Elections 2010 Salakana Aahidi Kufufua Viwanda

Wambugani

JF-Expert Member
Dec 8, 2007
1,757
276
Salakana aahidi kufufua viwanda
na Grace Macha, Moshi



MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Moshi Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Justin Salakana, ameahidi kama akishinda ataongea na Rais Jakaya Kikwete ili viwanda vilivyokufa ndani ya jimbo hilo viweze kufufuliwa .
Alitoa ahadi hiyo juzi, alipokuwa akihutubia mkutano wake wa kampeni kwenye viwanja vya zahanati ya Msaranga iliyopo Kata ya Ng'ambo.

Alisema anaamini Rais Kikwete atamsikiliza kwa kuwa ni mbunge aliyetokana na chama anachokiongoza hivyo akifufua viwanda hivyo vitasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya jimbo hilo.


Hata hivyo, kauli hiyo ameitoa kipindi ambacho serikali ilishajitoa katika kuendesha shughuli za kibiashara, jambo linalofanya utekelezaji wa ahadi hiyo kuwa ngumu.


Lakini kwa kipindi kirefu suala hilo limekuwa likishughulikiwa na mbunge aliyemaliza muda wake kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Philemon Ndesamburo, pamoja na uongozi wa mkoa.


Aliahidi kumaliza tatizo la mafuriko kwenye Kata ya Ng'ambo kwa kujenga mitaro ya kuhakikisha maji yote ya mvua yanaelekea mtoni.


Pia aliahidi kushughulikia tatizo la kukatika kwa umeme kunakosababishwa na watu kukata nyaya za kusambaza nishati hiyo.

======================

Hivi Mgombea Salakana haelewi kwamba Serikali katika Sera yake ubinafsishaji haihusiki na biashara ya viwanda?
 
Kufufua viwanda au kujenga viwanda vipya na vya kisasa kukidhi mahitaji na nguvu ya soko?Tuache porojo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom