Salama Kikwete na Michelle Obama wanatufundisha nini hapa?

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
SALMA+2.JPG

Mke wa rais, Salma Kikwete akimwagilia maji mti alipotembelea kituo cha kulea watoto cha SOS jijini Dar Es Salaam. Kinachogomba ni huyu mama kuwekewa mkeka kusimamia ili kumwagilia maji. Inashangaza viongozi wetu na wake zao wanavyoogopa udongo ilhali wametokea huko. Na isitoshe utajiri wanaochuma toka kwetu unatokana na udongo huu huu. Je huu ni mfano gani kwa vijana wetu kuhusu kupenda udongo na kufanya kazi za mikono? Ajabu huyu ni mke wa mtu anayejigamba kutetea sera yake ya Kilimo Kwanza. Hapa ni Kilimo Kwanza au Usafi Kwanza? Hivi nani anawashauri watawala wa namna hii ambao wnaishi kwenye Alinacha na dunia feki? Kwanini hawakujifunza kwa watawala walioonja chungu ya kuishi kwa kujidanganya kama Muamar Gaddafii ambaye hakuwa akijua kuwa walibya walikuwa wakimchukia hadi kumuu kwa kipigo kama mwizi? Nisaidieni jamani.

  • thumbnail.aspx
  • michelle-obama-garden-062010-590-494x329.jpg
  • original.jpg

Mimi naona hapo inatuonesha mmoja ana asili ya utumwa na mmoja ana asili ya umwinyi.
 
haya ni matatizo sana,,,,kila mtu hapa kwetu anataka kuheshimiwaheshimiwa tu, mbona baba wa taifa aliyafanya yote na watanzania twamkumbuka hadi leo, mifumo hii ihatufanya tumweshimu mke wa rais kama ndiye rais, sembuse rais makini naye hawez fanya hivi. hivi huu utaratibu wa kujikweza ndiyo nn? watu kama hawa elimu za bahati nasibu ndo mana hawana ustaarrabu...................
 
Mie naona mmoja ni limbukeni na mwingine mchapakazi. Hapa ndipo siri ya uombaomba wa nchi za kiafrika ulipo. Tunatawaliwa na watu wasiostahili hata kuwa wajumbe wa nyumba kumi achia mbali vyeo vya juu. Tanzania ni nini ikilinganishwa na Marekani? Wenye akili wataelewa.
 
haya ni matatizo sana,,,,kila mtu hapa kwetu anataka kuheshimiwaheshimiwa tu, mbona baba wa taifa aliyafanya yote na watanzania twamkumbuka hadi leo, mifumo hii ihatufanya tumweshimu mke wa rais kama ndiye rais, sembuse rais makini naye hawez fanya hivi. hivi huu utaratibu wa kujikweza ndiyo nn? watu kama hawa elimu za bahati nasibu ndo mana hawana ustaarrabu...................

Hivi mgeni wako aje umtandikie mkeka asiutumie si itakuwa kakutukana. Kwani huyo mama huwa anatembea na huo mkeka? wacheni ushamba, huo ustaarabu wewe unaujuwa au unausikia tu?
 
ndugu yangu zomba uwe unasoma kwa umakini bas,,,,,,,,kuna neno MFUMO nimelisema sana.........the system at work ndo ya kiaina, asa huelewi nini mpaka wajibu kiselasela tu,,,,,mfano hai umeoneshwa hapo..............tujibu hoja co maneno ya sokoni
 
Hoja "0" hujibiwa kwa mleta hoja kupewa darsa la nguvu.
 
Kama kuna ndoa inayoongoza kwa kuombaomba hapa duniani basi ni ya jakaya na salma. Pamoja na rekodi hiyo ndiyo ndoa inayoongoza kwa kujishaua kwa mavazi na ubishololo wa kila aina hapa duniani utadhani ni vijana waliooana juzi. Tunashukuru sana Mpayukaji kwa kupost picha za binadamu hao wawili ambao mmoja anaoishi nchi tajiri kuliko zote duniani na mwingine anaishi nchi maskini kuliko zote duniani lakini aina ya maisha wanayoishi inaakisi kinyume chake. Hata zingekuwa picha za jakaya na obama hali ingekuwa hiyohiyo.
 
mmoja ni msanii anayeogopa ardhi aliyotokea na kutuaminisha kuwa hatakuja kufa siku moja na mwingine ni mtu halisi anayeishi kihalisia haogopi ardhi aliyotoka lwani siku moja anajua atarudi hulo
 
Hivi mgeni wako aje umtandikie mkeka asiutumie si itakuwa kakutukana. Kwani huyo mama huwa anatembea na huo mkeka? wacheni ushamba, huo ustaarabu wewe unaujuwa au unausikia tu?
Hapana,

Nadahanai umewahi kusikia viongozi waliokataa kukalia viti walivyoandaliwa na viskbadilishwa. Kapteni Sankara alikuwa anajulikana sana kwa kukataa yale aliyoandaliwa kama rais ili ajumuike na raia wake kama raia mwingine. Nyerere alikuwa anabidlisha mara nyingi sana route za ziara zake za mikoni na kuishia kwenda ambako hakuwa ameandaliwa kwenda.

