Salakana aamua kumpinga Ndesamburo mahakamani

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,062
79,089
Salakana aamua kumpinga Ndesamburo mahakamani
Tuesday, 30 November 2010 21:16 0diggsdigg

Daniel Mjema, Moshi

ALIYEKUWA mgombea ubunge kupitia CCM Jimbo Moshi Mjini, Justine Salakana, amefungua kesi Mahakama Kuu kupinga ushindi wa Mbunge wa jimbo hilo, Philemon Ndesamburo (Chadema), akitaka kuitishwa kwa uchaguzi mdogo.
Salakana anayewakilishwa na Mawakili kutoka kampuni za MRL Lamwai & Co na BS Associates, amewasilisha hoja mbalimbali ikiwamo ya Paroko wa Kanisa Katoliki kushawishi waumini wake kutochagua CCM na wagombea wake.
Ndesamburo aliibuka mshindi baada ya kupata kura 28,697 akifuatiwa na Salakana wa CCM kura 16,972, Seif Madongo wa CUF kura 97, Godfrey Malisa wa TLP 54, Issack Kireti wa Sau kura 42 na Sungura wa NCCR Mageuzi kura 42.
Mgombea huyo analalamika kuwa asubuhi ya Oktoba 31, mwaka huu ambayo ilikuwa siku ya kupiga kura, Paroko wa Parokia ya Korongoni, Padri Apolinary Kiondo, aliwahubiria waumini wasiwapigie kura mafisadi na waliogawa fulana.

Katika hati ya madai, Salakana amemnukuu Padre Kiondo akitamka: "Msiwapigie kura mafisadi na wale waliowagawia fulana, kofia na skafu kwani hao ndio wanaoharibu nchi." Kauli anayodai ilimaanisha wapiga kura wasichague CCM.
Salakana analalamikia uchaguzi huo kuwa, ulitawaliwa na ukiukaji taratibu, ubaguzi na rushwa na kufanya uchaguzi usiwe huru na wa haki na kuomba mahakama kumzuia Ndesamburo kugombea kwa miaka kipindi cha mitano.
Pia, analalamikia matamshi ya Ndesamburo na mawakala wake kumuita yeye kuwa ni Mrombo, hana nyumba, amevamia Msitu wa Rongai na kutoa zawadi ya Sh2 milioni kwa mtu atakayeonyesha nyumba yake Moshi mjini.

Salakana analalamika kuwa, matamshi hayo yalimaanisha kuwa Mrombo kwa kabila, hakuwa na sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge, hivyo wapiga kura wakaacha kumchagua na kufanya uchaguzi huo kuwa batili kisheria.
Mgombea huyo amewasilisha kama vielelezo, nakala za magazeti ya Daily News, Mwananchi, HabariLeo, Tanzania Daima, Sema Usikike, Nipashe na Uhuru kuthibitisha kuwa matamshi hayo yalitolewa katika mikutano ya hadhara.
Wakati huohuo, mgombea mwingine kupitia NCCR Mageuzi, Faustine Sungura, amefungua kesi Mahakama Kuu dhidi ya Ndesamburo akidai ushindi wa mbunge huyo ulikuwa batili kutokana na kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi.
Katika kesi hiyo ya uchaguzi namba 1/2010, Sungura amemshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama mlalamikiwa wa kwanza na Ndesamburo mlalamikiwa wa pili.

Hata hivyo, katika kesi hiyo Sungura halalamikii matokeo, bali taratibu na kanuni za uchaguzi kuwa hazikufuatwa kupitisha wagombea wenzake sita na kwamba, ni yeye pekee aliyestahili kupitishwa na Nec.
Katika hati yake ya madai, Sungura anadai kuwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za Nec, wagombea ubunge walitakiwa warejeshe fomu zikiwa na picha ambazo zinamuonekano mweupe kwa nyuma.

Sungura ambaye hakuwahi kufanya mikutano ya hadhara ya kampeni kwa kipindi chote cha kampeni, amedai kuwa ni yeye pekee aliyerejesha fomu zilizokidhi sheria na kanuni za uchaguzi zilizoainishwa na Tume.
Mgombea huyo analalamika kuwa licha ya kuwawekea pingamizi na baadaye kuwakatia rufaa wagombea wenzake, Tume iliwaidhinisha kugombea wakati ikifahamu kuwa yeye pekee (Sungura) ndiye aliyestahili kupitishwa.

Katika hati hiyo ya malalamiko, Sungura anaomba mahakama itoe matamko matatu, moja Mahakama itamke kuwa kudhinishwa kwa wagombea wenzake sita kugombea ubunge Jimbo la Moshi Mjini ilikuwa batili.
Pia, Mahakama itamke kuwa kutangazwa kwa Ndesamburo kuwa mbunge ni batili, yeye ndiye alipaswa kuwa mgombea pekee na kwamba Mahakama imtamke yeye (Sungura) kuwa ndiye mbunge wa jimbo hilo.
Kesi hizo namba 1 na 2 zilizofunguliwa Alhamisi wiki iliyopita na juzi katika Mahakama Kuu Moshi, hazijapangiwa tarehe wala Jaji wa kuzisikiliza.

Salakana aamua kumpinga Ndesamburo mahakamani

My take
Kwa maoni yangu mhusika ana concrete grounds to advance his grievances... na inakuwaje watu wa Old Moshi ndio wanasifika kwa Ubaguzi katika Kilimanjaro iwe kwa Wa-Old Moshi wenzao kama Wauru na hii sasa kwa Mgombea mwenzake kisa anatokea Rombo. Hivi huyu Ndesamburo anayeweka watoto wake katika nafasi za Ubunge (Owenya na Kihwelu) ana hati-miliki ya kubagua watu? ana hati miliki ya jimbo la Moshi? Mbona Wabunge wengine wa Kilimanjaro waliopata kutokea CHADEMA na NCCR-Mageuzi hapo kabla hawajawahi kuweka familia zao katika uongozi? Mbona siskii Selasini akichagua mtoto wake kuwa Mbunge nafasi za viti maalum? Huyu Ndesamburo ana agenda gani na chama? kimekuwa familia sasa au? Ukiangalia vizuri wale waliohangaika kuanzisha chama hayupo katika list ya 1992 na hata 1995 hakuwepo hata kwenye chama, hii iko wazi, ghafla amekurupuka kinachofuata ni ubaguzi na upendeleo wa hali ya juu... kila mtu anafahamu ukimuunganisha na Mbowe, je ule utaratibu wa kubadili uongozi umeishia wapi? maana nachojua mimi kabla ya Waheshimiwa hawa kuingia madarakani kulishawahi kuwa na wakina Makani na Mtei na walitoka katika uongozi baada ya muda....Jamani demokrasia haimaanishi mwenendo huu tunaouna sasa ambapo ni dhahiri CHADEMA haiwezi kujitofautisha na CCM katika matendo nathani future yetu si nzuri kuna hiki kirusi kimeingia katika chama i.e. Undugunization we shouldn't walk blindly...ikumbukwe hata NCCR-Mageuzi ilikuwa at a peak at once na kilikufa kwa sababu ya kuhodhi madaraka (sababu great brains like Lamwai couldn't stand s1 like Mrema) na sasa tunaona wakina Ndesamburo wengii wanajitokeza na tambo za kuwa ni bora (+
watoto zao) na wana uchungu na chama kuliko wengineo......you know what something has to change!
 
+Hebu tuache upuuuzi mbona analalamikiwa Ndesanbulo tu nenda CCMhamuoni msururu wa wake na watoto wa vigogo walivyojazana bungeni,nadhani kikubwa iwe uwezo zaidi wa mtu lakini isiwe mtoto au ndugu ya kiongozi kama anauwezo asipewe.
 
Kama CHADEMA wako strategic hizo nafasi wangepewa watu kutoka majimbo yasiyo na representatives wao unaposema uwezo, ina maana wakina Zitto, Selasini, Nyerere na wengineo hawana ndugu au marafiki wenye uwezo? niambie huo uwezo wa Mh Owenya au Mh Kihwelu uliouona wa kuwafanya kushindwa kugombea majimboni ilhali wapo kwenye system muda woote na washawahi kuwa Wabunge (hasa Mh. Owenya!)! At least Dr Slaa naweza kum-tolerate maana Mh Kamili aligombea na akapata +21,000 votes kwa hiyo she represents the voice of that +21,000 votes entrusted her! au Mh Komu (wa Kigamboni) ambaye naye alipata 25,000+! Ndugu yangu, ni kushindwa kujitofautisha na CCM huko unakojifadhalisha nako ndo kutafanya chama kisifikie malengo unaposema Mbona so and so....anafanya hivi na vile ni sawa na ku-limit thinking horizon yako ya kuona ni kivipi chama kikimbie badala ya kutambaa! na it is a matter of time, kama mambo hayabadiliki wale great thinkers wataondoka kama ilivyokuwa wakina Dr Lamwai na NCCR-Mageuzi!
 
Kwa mawazo yangu, naona Chadema nao wamezidisha undugurization hawana tofauti na CCM. so i think they need to change alot to gain the wananchi confidence. Kwa post chache tu wamepeana wanandugu sasa ndio wangeshika nchi ingekuwaje!!!!!!!!!!!!!!.
 
Mfa maji..mwache atakuja kulipa fidia ya kesi huyo.
 
naomba uwaambie kuna msemo "kunya anye kuku akinya bata ameharisha..." nathani huo msemo unahusu wana CHADEMA haswa kwa wale wanaotetea swala la watu na watoto na wakwe zao kupewa viti maalum bila kuzingatia mustakabli wa chama kukua na juhudi binafsi za wanaozawadiwa viti hivyo katika kupata vile vya majimbo...nina msifu sana Bi Halima Mdee kwa alichofanya
 
Mfa maji..mwache atakuja kulipa fidia ya kesi huyo.
watu tusiwe na mapenzi ya upofu, suala la Ubaguzi lipo Kilimanjaro hata Komu wa Moshi Vijijini ameshindwa kwa vile ni M-huru na Wa-kibosho wakakataa kumpigia! sasa jiulize, hawa woote ni Wa-Old Moshi je tunyamaze kimya ilhali tunaona trend hii mbaya ya kansa ya ubaguzi wa sehemu atokako mgombea? Kunani na hawa Wa-Old Moshi?
 
Hii itakuwa ccm virus to demoralize our strong man ndesa pesa.salakana ni kweli hana nyumba moshi mjini na anaishi kwenye ghorofa la msajili tena jirani na tanesco moshi.anayebisha abishe.kwani kama hukugawa fulana na kofia kinachokuuma hapo ni nini?ukweli?
 
watu tusiwe na mapenzi ya upofu, suala la ubaguzi lipo kilimanjaro hata komu wa moshi vijijini ameshindwa kwa vile ni m-huru na wa-kibosho wakakataa kumpigia! Sasa jiulize, hawa woote ni wa-old moshi je tunyamaze kimya ilhali tunaona trend hii mbaya ya kansa ya ubaguzi wa sehemu atokako mgombea? Kunani na hawa wa-old moshi?
wacha kelele wewe wachaga hawana ubaguzi ila unachaguliwa kulingana na fedha unazomiliki na sio kuwa kiongozi wa dhiki ili utuibie?halafu kama huna pesa ni rahisi kunyamazishwa.unawajua ccm au unawadhania?
 
Uongozi na njaa wachaga ndo hatutaki.pesa mbele ndo maendeleo yatakuja.salakana hata wakiambiwa uchaguzi urudiwe leo tena bila kampeni hapati hata robo ya atakazopata mzee ndesa pesa a.k.a mbunge mpaka atakapoamua mwenyewe hataki tena.
 
Wewe kama kweli huyo Ndesamburo ana hela asingefanya mtaji viti maalum kuweka familia..! Na nakushangaa unavyosema so and so hana nyumba sijui hana fedha! Una uhakika? au hizo helicopter rightoff na hotel substandard za Ndesamburo zinakuchengua? mie nathani unaongea kiushabiki zaidi hata kama huna hela una haki ya kuwakilisha wenzio.. katiba haibagui, huu ndio ubaguzi wenyewe na usiseme Wachagga sema wa-Old Moshi wanaendekeza lana hiyo! Hiko chama kinachangiwa na wengi tu na hata kabla ya huyo Ndesamburo wako kujiunga nacho kilishakuwa na Wabunge kumfanya yeye kukipenda kwa hiyo ni umbumbu kufikiri ni mtu mmoja tu ndo amekifikisha hapo! unaweza dharau mchango na jitihada za Dr Slaa? mbona yeye hana hizo hela unazosema na tunajua mchango wake...
 
mfa maji haishi kutapatapa kwani hata uchaguzi ukirudiwa leo hii salakana hawezi kushinda. kuhusu paroko kuita CCM ni chama cha mafisadi hayo ni maoni yake ingawa mimi nakubaliana na maoni yake kuwa ni kweli. kila raia hata paroko anao uhuru wa kutoa mawazo yake binafsi mradi avunji sheria. kuhusu ukabila hakuna kitu kama hicho kwani hawa wote kabila lao ni wachaga kwahiyo hakuna ukabila. kuhusu salakana kuambiwa kwao ni rombo hilo ni kweli kuwa yeye ni mrombo ila kama ndesamburo alisema na kurekodiwa kuwa msimchague salakana kwa kuwa yeye ni anatoka rombo hilo ni kosa. kuhusu ndesamburo na hao watu wawili uliowataja wote hao SIYO WATOTO WA NDESAMBURO bali mmoja ni mfanyakazi wake na mwingine ni ameolewa na mwanae na kama alivyosema mhusika hapo juu hujui mchango wao ktk chama hivyo huna haki ya kuwashambulia na pili cha msingi ni uwezo wao na la mwisho ni kuwa kama wana uwezo halafu ukawaacha eti kwa kuwa ni mfanyakazi wa ndesamburo au katokea kuwa kaolewa
mtoto wa mzee ndesa HUONI KAMA HUO NI AINA NYINGINE YA UBAGUZI.
 
salakana anamatatizoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo,hata kama uchaguzi utarudiwa ndesa pesa atashinda tena,kwa hiyo ni kujisumbua tu.
 
wewe kama kweli huyo ndesamburo ana hela asingefanya mtaji viti maalum kuweka familia..! Na nakushangaa unavyosema so and so hana nyumba sijui hana fedha! Una uhakika? Au hizo helicopter rightoff na hotel substandard za ndesamburo zinakuchengua? Mie nathani unaongea kiushabiki zaidi hata kama huna hela una haki ya kuwakilisha wenzio.. Katiba haibagui, huu ndio ubaguzi wenyewe na usiseme wachagga sema wa-old moshi wanaendekeza! Hiko chama kinachangiwa na wengi tu na hata ya huyo ndesamburo wako kujiunga nacho kilishakuwa na wabunge kwa yeye kukipenda kwa hiyo ni umbumbu kufikiri ni mtu mmoja tu ndo amekifikisha hapo! Unaweza dharau mchango na jitihada za dr slaa? Mbona yeye hana hizo hela unazosema na tunajua mchango wake...
we chizi kweli mbona jk mweenyewe hana hata hiyo helcopta scrap wachilia mbali huyo kilaza salakana?pesa mbele mzeeee huelewi?salakana hata nyummba ya kuishi hana atamwongoza nani sasa?anakaa ghorofani na wahindi au ndo akishachaguliwa aanze na ujenzi binafsi wakati wananchi tunasubiri maendeleo?
 
mfa maji haishi kutapatapa kwani hata uchaguzi ukirudiwa leo hii salakana hawezi kushinda. kuhusu paroko kuita CCM ni chama cha mafisadi hayo ni maoni yake ingawa mimi nakubaliana na maoni yake kuwa ni kweli. kila raia hata paroko anao uhuru wa kutoa mawazo yake binafsi mradi avunji sheria. kuhusu ukabila hakuna kitu kama hicho kwani hawa wote kabila lao ni wachaga kwahiyo hakuna ukabila. kuhusu salakana kuambiwa kwao ni rombo hilo ni kweli kuwa yeye ni mrombo ila kama ndesamburo alisema na kurekodiwa kuwa msimchague salakana kwa kuwa yeye ni anatoka rombo hilo ni kosa. kuhusu ndesamburo na hao watu wawili uliowataja wote hao SIYO WATOTO WA NDESAMBURO bali mmoja ni mfanyakazi wake na mwingine ni ameolewa na mwanae na kama alivyosema mhusika hapo juu hujui mchango wao ktk chama hivyo huna haki ya kuwashambulia na pili cha msingi ni uwezo wao na la mwisho ni kuwa kama wana uwezo halafu ukawaacha eti kwa kuwa ni mfanyakazi wa ndesamburo au katokea kuwa kaolewa
mtoto wa mzee ndesa HUONI KAMA HUO NI AINA NYINGINE YA UBAGUZI.
acha ujinga wewe unataka kubisha Lucy Ndesamburo Owenya sio mtoto wa Ndesamburo? au unadhani tunaongea bila facts? tangu lini amekuwa Mfanyakazi na sio mtoto? na swala la uwezo sijui unamaanisha nini? maana ninavyojua uwezo unakuja na vihalalisho vya aliyofanya...kwa ujumla uchaguzi wao sio merited ndio nachoweza kusema !
 
Geza ulole yaani kwa hoja hizo umechemsha kama malaria sugu.ccm/salakana/jk na wengine wenye uhusiano nao hapa moshi ni kama kumrubuni mhafidhina kama malaria sugu ale nguruwe.hawauziki hata bure.huo ubaguzi unataka kuupenyeza hapa hauhitajiki cha msingi nijuavyo mimi wachaga na ccm ni ardhi na mbingu na ndo maana hata vunjo kashinda jogoo na siyo ccm.
 
issue hapa ni swala la ubaguzi na si kukubalika au la! nyie wa-Old Moshi mna dhambi ya ubaguzi! hilo halipingiki, mnavyombagua huyo salakana ati ni Mrombo mnahabri/mnajua hata mwanzilishi wa CHADEMA yenyewe ni Mrombo? au laana ya Ubaguzi inaendelea kuwaangamiza nyie watu wa Moshi Vijijini kuanzia wenyewe kwa wenyewe... nyie si ndio mliua NCCR-Mageuzi na Mrema wenu (Mwana-Moshi Vijijini wa Vunjo) na sasa kuna Mbatia anaisambaratisha TLP....au hujui hilo?
 
LUCY NDESAMBURO OWENYA SIYO mtoto wa ndesamburo bali ameolewa na mtoto wa ndesamburo na ndipo alipopata hilo jina la ndesamburo katikati, pamoja na hilo hiyo sio hoja hata kama ingekuwa kama hivyo unavyojaribu kulazimishia kuwa ni mwanae hilo sio tatizo la msingi ni michango na uwezo wake ndani ya chama kwani kumbuka kuwa chadema kabla ya umaarufu wake kilikuwa ni chama cha watu kujitolea zaidi since hujui michango na uwezo wake huna haki ya kumshambulia. unajua alijiunga lini na chadema?, amefanya nini kwenye chama ktk kipindi chote hicho? kama uwezi kujibu maswali haya siwezi kuunga mkono kumbagua mtu eti kwa kuwa ni mkwewe au mtoto wa fulani huo ni ubaguzi kwani unapochagua hautakiwi kutumia majina ya watu au mtoto wa nani? unless KITILA MKUMBO akisema alilazimishwa na NDESAMBULO kumchagua fulani bila hivyo hizo ni porojo za mitaani.
 
nathani nimekujibu hili, na uende ukalale great thinkers hawaleti uzushi humu ndani, na soma hapa na kwa taarifa yako hili liko wazi uache ubishi
Lucy Owenya: Ninastahili, sikubebwa | Gazeti la MwanaHalisi
 
asante sana GEZA ULOLE kwa source na nimekubaliana na wewe kuhusu uhusiano wake na ndesamburo lakini swali langu la msingi
ambalo nilisisitiza kwamba hata kama alikuwa mtoto wa ndesa hiyo siyo hoja ya msingi bali tunatakiwa kuangalia uwezo wake na michango ndani ya chama kwa SOURCE uliyotuma anaonekana ana elimu nzuri tu na anaonekana ni mtu anayefanya homework kisawa sawa kulingana na upeo wa maelezo yake kuhusiana na issue za viwanda lakini la misingi zaidi pia alijiunga na chama lini, michango yake ndani ya chama na SIYO ISSUE YA NANI AU MTOTO WA NANI ??
 
Back
Top Bottom