Salaam za ramadhan - ramadhan kareem | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salaam za ramadhan - ramadhan kareem

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ze burner, Aug 1, 2011.

 1. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  ASSALAAM ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATUH!

  ALLLAH S.W anasema katika kitabu chake kitukufu ya kwamba " kumbushaneni, hakika ya ukumbusho utamfaa mwenye kuamini."

  Wengi wetu tunasahau miongoni mwa fadhila zenye nguvu kabisa ambazo zitaongeza nguvu katika swaum zetu. hivyo ni vyema kukumbushana. Nitaeleza machache na ndugu wa kiislamu tusaidiane kuchangia ukumbusho huu.

  - SALAAM - kwa mwezi huu mtukufu pamoja na salaam ya kiislamu iliyozoeleka kuna salaam ya ziada ya kumtakia muislamu mwenzako ambayo ni kumwambia RAMADHAN KAREEM naye atajibu ALLAHU AKRAM.

  - MIALIKO - kumbuka kwamba kumualika muislamu mwenzako ni sunna ila kuitikia mwaliko pasipo na udhuru wowote ni faradhi (lazima) hivyo basi tupeane mialiko katika majumuiko ya kula futari na wala tusiache kuitika mialiko kwa hiyo ni ikharamu.

  - DAKU - ni vyema kama ambavyo mtume s.a.w ametuhimiza kuwahi kula futari na kuchelewesha daku.

  - kukithirisha ibada - kwani mwezi huu ni wa mavuno kwa waislamu. Hii ni pamoja na kusoma sana Qur-an.

  - Kuwajali masikini kwa kuwapatia angalau kiasi kwa ajili ya futari na daku.

  TUENDELEE KUKUMBUSHANA VITU VYA MSINGI NDUGU WAISLAMU.

  RAMADHAN MUBARAK WA BILLAHI TAWFIQ.
   
Loading...