Salam za Mstahiki Meya Boniface Jacob kwa Mh Aikael Mbowe

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
363
557
Dear
Freeman Aikael Mbowe.

Salaamu na baada ya salamu,pole na mapambano ya kutufikisha "Canaan" kupitia ukombozi wa pili wa Taifa hili... Najua fika ujasiri na uimara wako wakati wote,sitishwi wala sijawahi kuwa na wasiwasi juu ya maamuzi na kila hatua unayopiga kuelekea mbele.

Ndiyo maana nipokuwa upande mmoja na wewe sitishwi na upepo wa kisulisuli,wala mvua za mabarafu,kwa kuwa najua ulivyosimama imara dhidi ya dhoruba na vimbunga,vya kusi na tonadozi

Walipokupokonya vitega uchumi vyako ulicheka huku mikono umeweka mifukoni,ukatuduwaza na kutuacha tukibubujikwa na machozi,walipokuja kujachufua hotel yako na ukwepaji kodi,ulituambia umechoka kuonewa huruma na kama hayupo tayari kukutana na haya tuachane na siasa za upinzani Africa,wiki baadae tunaona wamekufuata mpaka kwenye bustani za mchicha na nyanya,

Mimi na vijana wenzangu tulinyamaza kimya safari hii tukiogopa kufokewa tena na wewe,na baadae tulikumbuka maneno yako ambayo ulikuwa ukitusisitiza kuyakumbuka wakati wote. "Ni kweli wanaotutesa si wengi kama sisi tunaoteswa,ila kuingiza nguvu wakati huu no kihatarisha maisha ya wanyonge walioupande wetu,kwa nini tusisubirie watesi wetu wakiwa mahala salama kwetu,kuepusha maafa"

Na kwamba jeshi zuri si lile linaloshinda vita tuh,bali ni lile linaloshinda vita bila umwagaji damu na upotevu wa rasilimali zake nyingi,ingawa siku zote vita huacha wahanga.

Dear Freeman Aikael Mbowe,nasubiria kwa hamu command yako ya kusongambele,na nijaua si mimi tuh,nakuhakikishia vijana wenye utayari ni zaidi ya mamillioni,waona jeshi la adui lipo nje ya geti letu je na kuanza kuitikisa ngome yetu? Tuendelee kusubiria sauti yako kuu dhidi yao?

Vijana wako tupo tayari kukulinda kwa gharama yoyote hata kama ni damu na uhai wetu,ili makusudio ya ukombozi wa Taifa hili yafikie kama ilivuokusudiwa.

Marehemu mawazo,alipata kusema "wanaotudhalilisha na kututesa sana wanatuharakisha sana,kufika tunapo elekea"

Tabia za vyombo vya dolla ni zilezile tuh,kizazi na kizazi avitoamka na kuwa upande wetu milele

Je tuendelee kusubiria lingine zaidi ya hili au wakati ni sasa,? Askari wako Mtiifu
BONIFACE JACOB
senior councillor UBUNGO
MJUMBE KAMATI KUU CHADEMA
 
Mvumilivu hula mbivu.......Mimi bado naamini huu msemo, CDM haiwezi kusimamishwa na mbinu dhaifu kama hizo, labda watusingizie vijana wote wa chadema kuwa tunauza ngada kisha watufunge...........sijawahi kushawishiwa kwa chochote na CCM, na haitakaa inishawishi daima.
 
Mimi nilidhani anandika waraka wa kumuonya kwa tabia hiyooo, kumbe ni kumpongeza halafu na kumwita shuujaaa na huku mnasema mnataka mabadiliko kweli??
Kama anaonewa si atajitetea??
Kumbe wakitaja vidagaaa mnapiga kelele kwamba nyangumi wanaachwa. sasa wamewataja nyangumi halafu mnalialia.
Au hayo ndo yale mabadiliko mlio kuwa mna tangazia umaa??
 
Naona wanajikomba watu huku. Ila mwizi ni mwizi na muuza unga ni muuza unga tu.

Byebyeeeeeeeeeeeeeeeee Mbowe kwenye siasa maana ninyi kupakazia watu mnaona ndo dili za kisiasa.

Ukomae na wewe uone sindano inavyoingia.
 
nasubiria kwa hamu command yako ya kusongambele, na nijaua si mimi tuh, nakuhakikishia vijana wenye utayari ni zaidi ya mamillioni ... Tuendelee kusubiria sauti yako kuu dhidi yao?

Vijana wako tupo tayari kukulinda kwa gharama yoyote hata kama ni damu na uhai wetu

Vijana zaidi ya mamilioni! Thubutu, labda nyuma ya keyboard ...!

BTW, acha akajibu tuhuma tu.
 
Kumlinda mtu mwenye uhakika wa kula yake miaka dahari mbele yeye na familia yake kwa gharama ya damu/ uhai wangu ni mtihani nisiotaka kuufaulu.

Hasa hasa viongozi wa kisiasa na kidini.

Nitatetea kwa hoja, nikizidiwa hoja nitakiri na kukubali mtazamo wa mpinzani wangu kisha nitalala mbele.
 
Back
Top Bottom