Mwacheni mama wa watu ale raha, kwani hilo ndilo lililoko ndani ya ukoo ule; nasikia kunako miaka ya 2007, mama Regina Lowassa aliwahi kuambia asubiri wakati wake kwani kila mtu atakula kwa zamu yake.
 
SALMA 2.JPG

Mke wa rais, Salma Kikwete akimwagilia maji mti alipotembelea kituo cha kulea watoto cha SOS jijini Dar Es Salaam. Kinachogomba ni huyu mama kuwekewa mkeka kusimamia ili kumwagilia maji. Inashangaza viongozi wetu na wake zao wanavyoogopa udongo ilhali wametokea huko. Na isitoshe utajiri wanaochuma toka kwetu unatokana na udongo huu huu. Je huu ni mfano gani kwa vijana wetu kuhusu kupenda udongo na kufanya kazi za mikono? Ajabu huyu ni mke wa mtu anayejigamba kutetea sera yake ya Kilimo Kwanza. Hapa ni Kilimo Kwanza au Usafi Kwanza? Hivi nani anawashauri watawala wa namna hii ambao wnaishi kwenye Alinacha na dunia feki? Kwanini hawakujifunza kwa watawala walioonja chungu ya kuishi kwa kujidanganya kama Muamar Gaddafii ambaye hakuwa akijua kuwa walibya walikuwa wakimchukia hadi kumuu kwa kipigo kama mwizi? Nisaidieni jamani.

  • thumbnail.aspx
  • michelle-obama-garden-062010-590-494x329.jpg
  • original.jpg

Huu wote ni ulimbukeni wa waandaji wa shughuli yote hiyo! Nani aliwaagiza kuweka mkeka?

Cha zaidi hapa ni kujipendekeza tu na mazoea ya maandalizi ta Kitanzania.
Wakati mwingine viongozi hawa waalikwa tunawalaumu bure, ingawa walipaswa kukosoa hali kama hiyo!

Hivi, hujawahi kuona maandalizi yanayofanyika kabla ya ujio au ugeni maarufu hata katika maisha yetu ya kawaida? Unajiandaa kumhadaa mgeni kwamba hayo ndiyo maisha yako ya siku zote!

Ajabu, pale tunapohitaji msaada, tutajiandaa kupita kiasi, maandalizi lukuki, kiasi kwamba mgeni akifika, hawezi kuona tuna shida gani, na ni msaada gani unahitajika! Gharama kubwa zinazotumika, we acha tu!

Mwalimu Nyerere [RIP], aliwahi kusema kwamba, hakuwa anapendezewa na harufu za rangi zilizokuwa zikipakwa siku chache kabla ya ziara zake!
 
SALMA+2.JPG

Mke wa rais, Salma Kikwete akimwagilia maji mti alipotembelea kituo cha kulea watoto cha SOS jijini Dar Es Salaam. Kinachogomba ni huyu mama kuwekewa mkeka kusimamia ili kumwagilia maji. Inashangaza viongozi wetu na wake zao wanavyoogopa udongo ilhali wametokea huko. Na isitoshe utajiri wanaochuma toka kwetu unatokana na udongo huu huu. Je huu ni mfano gani kwa vijana wetu kuhusu kupenda udongo na kufanya kazi za mikono? Ajabu huyu ni mke wa mtu anayejigamba kutetea sera yake ya Kilimo Kwanza. Hapa ni Kilimo Kwanza au Usafi Kwanza? Hivi nani anawashauri watawala wa namna hii ambao wnaishi kwenye Alinacha na dunia feki? Kwanini hawakujifunza kwa watawala walioonja chungu ya kuishi kwa kujidanganya kama Muamar Gaddafii ambaye hakuwa akijua kuwa walibya walikuwa wakimchukia hadi kumuu kwa kipigo kama mwizi? Nisaidieni jamani.

  • thumbnail.aspx
  • michelle-obama-garden-062010-590-494x329.jpg
  • original.jpg

Kama hawa viongozi wanakuwa na kinyaa, kwanini wafanye hiyo kazi?? waache tu, huwa inapendeza kama akifanya uhalisia, sio acting!!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom