Salaam za Uhuru: Kazi na Bata — Maana yake nini hasa?

Leo nilipanga kutoa salaam hizi za Uhuru kuwa Uhuru ni Kazi Lakini pia Kazi na Bata. Hata hivyo nilikuwa nina shughuli ya kihistoria huko Bahari Beach Hotel kulinda Uhuru wa Kufanya Siasa kwa kupinga muswada kandamizi wa Vyama vya Siasa unaopendekezwa na Serikali ya CCM. Basi jioni hii msome huku mkifurahia Uhuru na Bata ( kama zipo, Ila zitakuwepo baada ya Oktoba 2020 ).

====

Kazi na Bata — Maana yake nini hasa?

Zitto Kabwe

KATIKA mitandao ya kijamii na vyombo rasmi vya habari mwezi huu, kauli mbiu ya #KaziNaBata imepata msukumo mkubwa na nimekuwa nikipata maswali mengi kuhusu msemo huu unaojipatia umaarufu kila uchao.

Nimeona kwamba ni muhimu kwangu kutoa ufafanuzi wa msemo huu ili kwamba usipotoshwe au kupewa maana nyingine na watu ambao kwa namna moja au nyingine #KaziNaBata inawakera.

Siku zote, katika mapambano ya wanyonge kujikwamua kutoka katika makucha ya mfumo wowote, kumekuwa pia na ndoto ya kutaka kufaidi matunda ya jasho, machozi na damu yanayotokea wakati huo wa mapambano.

Kwenye kujikwamua kutoka katika makucha ya mfumo kandamizi, kunaweza kumaanisha hali bora za kiuchumi, heshima, haki na mambo mengine yanayoendana na hayo. Lakini mwisho wa yote, wanadamu watabaki kuwa wanadamu na watataka kufaidi matunda ya jitihada zao hizo.

Ni dhana ndiyo hasa ilikuwa msingi mkuu wa kauli mbiu maarufu ya wapigania haki za wafanyakazi mashuhuri wa karne ya 19 waliokuwa wakipigania mambo makubwa matatu tu kila uchao; “Saa nane za kufanya kazi, saa nane za kulala na saa nane za kufanya tunachotaka.

Mwaka 1912, kundi la wanawake waliokuwa wakifanya kazi katika mji wa Lawrence Massachusetts, uliokuwa kitovu cha viwanda vya kutengeneza nguo waligoma kufanya kazi kwa kudai malipo bora zaidi.

Ujumbe mkubwa uliokuwa umetamalaki katika mabango yao waliyoyabeba wakati wakiandamana ulikuwa ukisomeka “ Mikate na Mauaridi”. Kwa watafsiri wa misemo, ujumbe huo ulimaanisha kwamba watu wanataka kipato cha kuwatosheleza kula vizuri lakini pia kufanya mambo waliyokuwa wakiyapenda; jambo lililowakilishwa ipasavyo na alama hiyo ya uaridi.

Katika tafakari yake mujarabu kuhusu mapambano ya kudai Uhuru barani Afrika katikati ya k=arne ya 20, mwanamapinduzi kutoka Martinique, Ufaransa, Franz Fannon, alisema kwamba: “Kwa watu wanaotawaliwa, jambo lao la kwanza muhimu kwao ni ardhi yao. Ardhi ni muhimu kwa sababu ndiyo itakayowapa chakula na kulinda utu wao.”

Kwa kiasi fulani, tafakuri hiyo jadidi ya Fannon iliungwa mkono na mwanamapinduzi mwenzake wa Guinea-Bissau, Amilcar Cabral, aliyeshajiisha kwamba: “ Watu hupambana ili kuboresha maisha yao. Kuishi vema na kwa amani. Kuona wanaishi kwa muda mrefu na kwa maisha yenye kutia matumaini kuliko waliyokuwa wanaishi chini ya wakandamizaji.

Hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, naye kuna nyakati alionyesha wazi hisi zake katika mtazamo huu kwa kauli mbiu zake maarufu kama Uhuru na Maendeleo ambazo zilikuwa zikitekelezwa kwa vitendo kama ilivyokuwa kwenye vijiji vya Ujamaa –mfano mzuri zaidi ukiwa vilivyokuwa chini ya Ruvuma Development Association.

Kwa bahati mbaya, matamanio haya ya chakula, mauaridi na utu huwa hayapatikani. Hata katika utaratibu ule wa vijiji vya Ujamaa vilivyoanzishwa na serikali, utaratibu wa awali wa watu kukaa na kujipangia maendeleo yao ulivurugwa kwa mtindo mpya wa kupokea maagizo kutoka ngazi za juu.

Tangu aingie madarakani mwaka 2015, Rais John Magufuli ameibuka na kauli mbiu yake ya HapaKaziTu. Dhana hii ilijengwa katika msingi wa kupambana na rushwa ambayo ni tatizo kubwa hapa nchini na kauli mbiu ilitaka kutengeneza vuguvugu la kusafisha tatizo hilo na kuboresha utendaji wa serikali.

Kampeni hii ya Magufuli ilipokewa kwa moyo mkunjufu na walio wengi katika siku za awali za utawala wake ingawa sasa hali imebadilika na msisimko ule uliokuwepo sasa umegeuka kuwa fadhaa.

Badala ya vuguvugu hilo lenye kuleta matumaini ambalo aliahidi wakati wa kampeni za 2015 na katika siku zake za awali za urais, sasa hali imekuwa ya hofu.

Shughuli za kisiasa zimepigwa marufuku, wanasiasa wa Kitanzania sasa wanapigwa risasi na wengine wanatiwa nguvuni pasipo sababu za maana –huku waandishi wa habari na wanaharakati wakitoweka kusikojulikana, wanafunzi wenye mimba wakikataliwa kuendelea na masomo pasipo kusahau kadhia ya wavuvi, wafugaji na wakulima wanaotwezwa kupitia operesheni mbalimbali za kiusalama zinazoendeshwa na serikali hii.

Kwa upande mwingine, uchumi wa Tanzania unaelekea kwenye mserero wa kuporomoka na wananchi hawa wanyonge alioahidi kuwatetea ndiyo sasa wamegeuka kuwa wahanga wa kwanza wa siasa za Rais Magufuli.

Wamegeuka wahanga kwa sababu ahadi zinazotolewa na serikali kuhusu kuboresha sekta ya afya na elimu imebaki midomoni na kwenye makaratasi tu kwa sababu fedha zinazotangazwa kuwa zimepelekwa huko hazifanyiwi hivyo kibajeti. Kwa maana nyingine, ndugu zangu Waswahili wangesema zilongwa mbali, zitendwa mbali.

Utawala wa Rais Magufuli umeleta hali ngumu kiuchumi kiasi kwamba sasa kuna msemo mpya umeingia katika msamiati wa Kiswahili wenye kujaribu kuelezea kinachoendelea; Vyuma Vimekaza.

Kwa sababu ya ugumu unaoonekana katika maisha ya kila siku ya Watanzania, ile dhana ya HapaKaziTu aliyokuja nayo Magufuli sasa inachukuliwa kama ni neno la amri la kutaka mtu atekeleze jambo hata kama hataki kufanya hivyo.

Badala ya kuamsha amri ya uzalendo na kufanya kitu kwa matamanio makubwa ya yajayo mbeleni, HapaKaziTu imegeuka kuwa shuruti.

Mwanadahamu haishi kwa ajili ya kufanya kazi tu. Kwamba afanye kazi pasipo kuwa huru au kuona maisha yake yakibadilika hata kwa mambo ya kuonekana tu.

Kwa bahati nzuri, lugha ya Kiswahili, lugha adhimu ya taifa letu, tayari ina msamiti unaoleza kuhusu matamanio ya watu wake –Watanzania. Msemo wenyewe unasema “Kazi na Dawa”, ikimaanisha kwamba mtu yeyote anayefanya kazi, anatakiwa pia kuwa na jambo la kumpunguzia machungu na kumzawadia kwa jambo kubwa alilolifanya. Jambo la kujipongeza katika namna inayokubalika kisheria.

Jambo hilo sasa ndilo vijana wa kisasa wanaliita bata. Wahenga wetu waliliona hili miaka mingi kabla sisi wengine hatujaiona nchi yetu na vijana wetu wa sasa wanaliona hilohilo lakini katika lugha yao, muktadha wao.

Ukweli ambao haupingiki ni mmoja tu na umebaki hivyo kwa miaka yote; kwamba watu wanahitaji kufanya kazi lakini wanahitaji pia chakula mezani, wanahitaji kupendwa, wanataka uhuru wao, kutimiza haja zao, kuwa na maisha mazuri na kuwa na uhakika wa maisha yao ya sasa na baadaye.

Huu ndiyo ubinadamu. Huo ndiyo Utanzania. Kazi na Dawa, Kazi na Bata.

Watu wanahitaji kufanya kazi. Watu wanahitaji kufurahia maisha.

Huna maana niliambiwa wewe ni kibaraka wa ccm nikakataa lakini kumbe ulikuwa kibaraka wa jk na membe.ungekuwa na dhamira ya kweli ya kuwasaidia wananchi maskini usingetumika kisiasa.hayo yote uliyoyaandika hayana maana sababu dhamira ya kuwasaidia watanzania hauna.mwaka 2015 ukiwa katika uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu ulituambia benard membe alipewa mabilioni ya fedha na aliyekuwa Rais wa libya Mohamed gadafi zikiwa ni msaada kwa serikali ya Tanzania na hakuziwasilisha na badala yake amezifanya ni zake(ufisadi). Leo hii unatueleza upumbavu wako wa kazi na bata na baba yako membe yaani sasa hivi sio yule uliyetusimulia mwaka 2015.
 
Hoja zako zinachekesha. Heri wakoloni, au!

Kwa uelewa wako unadhani mkoloni lazima awe mzungu. Kwa taarofa yako ukoloni ni tabia, ni bora mkoloni mweupe kuliko huyu mweusi tuliyenaye. Ukitaka kuamini nenda Africa Kusini kaangalie maendeleo aliyoleta mkoloni mweupe, kisha njoo fananisha na maendeleo tuliyopata sisi baada ya kuwaondoa wazungu.
 
Kwa kuwa sijui umri wako nashindwa kukuweka kwenye nyakati gani za nchi hii umezaliwa na uzoefu wako wa maisha. Ila fikra na mawazo yako hayo yananielekeza kujua kiwango chako cha uelewa wa Taifa la Tanzania lilipotoka, lilipo na linapokwenda.
 
Hiyo ni kauli mbiu ya kihuni!!! haina uhalisia kwa nchi za kiafrika hata wazungu hawawezi kushabikia upuuzi huo
 
Ni Tanzania ambako wanasiasa wanatumia muda mwingi kujadili vibwagizo (slogan) vya uchaguzi mkuu miaka miwili kabla ya Uchaguzi!

Mwanasiasa kama Lowassa huwezi kumsikia leo anasema Mabadiliko Lowassa, Lowassa Mabadiliko kwa sababu huo muda wa chagizo umepita. Anajua 2020 atakuja na slogan nyingine pamoja na kuwa slogan ya 2015 ilikuwa maarufu. Hii ina maana kuwa, hoja ya msingi sio slogan za uchaguzi bali sera na Ilani ya Uchaguzi.

Wamarekani wengi kwa sasa hawajadili tena Make America Great Again kwa sababu kwa sasa sio kipaumbele.

Kwa sasa tunataka kushawishiwa tuanze kujadili chagizo la Uchaguzi badala ya Sera au Ilani za Uchaguzi.

Tanzania kuna vituko!

Wanasiasa wanataka kufanya siasa nyepesi nyepesi kwa sababu wamekosa uwezo wa kushawishi wananchi wengi kuhusu Sera za vyama vyao.

Leo hii ukiuliza watu wengi mitaaani kuhusu sera za Act-Wazalendo hawawezi kukupa jibu sahihi lakini kiongozi mkuu wa chama anataka kueneza kwanza kibwagizo cha uchaguzi mkuu. This is fun to say the least!

Kazi na bata mkuu, ndio stori ya mujini, kama hutaki fyeka kule.
 
Mh Zito mpeleke muswada wa vyama vya siasa kwa nchi marafiki dunia nzima waone ushenzi wa serikali hii! Tuma ujumbe the whole world to get them informed of gross democracy violation by this regime! hata UN tuma ujumbe kama mtu unanvyo toss coin!
Wakishapeleka kitokee nini?Yaani wahusika mnashinda nyuma ya keyboard, mzungu ndio aje awapambanie?
 
Ni Tanzania ambako wanasiasa wanatumia muda mwingi kujadili vibwagizo (slogan) vya uchaguzi mkuu miaka miwili kabla ya Uchaguzi!

Mwanasiasa kama Lowassa huwezi kumsikia leo anasema Mabadiliko Lowassa, Lowassa Mabadiliko kwa sababu huo muda wa chagizo umepita. Anajua 2020 atakuja na slogan nyingine pamoja na kuwa slogan ya 2015 ilikuwa maarufu. Hii ina maana kuwa, hoja ya msingi sio slogan za uchaguzi bali sera na Ilani ya Uchaguzi.

Wamarekani wengi kwa sasa hawajadili tena Make America Great Again kwa sababu kwa sasa sio kipaumbele.

Kwa sasa tunataka kushawishiwa tuanze kujadili chagizo la Uchaguzi badala ya Sera au Ilani za Uchaguzi.

Tanzania kuna vituko!

Wanasiasa wanataka kufanya siasa nyepesi nyepesi kwa sababu wamekosa uwezo wa kushawishi wananchi wengi kuhusu Sera za vyama vyao.

Leo hii ukiuliza watu wengi mitaaani kuhusu sera za Act-Wazalendo hawawezi kukupa jibu sahihi lakini kiongozi mkuu wa chama anataka kueneza kwanza kibwagizo cha uchaguzi mkuu. This is fun to say the least!
Nachojua slogan inatakiwa iwe expressive na sio hadi uandae desa kuielezea.
 
Kwa kuwa sijui umri wako nashindwa kukuweka kwenye nyakati gani za nchi hii umezaliwa na uzoefu wako wa maisha. Ila fikra na mawazo yako hayo yananielekeza kujua kiwango chako cha uelewa wa Taifa la Tanzania lilipotoka, lilipo na linapokwenda.

Nina ufahamu wa kutosha kuhusu taifa hili bila kujali umri wangu. Vinginevyo uniambie kujua ukweli wa nchi hii ni lazima uwe na umri fulani. Huenda tofauti yako yangu kwenye haya mambo ni nafasi tulizopo. Ww unatetemekea cheo wakati mimi ni mjasiriamali niliye huru.
 
Kama wewe mjasiriamali leo Rais, kupitia Mkuu wako wa Mkoa, anakupa kitambulisho ambacho hutasumbuliwa na mtu yeyote yule, ukatengeneze fedha uondokane na umaskini.

Hiyo ndiyo mikakati ya kuondokana na umaskini, ingawa si ya tija sana lakini ni mwanzo mzuri kuliko mabadiliko ya kuzungusha mikono.
 
Mimi ni mjasiriamali nisiyehitaji msaada wa rais. Huko kusaidiwa na serekali nimeshatoka siku nyingi ndugu. Halafu mimi sio mnyonge wala masikini. Pia sijawahi kuzungusha mikono maana sijawahi kumkubali Lowasaa wala sintomkubali. Na kwa uhakika sihitaji ajira yoyote iwe ya serekali au ya mtu binafsi maana niko vizuri. Uwezo wangu wa kimaisha ndio unanifanya nisiishi kwa kujinyenyekeza kwa watawala kama ww.
 
Leo nilipanga kutoa salaam hizi za Uhuru kuwa Uhuru ni Kazi Lakini pia Kazi na Bata. Hata hivyo nilikuwa nina shughuli ya kihistoria huko Bahari Beach Hotel kulinda Uhuru wa Kufanya Siasa kwa kupinga muswada kandamizi wa Vyama vya Siasa unaopendekezwa na Serikali ya CCM. Basi jioni hii msome huku mkifurahia Uhuru na Bata ( kama zipo, Ila zitakuwepo baada ya Oktoba 2020 ).

====

Kazi na Bata — Maana yake nini hasa?

Zitto Kabwe

KATIKA mitandao ya kijamii na vyombo rasmi vya habari mwezi huu, kauli mbiu ya #KaziNaBata imepata msukumo mkubwa na nimekuwa nikipata maswali mengi kuhusu msemo huu unaojipatia umaarufu kila uchao.

Nimeona kwamba ni muhimu kwangu kutoa ufafanuzi wa msemo huu ili kwamba usipotoshwe au kupewa maana nyingine na watu ambao kwa namna moja au nyingine #KaziNaBata inawakera.

Siku zote, katika mapambano ya wanyonge kujikwamua kutoka katika makucha ya mfumo wowote, kumekuwa pia na ndoto ya kutaka kufaidi matunda ya jasho, machozi na damu yanayotokea wakati huo wa mapambano.

Kwenye kujikwamua kutoka katika makucha ya mfumo kandamizi, kunaweza kumaanisha hali bora za kiuchumi, heshima, haki na mambo mengine yanayoendana na hayo. Lakini mwisho wa yote, wanadamu watabaki kuwa wanadamu na watataka kufaidi matunda ya jitihada zao hizo.

Ni dhana ndiyo hasa ilikuwa msingi mkuu wa kauli mbiu maarufu ya wapigania haki za wafanyakazi mashuhuri wa karne ya 19 waliokuwa wakipigania mambo makubwa matatu tu kila uchao; “Saa nane za kufanya kazi, saa nane za kulala na saa nane za kufanya tunachotaka.

Mwaka 1912, kundi la wanawake waliokuwa wakifanya kazi katika mji wa Lawrence Massachusetts, uliokuwa kitovu cha viwanda vya kutengeneza nguo waligoma kufanya kazi kwa kudai malipo bora zaidi.

Ujumbe mkubwa uliokuwa umetamalaki katika mabango yao waliyoyabeba wakati wakiandamana ulikuwa ukisomeka “ Mikate na Mauaridi”. Kwa watafsiri wa misemo, ujumbe huo ulimaanisha kwamba watu wanataka kipato cha kuwatosheleza kula vizuri lakini pia kufanya mambo waliyokuwa wakiyapenda; jambo lililowakilishwa ipasavyo na alama hiyo ya uaridi.

Katika tafakari yake mujarabu kuhusu mapambano ya kudai Uhuru barani Afrika katikati ya k=arne ya 20, mwanamapinduzi kutoka Martinique, Ufaransa, Franz Fannon, alisema kwamba: “Kwa watu wanaotawaliwa, jambo lao la kwanza muhimu kwao ni ardhi yao. Ardhi ni muhimu kwa sababu ndiyo itakayowapa chakula na kulinda utu wao.”

Kwa kiasi fulani, tafakuri hiyo jadidi ya Fannon iliungwa mkono na mwanamapinduzi mwenzake wa Guinea-Bissau, Amilcar Cabral, aliyeshajiisha kwamba: “ Watu hupambana ili kuboresha maisha yao. Kuishi vema na kwa amani. Kuona wanaishi kwa muda mrefu na kwa maisha yenye kutia matumaini kuliko waliyokuwa wanaishi chini ya wakandamizaji.

Hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, naye kuna nyakati alionyesha wazi hisi zake katika mtazamo huu kwa kauli mbiu zake maarufu kama Uhuru na Maendeleo ambazo zilikuwa zikitekelezwa kwa vitendo kama ilivyokuwa kwenye vijiji vya Ujamaa –mfano mzuri zaidi ukiwa vilivyokuwa chini ya Ruvuma Development Association.

Kwa bahati mbaya, matamanio haya ya chakula, mauaridi na utu huwa hayapatikani. Hata katika utaratibu ule wa vijiji vya Ujamaa vilivyoanzishwa na serikali, utaratibu wa awali wa watu kukaa na kujipangia maendeleo yao ulivurugwa kwa mtindo mpya wa kupokea maagizo kutoka ngazi za juu.

Tangu aingie madarakani mwaka 2015, Rais John Magufuli ameibuka na kauli mbiu yake ya HapaKaziTu. Dhana hii ilijengwa katika msingi wa kupambana na rushwa ambayo ni tatizo kubwa hapa nchini na kauli mbiu ilitaka kutengeneza vuguvugu la kusafisha tatizo hilo na kuboresha utendaji wa serikali.

Kampeni hii ya Magufuli ilipokewa kwa moyo mkunjufu na walio wengi katika siku za awali za utawala wake ingawa sasa hali imebadilika na msisimko ule uliokuwepo sasa umegeuka kuwa fadhaa.

Badala ya vuguvugu hilo lenye kuleta matumaini ambalo aliahidi wakati wa kampeni za 2015 na katika siku zake za awali za urais, sasa hali imekuwa ya hofu.

Shughuli za kisiasa zimepigwa marufuku, wanasiasa wa Kitanzania sasa wanapigwa risasi na wengine wanatiwa nguvuni pasipo sababu za maana –huku waandishi wa habari na wanaharakati wakitoweka kusikojulikana, wanafunzi wenye mimba wakikataliwa kuendelea na masomo pasipo kusahau kadhia ya wavuvi, wafugaji na wakulima wanaotwezwa kupitia operesheni mbalimbali za kiusalama zinazoendeshwa na serikali hii.

Kwa upande mwingine, uchumi wa Tanzania unaelekea kwenye mserero wa kuporomoka na wananchi hawa wanyonge alioahidi kuwatetea ndiyo sasa wamegeuka kuwa wahanga wa kwanza wa siasa za Rais Magufuli.

Wamegeuka wahanga kwa sababu ahadi zinazotolewa na serikali kuhusu kuboresha sekta ya afya na elimu imebaki midomoni na kwenye makaratasi tu kwa sababu fedha zinazotangazwa kuwa zimepelekwa huko hazifanyiwi hivyo kibajeti. Kwa maana nyingine, ndugu zangu Waswahili wangesema zilongwa mbali, zitendwa mbali.

Utawala wa Rais Magufuli umeleta hali ngumu kiuchumi kiasi kwamba sasa kuna msemo mpya umeingia katika msamiati wa Kiswahili wenye kujaribu kuelezea kinachoendelea; Vyuma Vimekaza.

Kwa sababu ya ugumu unaoonekana katika maisha ya kila siku ya Watanzania, ile dhana ya HapaKaziTu aliyokuja nayo Magufuli sasa inachukuliwa kama ni neno la amri la kutaka mtu atekeleze jambo hata kama hataki kufanya hivyo.

Badala ya kuamsha amri ya uzalendo na kufanya kitu kwa matamanio makubwa ya yajayo mbeleni, HapaKaziTu imegeuka kuwa shuruti.

Mwanadahamu haishi kwa ajili ya kufanya kazi tu. Kwamba afanye kazi pasipo kuwa huru au kuona maisha yake yakibadilika hata kwa mambo ya kuonekana tu.

Kwa bahati nzuri, lugha ya Kiswahili, lugha adhimu ya taifa letu, tayari ina msamiti unaoleza kuhusu matamanio ya watu wake –Watanzania. Msemo wenyewe unasema “Kazi na Dawa”, ikimaanisha kwamba mtu yeyote anayefanya kazi, anatakiwa pia kuwa na jambo la kumpunguzia machungu na kumzawadia kwa jambo kubwa alilolifanya. Jambo la kujipongeza katika namna inayokubalika kisheria.

Jambo hilo sasa ndilo vijana wa kisasa wanaliita bata. Wahenga wetu waliliona hili miaka mingi kabla sisi wengine hatujaiona nchi yetu na vijana wetu wa sasa wanaliona hilohilo lakini katika lugha yao, muktadha wao.

Ukweli ambao haupingiki ni mmoja tu na umebaki hivyo kwa miaka yote; kwamba watu wanahitaji kufanya kazi lakini wanahitaji pia chakula mezani, wanahitaji kupendwa, wanataka uhuru wao, kutimiza haja zao, kuwa na maisha mazuri na kuwa na uhakika wa maisha yao ya sasa na baadaye.

Huu ndiyo ubinadamu. Huo ndiyo Utanzania. Kazi na Dawa, Kazi na Bata.

Watu wanahitaji kufanya kazi. Watu wanahitaji kufurahia maisha.
hakuna kosa kubwa kwa kiongozi kuwa mjinga,duniani kote nchi zilizoendelea na wananchi wake wanaotusaidia hizo kodi ambazo ndio zinawafanya akina Zitto wavae suti ni kuchapa kazi,wenyewe hawapondi maisha kila kukicha ni kazi sasa kiongozi lofa unayetegemea kodi kwingine unataka eti ufanye kazi na kula bata,badala ya kuwekeza kwa ajili ya vizazi vijazo,kula bata na wajane sio
 
Back
Top Bottom