Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,174
Salakana aamua kumpinga Ndesamburo mahakamani Send to a friend Tuesday, 30 November 2010 21:16 0diggsdigg
Daniel Mjema, Moshi
ALIYEKUWA mgombea ubunge kupitia CCM Jimbo Moshi Mjini, Justine Salakana, amefungua kesi Mahakama Kuu kupinga ushindi wa Mbunge wa jimbo hilo, Philemon Ndesamburo (Chadema), akitaka kuitishwa kwa uchaguzi mdogo.
Salakana anayewakilishwa na Mawakili kutoka kampuni za MRL Lamwai & Co na BS Associates, amewasilisha hoja mbalimbali ikiwamo ya Paroko wa Kanisa Katoliki kushawishi waumini wake kutochagua CCM na wagombea wake.
Ndesamburo aliibuka mshindi baada ya kupata kura 28,697 akifuatiwa na Salakana wa CCM kura 16,972, Seif Madongo wa CUF kura 97, Godfrey Malisa wa TLP 54, Issack Kireti wa Sau kura 42 na Sungura wa NCCR Mageuzi kura 42.
Mgombea huyo analalamika kuwa asubuhi ya Oktoba 31, mwaka huu ambayo ilikuwa siku ya kupiga kura, Paroko wa Parokia ya Korongoni, Padri Apolinary Kiondo, aliwahubiria waumini wasiwapigie kura mafisadi na waliogawa fulana.
Katika hati ya madai, Salakana amemnukuu Padre Kiondo akitamka: Msiwapigie kura mafisadi na wale waliowagawia fulana, kofia na skafu kwani hao ndio wanaoharibu nchi. Kauli anayodai ilimaanisha wapiga kura wasichague CCM.
Salakana analalamikia uchaguzi huo kuwa, ulitawaliwa na ukiukaji taratibu, ubaguzi na rushwa na kufanya uchaguzi usiwe huru na wa haki na kuomba mahakama kumzuia Ndesamburo kugombea kwa miaka kipindi cha mitano.
Pia, analalamikia matamshi ya Ndesamburo na mawakala wake kumuita yeye kuwa ni Mrombo, hana nyumba, amevamia Msitu wa Rongai na kutoa zawadi ya Sh2 milioni kwa mtu atakayeonyesha nyumba yake Moshi mjini.
Salakana analalamika kuwa, matamshi hayo yalimaanisha kuwa Mrombo kwa kabila, hakuwa na sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge, hivyo wapiga kura wakaacha kumchagua na kufanya uchaguzi huo kuwa batili kisheria.
Mgombea huyo amewasilisha kama vielelezo, nakala za magazeti ya Daily News, Mwananchi, HabariLeo, Tanzania Daima, Sema Usikike, Nipashe na Uhuru kuthibitisha kuwa matamshi hayo yalitolewa katika mikutano ya hadhara.
Wakati huohuo, mgombea mwingine kupitia NCCR Mageuzi, Faustine Sungura, amefungua kesi Mahakama Kuu dhidi ya Ndesamburo akidai ushindi wa mbunge huyo ulikuwa batili kutokana na kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi.
Katika kesi hiyo ya uchaguzi namba 1/2010, Sungura amemshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama mlalamikiwa wa kwanza na Ndesamburo mlalamikiwa wa pili.
Hata hivyo, katika kesi hiyo Sungura halalamikii matokeo, bali taratibu na kanuni za uchaguzi kuwa hazikufuatwa kupitisha wagombea wenzake sita na kwamba, ni yeye pekee aliyestahili kupitishwa na Nec.
Katika hati yake ya madai, Sungura anadai kuwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za Nec, wagombea ubunge walitakiwa warejeshe fomu zikiwa na picha ambazo zinamuonekano mweupe kwa nyuma.
Sungura ambaye hakuwahi kufanya mikutano ya hadhara ya kampeni kwa kipindi chote cha kampeni, amedai kuwa ni yeye pekee aliyerejesha fomu zilizokidhi sheria na kanuni za uchaguzi zilizoainishwa na Tume.
Mgombea huyo analalamika kuwa licha ya kuwawekea pingamizi na baadaye kuwakatia rufaa wagombea wenzake, Tume iliwaidhinisha kugombea wakati ikifahamu kuwa yeye pekee (Sungura) ndiye aliyestahili kupitishwa.
Katika hati hiyo ya malalamiko, Sungura anaomba mahakama itoe matamko matatu, moja Mahakama itamke kuwa kudhinishwa kwa wagombea wenzake sita kugombea ubunge Jimbo la Moshi Mjini ilikuwa batili.
Pia, Mahakama itamke kuwa kutangazwa kwa Ndesamburo kuwa mbunge ni batili, yeye ndiye alipaswa kuwa mgombea pekee na kwamba Mahakama imtamke yeye (Sungura) kuwa ndiye mbunge wa jimbo hilo.
Kesi hizo namba 1 na 2 zilizofunguliwa Alhamisi wiki iliyopita na juzi katika Mahakama Kuu Moshi, hazijapangiwa tarehe wala Jaji wa kuzisikiliza.