Salaam za Siku ya Wanawake Duniani 2019 kutoka Wizara ya Afya

Papaa Muu

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
243
500
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) inapenda kuwajulisha wadau wa maendeleo ya jinsia na wanawake pamoja na Watanzania kwa ujumla kuwa Tanzania itaungana na Nchi Nyingine Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa tarehe 8, Machi ya kila mwaka.

Kaulimbiu ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2019 inasema: “Badili Fikra Kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu”.

Kwa mwaka huu, Maadhimisho yataendelea kufanyika katika ngazi ya Mkoa ili kutoa wigo mpana kwa wanawake, wadau mbalimbali na kila Mtanzania kutathmini hatua tulizofikia kama Taifa katika masuala ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake na wasichana. Aidha, Maadhimisho haya ni fursa ya kujadiliana namna ya kukabiliana na changamoto katika kufikia Maendeleo jumuishi.
KAULI-MBIU-WANAWAKE-2019.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom