salaam za obama kwa JK hizi hapa. mwezi mmoja baada ya uchaguzi. akili ni nywele | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

salaam za obama kwa JK hizi hapa. mwezi mmoja baada ya uchaguzi. akili ni nywele

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kweleakwelea, Dec 7, 2010.

 1. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  salam za OB kwa JK kama alivyozipost michuzi. salamu hizi zilizotoka baada ya kimya kikuu kirefu zimetumia fasihi ya ajabu kufikisha ujumbe. zisome, tafakari chukua hatua.akili ni nywele kila Ntu ana zake. we unazielewaje?

  MICHUZI

  [​IMG]Rais wa Marekani,Barrack Obama


  Kwa niaba ya Marekani, Ninawapongeza watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukamilisha uchaguzi mkuu hivi karibuni na kuendeleza utamaduni wenu wa kuendesha chaguzi za vyama vingi toka mwaka 1992.

  Ninatarajia kufanya kazi na Rais Jakaya Kikwete na wabunge wa Bunge la Kumi tunapoendelea kujenga na kuimarisha ubia wa muda mrefu na wenye mafanikio kati ya mataifa yetu katika kuendeleza malengo ya pamoja ya maendeleo na kukabiliana na changamoto nyingi za kimataifa zinazotukabili.

  Aidha, ninatoa pongezi zangu za dhati kwa Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Seif Sharif Hamad, serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa na zaidi sana kwa watu wa Zanzibar ambao wameweka historia kwa kufanya uchaguzi wa amani baada ya miaka kadhaa ya chaguzi zilizogubikwa na machafuko.

  Kama nilivyomueleza Rais Kikwete nilipokutana naye katika Ikulu ya White House hapo mwaka 2009, Watu wa Marekani wanawaunga mkono Watanzania wote katika jitihada zenu za kuimarisha utawala wa kidemokrasia na uwazi, kutumia kikamilifu fursa za Muungano wenu na kuhakikisha kuwa hatua mlizopiga na mafanikio mliofikia katika kujenga amani na ustawi wa kudumu hayarudi nyuma.   
 2. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  The source. PUTS ME OFF. I doudt the unyele wa akili
   
 3. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  usichoke tuanzie kwenye red!

  Rais wa Marekani,Barrack Obama

  Kwa niaba ya Marekani, Ninawapongeza watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukamilisha uchaguzi mkuu hivi karibuni na kuendeleza utamaduni wenu wa kuendesha chaguzi za vyama vingi toka mwaka 1992.

  Ninatarajia kufanya kazi na Rais Jakaya Kikwete na wabunge wa Bunge la Kumi tunapoendelea kujenga na kuimarisha ubia wa muda mrefu na wenye mafanikio kati ya mataifa yetu katika kuendeleza malengo ya pamoja ya maendeleo na kukabiliana na changamoto nyingi za kimataifa zinazotukabili.

  Aidha,
  ninatoa pongezi zangu za dhati kwa Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Seif Sharif Hamad, serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa na zaidi sana kwa watu wa Zanzibar ambao wameweka historia kwa kufanya uchaguzi wa amani baada ya miaka kadhaa ya chaguzi zilizogubikwa na machafuko.

  Kama nilivyomueleza Rais Kikwete nilipokutana naye katika Ikulu ya White House hapo mwaka 2009, Watu wa Marekani wanawaunga mkono Watanzania wote katika jitihada zenu za
  kuimarisha utawala wa kidemokrasia na uwazi, kutumia kikamilifu fursa za Muungano wenu na kuhakikisha kuwa hatua mlizopiga na mafanikio mliofikia katika kujenga amani na ustawi wa kudumu hayarudi nyuma.
   
 4. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280

  Mbona hii ilitoka siku nyingi tu kwa kingereza. Unless siku zote hizi ilikuwa inakuwa translated kwa kiswahili. Au Michuzi hajui tofauti ya hii na ile ya Kingereza??
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135


  Ahsante Rais Obama, na sie twakuahidi kushirikiana nawe. Uchaguzi wetu umeisha kwa amani, huru na haki. Na tumepata Rais wetu ambae ni chaguo la watanzania na aliyeshinda kwa kishindo Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na ameifanyia mengi Tanzania yetu yenye kuleta ustawi na maisha bora kwa wananchi wake.
   
 6. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180

  kaazi kweli kweli haya tuanze...
  , Ninawapongeza watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - ni lazima kwani tumepiga kura
  kuendeleza utamaduni wenu wa kuendesha chaguzi za vyama vingi toka mwaka 1992. - kwani tunachagua chama kile kile hata kama hakina jipya, tunachakachua etc......hatuandamani na tunapenda amani na utulivu kuliko njaa.
  Ninatarajia kufanya kazi na Rais Jakaya Kikwete na wabunge wa Bunge la Kumi tunapoendelea kujenga na kuimarisha ubia wa muda mrefu na wenye mafanikio kati ya mataifa yetu katika kuendeleza malengo ya pamoja ya maendeleo na kukabiliana na changamoto nyingi za kimataifa zinazotukabili. - hana namna nyingine kwani mumemchagua wenyewe na maisha lazima yaendelee marekani hata tanzania. lakini huyu HAJAPONGEZWA KWA USHINDI


  Aidha,
  ninatoa pongezi zangu za dhati kwa Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais Seif Sharif Hamad, - HAWA WANASTAHILI PONGEZI KWA KUWEKA MBELE MASLAHI YA TAIFA

  Kama nilivyomueleza Rais Kikwete nilipokutana naye katika Ikulu ya White House hapo mwaka 2009, Watu wa Marekani wanawaunga mkono Watanzania wote katika jitihada zenu za kuimarisha utawala wa kidemokrasia na uwazi, kutumia kikamilifu fursa za Muungano wenu na kuhakikisha kuwa hatua mlizopiga na mafanikio mliofikia katika kujenga amani na ustawi wa kudumu hayarudi nyuma. - KUNA HAJA YA KUKUZA DEMOKRASIA NA IKIWEZEKANA WATATOA FUNGU LA KUANDIKA UPYA KATIBA?

  nani mungine ana pongezi toka ulaya? alete tuzijadili humu!
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kwetu hii post huitwa NDAZA.
  Nikimaanisha izo salamu zilikuwepo umu kitambo tuu labda heading ndio tofauti
   
 8. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0


  NImependa hapo kwenye red. Hivi nani ananufaika zaidi?????

  Ningependsa ijitokeze taasisi yenye utashi siku moja ifanye utafiti kubaini mnufaikaji zaidi wa ubia huu. Isje kuwa mambo ya kunipa jiti hadharani wakati unaniibia mamilioni na utashi wangu wa kufikiri na kujiamulia mambo yangu kisiri.
   
 9. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Mbona hajampongeza Mkwere kwa kuchaguliwa tena?? nafikiri CIA washamwambia Obama kuwa Mkwere kaiba kura ha ha ahaha safisana Obama kwa kumpongeza Dk.Shein na Maalim Seif na Kutompongeza Mkwere
   
 10. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  c.r.a.p
   
 11. m

  matawi JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkwere alipopata hii salamu nasikia alianguka bafuni ila hatukuambiwa. Tusubiri akialikwa chai na dogo tuone kama ataenda kunywa
   
Loading...