni kuongeza demokrasia, uwazi na uwajibikaji.

Siasa ya vyama vingi ilimaanishwa kuifanya serikali iliyoko madarakani kuongoza wakiwa makini wakihofia kuwa kosa lolote lingeweza kuwaondoa madarakani. Kwa imani hii yeyote atakayekuwa madarakani atakuwa makini kwa kuhofia kuwa mzaha wowote utamnyima kuendelea kushika dola siku zijazo.

Kwa bahati mbaya sana Tanzania ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa CCM iliyokuwa madarakani wakati huo iliendelea na mamlaka yake na nguvu zake nyingi ilizokuwa nazo. Wakati vyama vingine vinazaliwa vikiwa vichanga na masikini kabisa viliikuta CCM ikiwa chama kikubwa chenye mtandao nchi nzima, mali nyingi sana na uzoefu mkubwa wa kujikita katika utawala.

Hii ni kusema kwamba Tanzania iliingia kwenye mfumo wa vyama vingi kama kiini macho tu. Serikali iliyokuwa madarakani kwa wakati ule kwanza kwa kutambua na kushangilia ujuzi mdogo wa mambo ya siasa kwa wananchi wake na kwa kutumia mabavu ilipoka demokrasia kwa lengo la kuihakikishia CCM uhakika wa kukaa madarakani milele kutokana na kuweka tofauti kubwa ya kiuwezo baina yake na vyama vingine vya siasa.

Kwa kosa hili sasa haiwezekani kuwalazimisha viongozi kutii kiapo chao cha utii kwa utumishi wao. Wanajua wazi kuwa hali ya kupingwa itaendelea kwa maneno tu na wala hakuna jinsi ambavyo kitatokea chama kingine kikaweza kuitoa CCM madarakani. Hawana hofu ya kuondolewa madarakani kwa nini wawajibike kwa wananchi?

Katika hila zao ili waweze kuiibia nchi wanavyotaka, mafisadi wamefanikiwa kuwekeza kwa nguvu nyingi CCM na kuiimarisha ili ividhoofishe vyama vingine na kubakia yenyewe imara lakini kwa sharti la kutokuzuia wizi wa mafisadi hao.

Sasa tunapozungumzia nguvu ya CCM kuwa kubwa sana dhidi ya vyama vingine tunazungumzia fursa ya wezi (mafisadi) kupora kwa nguvu sana mali za Tanzania.

Kama Tanzania inataka kupona dhidi ya wizi na uporaji unaoendelea leo basi ni lazima turudi kujadili upya na kwa umakini tuone kanuni za kuingia kwenye siasa za vyama vingi vya siasa.

Hata hivyo ni lazima sheria itumike kuifuta CCM kwani kutokana na ulaghai wake wa kujibakizia mali zote ambazo wananchi walivuna kwa pamoja walipokuwa katika mfumo wa chama kimoja cha siasa.

Sababu ya pili ya kuifuta CCM ni kutokana na chama chenyewe kuwa maficho ya mafisadi na ya kwamba haiwezekani kukiachanisha chama hicho na mafisadi.

Sababu ya tatu ya kuifuta CCM ni kuwa kutokana na chama hicho kukubuhu kwa rushwa kwenye kila kitu kinachofanya basi vita ya rushwa haiwezi kufanikiwa nchini. Kwa kuwa tumetangaza kuwa rushwa ni adui mkubwa wa nchi hii na kwa kuwa nguvu kubwa ya CCM inatokana na matumizi makubwa ya rushwa basi njia pekee ya kuinusuru nchi dhidi ya rushwa ni kuifuta CCM.

Sababu ya nne ya kuifuta CCM ni kutokana na kuwafanya watanzania wengi hata vijana kuishi maisha ya kutegemea upendeleo. CCM ni chama ambacho watu hujiunga ili kupata manufaa fulani. Kwa hiyo watu wote wasiopenda kujibidiisha, hujiunga na chama hicho. Sasa ili kuwafanya watanzania hasa vijana kuwa na tabia ya kuwajibika na kujibidiisha basi ni lazima tufyeke kichaka kinachowavutia watu wavivu (CCM)

Sababu ya tano ya kuifuta CCM ni ili kuifanya demokrasia iweze kufanya kazi. CCM ni kikwazo kikubwa cha demokrasia. Kila siku CCM inabuni mbinu za kuvihujumu vyama vingine na kupunguza fursa za watanzania za kukemea uovu. Wanafanya hivyo kwa kutumia nguvu ambazo wanazo tayari. Na kwamba kwa kweli hawaoni aibu hata kidogo kutumia fedha za nchi kuihujumu nchi. Nakiri kuwa CCM haiwezi kuacha hii tabia ya kuhuni. Dawa pekee ni kuifuta.

Zipo sababu zingine nyingi sana za kuifuta CCM, Hatua hii ni ya kizalendo yenye nia ya kuikomboa nchi yetudhidi ya uduni ambao inao na inaendelea kuwa nao kutokana na uwepo wa CCM.

Hapa mtandaoni nawakaribisha sana tujadili hoja hii na kuiboresha, ili kuinusuru nchi yetu. Najua watanzania hatuthubutu kujadili kufutwa kwa CCM. Huu ni mkakati wao mmojawapo pia. Wamewafanya watanzania waamini kuwa maana ya uongozi ni kutawaliwa na CCM. Kumbe huku ndiko kuimaliza nchi yetu.

Hatuwezi kuthubutu kuiondoa CCM madarakani kama hatuthubutu hata kujadili kuifuta kwa makosa ya wazi kabisa ambayo imefanya.

Sitanyamaza: hadi CCM ifutwe!!
KaMENDE,
Nimesoma thread yako, lakini kwanza sikuona umuhimu wa kuingia na kuchangia kwani nilihisi ni zile za makada wa propaganda wa CHAMA fulani ambao wametapakaa humu ndani kuandika hata kwa yale wasiyo yajua kwa ufasaha.
Lakini baadae nikaona kama mmoja wa wa-JF nitakuwa sikutendei haki kama sitakusaidia kwa mawazo japo kidogo ili upate mwelekeo.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesajiliwa kwa mujibu wa sheria halali ya vyama vya siasa. Sheria ambayo pia imeanzisha vyama vingine vikiwemo vyama maarufu kama CUF, NCCR nk. Sasa endapo kama unataka Chama Cha Mapinduzi kifutwe basi huna budi wewe mwenyewe au kupitia wakala wako uende mahakamani ukawasilishe shauri lako la kufutwa kwa Chama Cha Mapinduzi. Kwa kawaida mahakamani hawakatai kupokea shauri, nina hakika shauri lako litasikilizwa na haki itapatikana.Nakutakia kila la heri.
 
Kevo

Kevo

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2008
Messages
1,333
Likes
19
Points
0
Kevo

Kevo

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2008
1,333 19 0

Very Ironical!
Over my dead body kama watakifuta!kwanza by the time unafungua hiyo kesi tayari utakuwa maiti sasa sijui nani ataifungua Mkuu?
Unadhani tuko Uturuki hapa chama tawala kinafutwa?Hata siku moja hizo ni ndoto zisizotimilika!
 
Pundamilia07

Pundamilia07

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2007
Messages
1,433
Likes
12
Points
135
Pundamilia07

Pundamilia07

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2007
1,433 12 135
Very Ironical!
Over my dead body kama watakifuta!kwanza by the time unafungua hiyo kesi tayari utakuwa maiti sasa sijui nani ataifungua Mkuu?
Unadhani tuko Uturuki hapa chama tawala kinafutwa?Hata siku moja hizo ni ndoto zisizotimilika!
Kevo,
Usimkatishe tamaa, anaweza kupata ushauri zaidi kutoka kwa Mch. Mtikila
 
M

Major

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2007
Messages
1,425
Likes
1,156
Points
280
M

Major

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2007
1,425 1,156 280
ukitaka kuwa jambazi,au ukitaka kuwa mhujumu uchumi wa nchi,au fisadi lililokubuhu au chinja chinja au mchuna albino ngozi usipate tabu wala usihofu wewe jiunge na ccm na uwakumbatie basi utakuwa salama kuliko papa benedict
 
MotoYaMbongo

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2008
Messages
1,898
Likes
269
Points
180
MotoYaMbongo

MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2008
1,898 269 180
I know kufuta CCM kisheria itakuwa ngumu sana, mi nafkiri njia rahisi ni sie vijana wenye uchungu na nchi yetu, tuanze mkakati wa kuingia jeshini kwa wingi, halafu tujiendeleze kielimu ili tushike nafasi za uongozi ktk jeshi na uofisa wa jeshi, sasa tukishaenea vizuri, kazi ni moja, kufanya mapinduzi ya kung'oa ili kung'oa CCM kwa faida ya wazalendo wa nchi hii. Kisha tukamate mafisadi wote na tukifute kabisa chama hiki na kusimamia uchaguzi ambao utaleta serikali makini ya kiraia kwa faida ya taifa letu. Hima vijana tuingie jeshini, wengine wametangulia na wameshaanza kutotii amri za wakubwa kama suala la nauli. Hii ndo njia itayotusaidia. Mungu tusaidie ili tuje tufanikishe mpango wetu huu.
 
W

wa hapahapa

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Messages
5,669
Likes
1,696
Points
280
W

wa hapahapa

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2012
5,669 1,696 280
aiseee....
 
isma isma

isma isma

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2015
Messages
497
Likes
339
Points
80
isma isma

isma isma

JF-Expert Member
Joined Oct 2, 2015
497 339 80
I know kufuta CCM kisheria itakuwa ngumu sana, mi nafkiri njia rahisi ni sie vijana wenye uchungu na nchi yetu, tuanze mkakati wa kuingia jeshini kwa wingi, halafu tujiendeleze kielimu ili tushike nafasi za uongozi ktk jeshi na uofisa wa jeshi, sasa tukishaenea vizuri, kazi ni moja, kufanya mapinduzi ya kung'oa ili kung'oa CCM kwa faida ya wazalendo wa nchi hii. Kisha tukamate mafisadi wote na tukifute kabisa chama hiki na kusimamia uchaguzi ambao utaleta serikali makini ya kiraia kwa faida ya taifa letu. Hima vijana tuingie jeshini, wengine wametangulia na wameshaanza kutotii amri za wakubwa kama suala la nauli. Hii ndo njia itayotusaidia. Mungu tusaidie ili tuje tufanikishe mpango wetu huu.
Vepe mkuu mpango wenu wa kuingia jeshini na kushika nafasi za juu umeshakamilika na vipi kwa upande wa kutokutiii amri nako mmeshaanza kuleta mgomo huko jeshini ????
 
cheguevara

cheguevara

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Messages
935
Likes
368
Points
80
cheguevara

cheguevara

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2012
935 368 80
Ndoto za mwendawazimu kabisa sera mmeshindwa kuuza
 
crabat

crabat

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2012
Messages
4,262
Likes
879
Points
280
crabat

crabat

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2012
4,262 879 280
Naunga mkono hoja.
Kama ccm haikufutwa kabisa isiwepo zaidi pale makumbusho basi nchii hii itakua nyuma.
Rwanda wametuwacha
Uganda tumewapiga vita wanatuacha
Kenya wanatuacha
Somali hiooo nayo inatuwacha
Jibu moja ccm ifutwe kabisa ilo nchi iondokane na nuksi...
 
W

wa hapahapa

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Messages
5,669
Likes
1,696
Points
280
W

wa hapahapa

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2012
5,669 1,696 280
ccm ni kikwanzo cha maendeleo....
 
ijooo

ijooo

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2017
Messages
702
Likes
1,022
Points
180
ijooo

ijooo

JF-Expert Member
Joined May 13, 2017
702 1,022 180
Naunga mkono hoja.
Kama ccm haikufutwa kabisa isiwepo zaidi pale makumbusho basi nchii hii itakua nyuma.
Rwanda wametuwacha
Uganda tumewapiga vita wanatuacha
Kenya wanatuacha
Somali hiooo nayo inatuwacha
Jibu moja ccm ifutwe kabisa ilo nchi iondokane na nuksi...
Duuh unajua watanzania ni waoga kuliko uwoga wenyewe sjapata kuona duniani mtu anaumizwa na anaogopa kusema na kupinga uonevu ccm 50+ yrs ni walewale ni upuuzi mpk umepitiliza sasa na dharau na ubabe juu God dont pull the trigger fingers do its time they taste their own medicine......
 
Forum statistics

Threads 1,238,015
Members 475,830
Posts 29,309,675