Salaam za pole na rambirambi msiba wa Mpoki Bukuku kutoka CHADEMA

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,672
2,000
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mmoja wa waandishi wa habari (za picha) waandamizi nchini, Mpoki Bukuku kilichotokea kwa ajali ya gari akitokea kazini.

Kwa hakika tasnia ya habari imempoteza mmoja wa wapambanaji hodari ambaye hakusita kuitetea na kuilinda kamera yake hata mbele ya vitisho vya aina yoyote ile vilivyolenga kuminya uhuru wa habari.

Mpoki Bukuku ambaye hadi mauti yanamkuta alikuwa Mpiga Picha Mwandamizi wa Magazeti ya The Guardian Limited, ameondoka katika kipindi ambacho vyombo vya habari na uhuru wa habari kwa ujumla ambao yeye aliutetea kwa vitendo, ukipitia katika changamoto kubwa. Ujasiri na uthubutu wake ungehitajika sana katika nyakati hizi.

CHADEMA inaungana na tasnia nzima ya habari katika kumlilia Bukuku kwa majonzi makubwa. Tunatoa pole na salaam za rambirambi kwa familia yake, ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi wenzake wa The Guardian Ltd, wanahabari wenzake na wadau wa habari kwa ujumla nchini kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Mwenyezi Mungu awatie nguvu na kuwapatia moyo wa subira katika wakati huu mgumu wa kumlilia Mpoki.
 
Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,248
2,000
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SALAAM ZA POLE NA RAMBIRAMBI MSIBA WA MPOKI BUKUKU

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mmoja wa waandishi wa habari (za picha) waandamizi nchini, Mpoki Bukuku kilichotokea kwa ajali ya gari akitokea kazini.

Kwa hakika tasnia ya habari imempoteza mmoja wa wapambanaji hodari ambaye hakusita kuitetea na kuilinda kamera yake hata mbele ya vitisho vya aina yoyote ile vilivyolenga kuminya uhuru wa habari.

Mpoki Bukuku ambaye hadi mauti yanamkuta alikuwa Mpiga Picha Mwandamizi wa Magazeti ya The Guardian Limited, ameondoka katika kipindi ambacho vyombo vya habari na uhuru wa habari kwa ujumla ambao yeye aliutetea kwa vitendo, ukipitia katika changamoto kubwa. Ujasiri na uthubutu wake ungehitajika sana katika nyakati hizi.

CHADEMA inaungana na tasnia nzima ya habari katika kumlilia Bukuku kwa majonzi makubwa. Tunatoa pole na salaam za rambirambi kwa familia yake, ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi wenzake wa The Guardian Ltd, wanahabari wenzake na wadau wa habari kwa ujumla nchini kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Mwenyezi Mungu awatie nguvu na kuwapatia moyo wa subira katika wakati huu mgumu wa kumlilia Mpoki.

Tumaini Makene
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom