Salama kwa Rais Samia: Baada ya ma-DED sasa nguvu ihamie kwenye Mipango ya Halmashauri na Wizara

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
1627935170156.png

Muhtasari murua wa Mpango wa Maendeleo wa Tatu wa Tanzania wa 2021-2026, (Chanzo: FYDP III, uk. 161).

Nimeona mkeka wa ma-DED leo. Huu ni mkeka wa nne tangu Rais Samia akalie kiti cha U-rais. Mikeka iliyotangulia ni ile ya mawaziri, ma-RAS, na ma-DC.

Hivyo, hii ni hatua nzuri katika harakati za kiongozi mpya ofisini kutengeneza timu yake.

Nampongeza Rais kwa hatua hii, kwani itapunguza unyanyapaa wa baadhi ya wananchi dhidi ya serikali anayoiongoza, hasa katika ngazi ya Halmashauri.

Nikiwa natekeleza kazi zangu kama mtafiti na mchambuzi huru wa masuala ya siasa za kitaifa, na ambaye amechagua kuunga mkono Timu Samia kwa njia ya hoja zenye ushahidi, sasa napendekeza yafuatayo:

1. Mpango wa maendeleo wa Taifa (2021-2026) nimeuona, kuusoma na kuuhakiki kabla na baada ya toleo la mwisho. Sasa FYDP III imekaa vizuri.

Nimependa sana ukurasa ule wa 161 kama nilivyoupiga picha na kuuweka hapo juu. Bado mipango mikakati ya Wizara. Mawaziri Wasimamiwe ili wakamilishe kazi hii haraka.

Mipango hiyo itampa Rais msingi wa kusimamia utendaji kazi wao. Huu mpango wa Taifa uliozindulizwa majuzi hauna ufafanuzi wa kina kwa kila Wizara wenye kuonyesha nani atafanya nini, lini, kwa vipi, na kwa nini.

Lakini pia, bado utekelezaji wa communication and visibility plan. Watu wengi hawafahamu mpango huu. Serikali iweke nguvu katika eneo hili la stakeholders engagement.

2. Kuna ombwe la mipango mikakati katika Halmashauri zetu nyingi. Hivyo, Rais aagize ma-DED wapya washirikiane na ma-DC kuandaa Mabaraza ya Mashauriana ya Wilaya (DCC) ili kuandaa mipango ya maendeleo ya wilaya zetu ili hatimaye ipitishwe na vikao vya Kanseli.

3. Rais asisahau kufanyia kazi suala la ma-OCD na ma-WEO. Hawa na ma-DED aliowapumzisha lao moja. Mbele ya macho ya jamii watu hawa ma-OCD na ma-WEO hawakubaliki kwa sababu ambazo nimekwishazisema huko nyuma.

4. Kuna watu makini walitolewa serikali kuu na kutupwa serikali za pembezoni kwa kuwa walitoa ushauri mzuri lakini haukupendwa na hayati Magufuli. Watafutwe na kurejeshwa metropolitan ili wamsaidie kazi Rais mpya.

Natoa mfano mmoja. Profesa Kamuzora, RAS wa Kagera alikumbwa na visanga viwili. Kwanza, alikuwa mjumbe wa bodi ya TTCL. Akakataa kusaini andiko Fulani kwa kuwa aliona halina maslahi kwa Taifa. DG wa TTCL, anaitwa Waziri Kindamba, anajua alikokwenda kumchongea. Kamuzora alitukanwa kama mtoto.

Pili, Kamuzora aliandika expert opinion kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo na kusema mradi unafaa. Baada ya andiko lake kufika kwa Raia namba moja hakuamini alichoambiwa. Baadaye akatupwa huko kwenye u-RAS. Wako wengine kadhaa waliokumbwa na masaibu haya, lakini vichwani mwao wanayo madini. Watafutwe.

Baada ya kusema hayo, kwa leo sina mengi. Nitakuwa nafuatilia utekelezaji wa mipango ya serikali katika maeneo hayo hapo juu.

Baada ya kupata unafuu wa ratiba nitatekeleza ile ahadi yangu ya kufanya SWOT analysis na TOWS analysis ya serikali ya awamu ya sita kabla ya 19 Septemba 2021, yaani, tathmini ya kipindi cha miezi sita ya kwanza.

Kazi iendelee kwa kasi na viwango.
 
Suala kubwa ni katiba mpya, hizo nyingine ni bra bra tu
 
Suala kubwa ni katiba mpya, hizo nyingine ni bra bra tu
Katiba?
Swali: Kama Katiba ikiwa na vifungu vizuri tukawa na Rais hataki kuvifuata, kama alivyokataa hayati Magufuli, kinga yetu iko wapi?
 
Itakuwa kama US Trump alipojaribu kung'ang'ania madarakani aliposhindwa uchaguzi au kutumia ofisi yake kumchafua mpinzani wake Biden kule Ukraine.

Kwani hapa Ndugai alishindwaje kuwa na msimamo kama wa Nancy Pelos?
Hebu chimba chimba zaidi ukweli uamke...
 
Mwenyekiti wa Chama akimfuta uanachama wake anapoteza ubunge na uspika wake. Nancy Pelosi hata akihama chama bado anabaki na uspika wake hadi muda wake uishe. Trump hawezi kupitish bajeti yoyote bila Nancy Pelosi( Trump alikuwa analetewa bajeti na Pelosi asaini kama anaona inafaa, wajadiliane wafikie muafaka kama anaona haifai au afunge serikali yake kama hataki hayo yote mawili).

Naona kama kichwa chako kina madini fulani vile!
 
Back
Top Bottom