mkafrend
JF-Expert Member
- May 12, 2014
- 3,047
- 1,503
Wakurugenzi wateule, Salaam!
Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Buyungu kupitia CCM na mshindi wa pili wa kura ya maoni Bw. Msakila Kabende - Afisa Takwimu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera leo akiongea na radio KWIZERA FM inayosikika katika kanda ya Ziwa ametoa salaam za pongezi kwa wateule wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kufuatia kuaminiwa na Mhe. Dkt. John P. Magufuli kushika nafasi hizo.
Aidha, amewaomba kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kusimamia rasilimali za umma kwa umakini wa hali ya juu ili wananchi wa Tanzania waweze kupata kwa haraka huduma za kijamii kama vile elimu, maji, umeme, afya, miundombinu n.k.
Katika mahojiano ya dakika takribani 45 hivi amewataka wakurugenzi hao kuhakikisha huduma wanazosimamia haziwabagui watu kwa ajili ya itikadi zao za kisiasa na kikanda ili kuhakikisha kila mwananchi anatoa mchango wa maendeleo katika taifa letu.
Akizungumzia kuhusu jinsi alivyouchukulia uteuzi wa magufuli alisema - "Mhe. Dkt. John Magufuli ni rais wa kuigwa katika karne hii - kuwa ni rais aliyehitajika katika nchi yetu". Aliongeza kuwa pamoja na changamoto zinazoikabili nchi yetu lakini ana matumaini makubwa kwamba kipindi cha uongozi wa rais huyu Tanzania itakuwa katika mstari munyoofu wa kiuadilifu na kiuchumi.
Akizungumzia hatua ya CHADEMA kuwa na mpango wa kwenda kuzuia mkutano wa CCM Dodoma alisema - "Tanzania ilijengwa na Mwl Nyerere katika misingi ya kuheshimiana - mtu mmoja kumheshimu mwenzake; kundi moja kuheshimiana na kundi jingine na chama kimoja kuheshimiana na vyama vingine" - Hivyo kuwataka CHADEMA kutofanya jaribio hili kwa kuwa watakuwa wanakiuka misingi husika na kwamba hata CCM haijawahi kuzuia mkutano wowote wa chama cha siasa hapa nchini"
Mwishoni, aliwatakia wateule wote wa awamu ya tano afya na mafanikio makubwa katika kazi zao.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!