Salam kwa mafisadi kutoka Korea

Bowbow

JF-Expert Member
Oct 20, 2007
541
30
Salam kwa mafisadi kutoka Korea.

Naye Lowassa akawaambia mawaziri wengine"
KESHENI mkiomba kwani hamjui siku wala saa atakayokuja Dr. Mwakyembe. Nami naenda mtaani kuwaandalia kijiwe ili nitakapokuwapo nanyi muwepo.

Nanyi muonapo tume zaundwa basi mtambue muda wa mavuno ya MAFISADI umekaribia".

Kisha akakwea tena Ikulu kuomba Rais asimfilisi. Lakini RICHMOND akatokea na jeshi la Mwakyembe na kusema " Nitakayembusu huyo ndie....!".Mara Chenge akatoa Upanga wake alani na kumkata mfuasi wa Mwakyembe(Anna Kilango) sikio. Lowassa akamwambia Chenge "rudisha upanga wako alani, Kikombe nilichotupiwa na Kikwete Sina budi Kukinywa"

Moja kati wa mayahudi wale aitwaye Selelii hakuamini kama Lowasa Kajiuzulu,akatwaa mkuki akamchoma ubavuni na tazama...Ikatoka gas ya songosongo na mafuta ya transfoma...Siku ya tatu wakaenda pale ofisini kwake..Lakini wakakuta wingu la Mvi limetanda na Suti ya mistarimistari pale kitini walipomweka..yule morani waliyemkuta getini akawaambia mnayemtafuta hayupo.....Ameshapaa kwenda Monduli na yupo kuume kwa Laiboni..Nao Wakasema..."Hakika huyu alikuwa Fisadi".
 
Salam kwa mafisadi kutoka Korea.

Naye Lowassa akawaambia mawaziri wengine"
KESHENI mkiomba kwani hamjui siku wala saa atakayokuja Dr. Mwakyembe. Nami naenda mtaani kuwaandalia kijiwe ili nitakapokuwapo nanyi muwepo.

Nanyi muonapo tume zaundwa basi mtambue muda wa mavuno ya MAFISADI umekaribia".

Kisha akakwea tena Ikulu kuomba Rais asimfilisi. Lakini RICHMOND akatokea na jeshi la Mwakyembe na kusema " Nitakayembusu huyo ndie....!".Mara Chenge akatoa Upanga wake alani na kumkata mfuasi wa Mwakyembe(Anna Kilango) sikio. Lowassa akamwambia Chenge "rudisha upanga wako alani, Kikombe nilichotupiwa na Kikwete Sina budi Kukinywa"

Moja kati wa mayahudi wale aitwaye Selelii hakuamini kama Lowasa Kajiuzulu,akatwaa mkuki akamchoma ubavuni na tazama...Ikatoka gas ya songosongo na mafuta ya transfoma...Siku ya tatu wakaenda pale ofisini kwake..Lakini wakakuta wingu la Mvi limetanda na Suti ya mistarimistari pale kitini walipomweka..yule morani waliyemkuta getini akawaambia mnayemtafuta hayupo.....Ameshapaa kwenda Monduli na yupo kuume kwa Laiboni..Nao Wakasema..."Hakika huyu alikuwa Fisadi”.

Huyu mshikaji ananifanya nianze kuamini kuwa Biblia ilikwishaongelea kila kitu kitakachotekea duniani. Kumbe jesus alikuwa anamwongelea Lowassa? Duh!!!!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom