Salama na Fatma Karume (Shangazi)

Ana mume,hata kwenye interview kaweka wazi,Jaribu kuitafuta YouTube.
Na huyo mume wake walikutana kipindi fatuma ana miaka 16, kwa sasa Fatuma ana miaka 51. watoto hajaongelea so naamini atakuwa nao.
Hahaaa.... Unamwambia wengine waende YouTube huku N ww hujamsikiliza Kumbe..

Kasema moja kati ya happiest moments ni kukaa na familia yake yaani watoto wake wawili mmoja wa kike mwengine wa kiume na housegirl....
 
Wanahabari wa Tanzania wengine ovyo sana.

Unamuita mtu kwenye mahojiano, anataka kufunguka, halafu unamkataza mengine asiongee?

Upumbavu gani huu?

Inategemeana kiongozi. Tz ya leo sio ya zamani. Unaweza sababisha kituo kufungwa kwa sababu ya interest fulani... tumebana uhuru wenyewe..
 
Hahaaa.... Unamwambia wengine waende YouTube huku N ww hujamsikiliza Kumbe..

Kasema moja kati ya happiest moments ni kukaa na familia yake yaani watoto wake wawili mmoja wa kike mwengine wa kiume na housegirl....
Mkuu nimeingalia mara mbili nikiwa nyumbani EATV ambapo hicho kipindi cha salama hurushwa,ila mara zote sijaiangalia mwanzo na baadhi ya vipande kwa sababu kadha wa kadha.
Mara ya kwanza nilikuwa na mgeni so concentration ilikuwa kidogo,na mara ya pili niliifuma imeshaanza so ukichangia na vikazi nilivyoluwa nafanya nilikuwa nakosa ku-catch kila kitu.
Nimemshauri aende Youtube kwa sababu baada ya kurushwa kwa Tv huwa baadae wana-upload huko,ndio maana kuna watu waliitafuta huko baada uzi kuletwa hapa na kuikosa inamaana ilikuwa haijawekwa.
Unaponishutumu sijaangalia,unakuwa unakosea maana hizo taarifa za umri wake na kipandi amekutana na mume wake(wakati huo wakiwa marafiki) lilikuwa swali la mwisho mwisho.
 
Salama anawahoji kupitia TV ipi?
EATV kila Halhamisi saa tatu usiku, ila uwa anachanganya changanya anahoji wasanii zaidi na vijana wenye influence kama yule dogo ambaye ameanzisha brand yake ya vifaa kwa kushirikiana na investors na designers wa vifaa toka silcon valley
 
Jana nimebahatika kutazama kipindi cha Salama Jabir akipiga story na Fatuma Karume.

Wamezungumzia mambo mengi ila mimi kwangu hasa nilichokiona kwa Shangazi ni kwamba ni mtu ambaye hana furaha (ni mtazamo wangu) kutokana na muonekano wake. Na hii ninahisi inasababishwa na mtazamo wake kuhusu mambo yanayoendelea hasa akilalamika sana kuhusu mfumo wa kutoa haki hasa mahakama kuwa hazifanyi kazi kwa haki na kuwa kama mhimili unaojitegemea.

Pia, katika maelezo yake nahisi jambo lingine linalomsumbua, ni kwamba anaona kuna watu wanaonewa wanakandamizwa na hawajui kama wanaonewa wala kukandamizwa bado wanaona kila kitu ni sawa na hata ukiwaeleza hawaelewi unachowaeleza. Hili jambo uwa linawasumbua wengi nadhani Zitto akiwa mmoja kati ya watu ambao uwa wanachambua mambo ambayo wengi uwa hawayaelewi na wala kumsikiliza.

Pia, alijaribu kughusia kuhusu ofisi yao kuchomwa moto japo Salama alimuwahi akamwambia hataki kwenda huko na pia aligusia kuwa kafungiwa kufanya shughuli za uwakili, na akaendelea kuwa anaishi kwa kufanya shughuli za arbitration huko Uingereza na ni shughuli aliyokuwa akiifanya hata kabla hajaanza kufanya masuala ya uwakili Tanzania.

Ilikuwa interview nzuri nilipata kumfahamu zaidi huyu shangazi. Mungu ampatie maisha marefu huyu mwanamama.

Wajinga ndio waliwao.
 
Ana mume,hata kwenye interview kaweka wazi,Jaribu kuitafuta YouTube.
Na huyo mume wake walikutana kipindi fatuma ana miaka 16, kwa sasa Fatuma ana miaka 51. watoto hajaongelea so naamini atakuwa nao.

Amesema anao wawili, wakiume na wa kike.

Nampenda sana shangazi sababu ni mwanamke smart kichwani, tough, na ni mzuri pia kwa muonekano, Nimempatia picha akiwa mahakamani alivyo mtata. Ni mwalimu mzuri anaweza kueleza kitu ukaelewa.

Nimeobserve kuwa kuna vitu anajicontradict, lakini pia ana twist mambo kwa maslahi yake (Nafikiri ni asili ya mawakili wote)
 
Kuna saa huwezi kumuelewa mtu aliyekulia maisha ya juu hata kama anakueleza ukweli unabaki kuona anakusimanga,anakusumbua,hajui shida zako bali anaigiza kuzifahamu. Hali anayopitia shangazi ni hali wanayopitia wengi.

Angalia wataalam wa masuala ya watoto,wamama wakishafahamu huyo mtaalam hana au hajawahi kuwa na mtoto basi wanaona hafai hata kama ana utaalam wa kiasi gani.

Nakuelewa.

Mimi pia huwa nawashangaa wale wanawake wanaofundishwa jinsi ya kukaa na mume (kwenye kitchen party), huku mfundishaji hana mume.
 
Jana nimebahatika kutazama kipindi cha Salama Jabir akipiga story na Fatuma Karume.

Wamezungumzia mambo mengi ila mimi kwangu hasa nilichokiona kwa Shangazi ni kwamba ni mtu ambaye hana furaha (ni mtazamo wangu) kutokana na muonekano wake. Na hii ninahisi inasababishwa na mtazamo wake kuhusu mambo yanayoendelea hasa akilalamika sana kuhusu mfumo wa kutoa haki hasa mahakama kuwa hazifanyi kazi kwa haki na kuwa kama mhimili unaojitegemea.

Pia, katika maelezo yake nahisi jambo lingine linalomsumbua, ni kwamba anaona kuna watu wanaonewa wanakandamizwa na hawajui kama wanaonewa wala kukandamizwa bado wanaona kila kitu ni sawa na hata ukiwaeleza hawaelewi unachowaeleza. Hili jambo uwa linawasumbua wengi nadhani Zitto akiwa mmoja kati ya watu ambao uwa wanachambua mambo ambayo wengi uwa hawayaelewi na wala kumsikiliza.

Pia, alijaribu kughusia kuhusu ofisi yao kuchomwa moto japo Salama alimuwahi akamwambia hataki kwenda huko na pia aligusia kuwa kafungiwa kufanya shughuli za uwakili, na akaendelea kuwa anaishi kwa kufanya shughuli za arbitration huko Uingereza na ni shughuli aliyokuwa akiifanya hata kabla hajaanza kufanya masuala ya uwakili Tanzania.

Ilikuwa interview nzuri nilipata kumfahamu zaidi huyu shangazi. Mungu ampatie maisha marefu huyu mwanamama.

Atulie tu ale pension ya mzee wake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom