Salaam za Kiongozi wa ACT Wazalendo Ndg. Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto Juu ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika Alhamis, 9 Disemba 2021

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,879

Leo tarehe 9 Disemba, sehemu moja ya Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania, iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, inatimiza umri wa miaka 60 tangu Uhuru wake. Ni siku muhimu mno kwa Taifa letu, kwa sababu ya umuhimu wake huo nimeamua nami kuzungumza nanyi moja kwa moja kwa njia hii kutafakari nanyi masuala machache ninayotaka tuyajadili kwa pamoja kama Taifa katika siku hii muhimu kwa Wananchi wa Tanzania Bara na Watanzania kwa ujumla.

Sio mataifa yote yameendelea kuwa pamoja baada ya kupata uhuru wao kutoka kwa wakoloni. Zipo baadhi ya nchi ndani ya Afrika ziliparaganyika miaka michache tu baada ya uhuru. Zipo nchi ambazo leo hii, ni muunganiko tu wa makabila na hazina sifa ya kuitwa mataifa; zipo pia nchi ambazo, tangu zilipopata uhuru hazijawahi kuonja ladha ya amani japo kwa miaka miwili mfululizo. Aidha, zipo nchi ambazo mapinduzi na umwagaji damu vimekuwa moja ya alama zao.

Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutuepusha na madhila ya aina hiyo, na kwa kutupatia viongozi waasisi waliokuwa na maono na uzalendo wa hali ya juu. Nitumie fursa hii kuwashukuru wazee wetu hao kwa kutuwekea msingi imara wa Taifa letu.

Tunapoadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika, tunayo kila sababu ya kuwashukuru wananchi wote wa Tanzania. Kila mmoja kwa nafasi yake ametoa mchango katika kujenga Taifa letu. Kipekee kabisa, nilishukuru na kulipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwa kuendelea kuwa chombo imara na cha kutumainiwa katika ulinzi wa mipaka ya Taifa letu. JWTZ imeendelea kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kama ilivyokuwa dhamira ya kuanzishwa kwake.

Ndugu Wananchi
Kwa vyovyote vile, hii ni hatua kubwa sana na ni jambo la kujivunia kuwa sehemu ya wananchi wanaoshuhudia sehemu moja ya Taifa letu likiadhimisha miaka 60. Miaka 60 ni umri mkubwa kwa Taifa, huu ni umri wa mtu ambaye kwa mujibu wa Sheria zetu za utumishi wa umma, angetakiwa kuwa amestaafu, mzee mwenye busara zake, mwenye uzoefu, anayetenda kwa hekima, na anayerithisha watoto, wajukuu na jamii inayomzunguka yale mambo mema aliyoyapitia pamoja na kuwaonya wajiepushe na yale mabaya aliyoyapitia. Kwa hakika kuna mafanikio makubwa na ya kupigiwa mfano, vile vile kuna mafunzo mengi yanayotokana na yale ambayo hatujaweza kufanikisha. Ni lazima kujipongeza.

Pamoja na kujipongeza na kusherehekea miaka hii 60, kwa kujivunia mafanikio yetu kama Taifa, hatuna budi pia kuzitazama changamoto zetu mbalimbali. Wale tuliokuwa nao sawa Miaka ya 60 kama vile China, Vietnam, Korea na Malaysia Leo wapo mbali sana kimaendeleo. Kwa Mfano Nchi ya Vietnam, Mwaka 2003 tulikuwa nao Sawa kwa kipimo cha Wastani wa Pato la Mwananchi mmoja mmoja kwa USD 450, Leo Mwaka 2021 wametuzidi kwa takribani mara 3. Bado Uchumi wetu ni Duni sana na ni muhimu sana kwa TAIFA kujiuliza maswali magumu, KWANINI HATUPIGI HATUA KWA KASI KUBWA KAMA WENZETU.

Changamoto mbaya zaidi ni zile ambazo zipo ndani ya uwezo wetu, hasa zile zinazovunja umoja wetu wa Kitaifa. Kwa hakika hatuko wamoja, kuna manungúniko mengi, hasa ya kisiasa na hata kiuchumi. Tuna miaka 60 ya Uhuru lakini bado hatuna uhuru na ustaarabu wa kuchagua Viongozi wetu kwa haki; tukiitisha uchaguzi ni lazima tuuane; Tuna miaka 60 lakini hatuvumiliani kisiasa, tunashutumiana na hata kufungana, tunazuiana kufanya shughuli halali za kisiasa, tuna miaka 60 lakini bado tu masikini sana nk.

Ndugu Wananchi,
Hatuwezi kuendelea namna hii tukitaraji kuwa mambo yatabadilika yenyewe. Ni muhimu sana kufanya Tafakari ya Pamoja kama Taifa ili kujenga matumaini ya Taifa letu kutupeleka Miaka 60 ijayo. Nina ushauri.

Ninachokishauri si kipya, alikishauri mzee wetu, Rais wa Awamu ya Nne, ndugu Jakaya Kikwete wakati tulipoadhimisha miaka 50 ya Uhuru, kwamba ni furaha kuwa Taifa letu kutimiza miaka 50, lakini ni muhimu tujitafakari na kuja na njia mpya ya kwendea miaka 50 inayofuata, njia ya mzee Jakaya ilikuwa ni kuanzisha “Mchakato wa Katiba Mpya”. Tulitumia miaka mitatu kujadiliana kama Taifa juu ya Katiba yetu mpya iweje, ingawa mchakato ule hatukuumaliza lakini yapo mafunzo ambayo tumeyapitia kama Taifa, kwanza kwa kutoumaliza ule mchakato, na pili kwa kuuona umuhimu wa ule mchakato. Matokeo ya maono ya Watanzania kwa Miaka 50 inayokuja yaliwekwa katika Rasimu ya Katiba na hatimaye kwenye Katiba pendekezwa. Sio kila mtu aliyapenda yote yaliyokuwamo katika nyaraka hizi. Hilo haliwezekani kwani wakati wowote ule Nchi yetu angalau 40% ya Watu wake hupingana na 60% ya Watu wengine. Muhimu ni kupata mwafaka kwa kutilia umuhimu yale tunayokubaliana. Hatukupata muafaka wakati ule. Tukapita kwenye kipindi kigumu ambacho kinapaswa kuwa funzo kubwa ili tusirejee huko. Ni lazima turidhiane. Ni lazima tujenge Taifa ambalo kila Mwananchi anashiriki katika masuala ya Nchi bila ubaguzi. Ni lazima tutazame yepi yanatuunganisha tuyashike na yepi tuna mitazamo tofauti tujadili kwa lengo la kupata suluhisho. Kama upande wa Zanzibar wameweza kukaa na kuendesha Serikali kwa Pamoja kwanini ishindikane Tanzania Bara?

Ndugu Wananchi,
Nashauri kama Taifa tufanye mambo manne yafuatayo ili kurudisha umoja wetu kama Taifa:

1. Tufanye Mazungumzo ya Viongozi wa Vyama vya siasa ili kutafakari na kurekebisha makosa makubwa ya 2019 na 2020.
2. Kwamba Kiongozi mwenzetu wa Kisiasa, ndugu Freeman Mbowe aliyepo jela makosa yake ni ya kisiasa na suluhisho lake lazima liwe la kisiasa sio la kijinai. Nazisihi Mamlaka zinazohusika na Mashtaka kuwa ndugu Mbowe aachiwe Huru ili tuwe naye kwenye mazungumzo kati ya Rais na Vyama vya siasa mnamo tarehe 16 - 17 disemba 2021.
3. Mazungumzo ya Vyama vya Siasa yajikite kwenye kuangalia namna nzuri ya kuandika upya Sheria ya Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya siasa. Vile vile Sheria mbalimbali kandamizi zitazamwe upya na kurejewa.
4. Mwaka 2022 tunatimiza Miaka 30 tangu Nchi yetu irejee kwenye Mfumo wa vyama vingi vya Siasa. Ni muhimu sasa kuanza majadiliano na mazungumzo rasmi kitaifa kuhusu namna ya kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya.

Ndugu Wananchi,
Binafsi ningetamani miaka 60 ijayo, Taifa letu liendelee kuwa moja, lenye ushawishi kwenye ukanda huu na duniani kwa ujumla. Taifa lenye wananchi wanaojitambua, wenye maarifa, wasio masikini na wanaopendana. Bila Kuwa wamoja sasa hatutaweza kukaa pamoja na kujenga hilo ninalotamani kurithisha kwa vizazi vinavyokuja. Lakini ili kuwa wamoja ni lazima kuimarisha mifumo ya Haki ili kudumisha Amani. Tusiogope kujadiliana.

Ninawatakia tafakari njema, tunapoanza safari ya miaka 60 ijayo.

Asanteni sana kunisikiliza
 
Wachana na makala ndefu, chama chako kiko tayari kuungana na wenzio pale wanapokuwa na jambo lao hasa kupinga uvunjifu wa sheria unaofanywa na CCM kwa kushirikiana na dola?

Zanzibar tuliona na baadhi ya majimbo huku bara yaliyorudia uchaguzi, mlienda kushiriki chaguzi zile licha ya kasoro nyingi zilizojitokeza kwenye uchaguzi mkuu uliopita 2020.

Mfano Mbagala, mlishiriki lakini mkaambulia vipigo kwa mawakala wenu mkaanza kulia, kwa kushiriki kwenu hamuoni mnarudisha nyuma harakati za wenzenu kudai haki sawa na sheria za uchaguzi zifuatwe?

Naandika hivyo kwasababu nimeanza kuona chama chako kuwa sehemu ya serikali (Zanzibar) umeanza kuwa na tabia ya kun'gata na kupuliza, na mfano wa hilo ni moja ya kauli zako ya hivi karibuni kuwa hautakuwa unapinga kwenye awamu hii ya Samia kama ulivyokuwa ukifanya wakati wa Magufuli, haya mambo yanakufanya usieleweke.

Pia, leo unadai Mbowe aachiwe huru ni kesi ya kisiasa, lakini uliwahi kunukuliwa twitter ukionesha kwamba ulipanga na Mbowe kufanya vurugu, hapa tukuelewe vipi? wewe ni mwanasiasa wa aina gani?
 
Wachana na makala ndefu, chama chako kiko tayari kuungana na wenzio pale wanapokuwa na jambo lao hasa kupinga uvunjifu wa sheria unaofanywa na CCM kwa kushirikiana na dola?

Zanzibar tuliona na baadhi ya majimbo huku bara yaliyorudia uchaguzi, mlienda kushiriki chaguzi zile licha ya kasoro nyingi zilizojitokeza kwenye uchaguzi mkuu uliopita 2020, mfano Mbagala, mlishiriki lakini mkaambulia vipigo kwa mawakala wenu, kwa kushiriki kwenu hamuoni mnarudisha nyuma harakati za wenzenu kudai haki sawa na sheria za uchaguzi zifuatwe?

Naandika hivyo kwasababu nimeanza kuona chama chako kuwa sehemu ya serikali (Zanzibar) umeanza kuwa na tabia ya kun'gata na kupuliza, na mfano wa hilo ni moja ya kau kauli zako hivi karibuni kuwa hutakuwa unapinga kwenye awamu hii ya Samia kama ulivyokuwa ukifanya wakati wa Magufuli.
Mwenzenu yuko mahabusu kwa kesi za kinumba bado nyie mna hangaika kumualika rais kwenye kikao badala ya kuungana wote kama wapinzani kupinga wanayo tendea wapinzani. Kwani rais haoni mnayo taka kwenda kumuambia? Kwani rais haoni ushahida wa uongo unao tolewa na mapolisi wake? Kwani rais haoni Ccm wakifanya mikutano nchi nzima tena ya hadhara na kulindwa na polisi wakati wapinzani wakifanya kikao cha ndani wana kamatwa?
Hebu Zityo sahauni kuongea na Mh rais kwenye huo mkutano maana she is a part and parcel ya haya yanayo tendeka hapa nchini. Ata kuja kuwachora tuu. Taki it from me..
 
Sometimes huwa napata shida kuona logic ya kukaa mezani na watu wanaotumia vibaya madaraka kushauriananao juu ya jambo ambalo wao wamelisabisha kwa kutumia vibaya madaraka na kesi ya Mbowe ni mfano mzuri.

Huwa naona ni sawa na kutaka majadilioni na mwizi uliemkuta na mali yako. Akuibie kisha umuombe mjadiliane namna ya kukurudishia mali yako!

Anyway, siasa zina mambo ya hovyo sana tena ambayo hayana logic kabisa, ila kwasababu mambo hayo yanahusisha decision makers wa nchi, ndio maana yanaonekana kuwa na umuhimu ila baadhi
ya mambo huwa ni uzandiki na upuuzi mtupu.
 
Leo tarehe 9 Disemba, sehemu moja ya Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania, iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, inatimiza umri wa miaka 60 tangu Uhuru wake. Ni siku muhimu mno kwa Taifa letu, kwa sababu ya umuhimu wake huo nimeamua nami kuzungumza nanyi moja kwa moja kwa njia hii kutafakari nanyi masuala machache ninayotaka tuyajadili kwa pamoja kama Taifa katika siku hii muhimu kwa Wananchi wa Tanzania Bara na Watanzania kwa ujumla.

Sio mataifa yote yameendelea kuwa pamoja baada ya kupata uhuru wao kutoka kwa wakoloni. Zipo baadhi ya nchi ndani ya Afrika ziliparaganyika miaka michache tu baada ya uhuru. Zipo nchi ambazo leo hii, ni muunganiko tu wa makabila na hazina sifa ya kuitwa mataifa; zipo pia nchi ambazo, tangu zilipopata uhuru hazijawahi kuonja ladha ya amani japo kwa miaka miwili mfululizo. Aidha, zipo nchi ambazo mapinduzi na umwagaji damu vimekuwa moja ya alama zao.

Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutuepusha na madhila ya aina hiyo, na kwa kutupatia viongozi waasisi waliokuwa na maono na uzalendo wa hali ya juu. Nitumie fursa hii kuwashukuru wazee wetu hao kwa kutuwekea msingi imara wa Taifa letu.

Tunapoadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika, tunayo kila sababu ya kuwashukuru wananchi wote wa Tanzania. Kila mmoja kwa nafasi yake ametoa mchango katika kujenga Taifa letu. Kipekee kabisa, nilishukuru na kulipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwa kuendelea kuwa chombo imara na cha kutumainiwa katika ulinzi wa mipaka ya Taifa letu. JWTZ imeendelea kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kama ilivyokuwa dhamira ya kuanzishwa kwake.

Ndugu Wananchi
Kwa vyovyote vile, hii ni hatua kubwa sana na ni jambo la kujivunia kuwa sehemu ya wananchi wanaoshuhudia sehemu moja ya Taifa letu likiadhimisha miaka 60. Miaka 60 ni umri mkubwa kwa Taifa, huu ni umri wa mtu ambaye kwa mujibu wa Sheria zetu za utumishi wa umma, angetakiwa kuwa amestaafu, mzee mwenye busara zake, mwenye uzoefu, anayetenda kwa hekima, na anayerithisha watoto, wajukuu na jamii inayomzunguka yale mambo mema aliyoyapitia pamoja na kuwaonya wajiepushe na yale mabaya aliyoyapitia. Kwa hakika kuna mafanikio makubwa na ya kupigiwa mfano, vile vile kuna mafunzo mengi yanayotokana na yale ambayo hatujaweza kufanikisha. Ni lazima kujipongeza.

Pamoja na kujipongeza na kusherehekea miaka hii 60, kwa kujivunia mafanikio yetu kama Taifa, hatuna budi pia kuzitazama changamoto zetu mbalimbali. Wale tuliokuwa nao sawa Miaka ya 60 kama vile China, Vietnam, Korea na Malaysia Leo wapo mbali sana kimaendeleo. Kwa Mfano Nchi ya Vietnam, Mwaka 2003 tulikuwa nao Sawa kwa kipimo cha Wastani wa Pato la Mwananchi mmoja mmoja kwa USD 450, Leo Mwaka 2021 wametuzidi kwa takribani mara 3. Bado Uchumi wetu ni Duni sana na ni muhimu sana kwa TAIFA kujiuliza maswali magumu, KWANINI HATUPIGI HATUA KWA KASI KUBWA KAMA WENZETU.

Changamoto mbaya zaidi ni zile ambazo zipo ndani ya uwezo wetu, hasa zile zinazovunja umoja wetu wa Kitaifa. Kwa hakika hatuko wamoja, kuna manungúniko mengi, hasa ya kisiasa na hata kiuchumi. Tuna miaka 60 ya Uhuru lakini bado hatuna uhuru na ustaarabu wa kuchagua Viongozi wetu kwa haki; tukiitisha uchaguzi ni lazima tuuane; Tuna miaka 60 lakini hatuvumiliani kisiasa, tunashutumiana na hata kufungana, tunazuiana kufanya shughuli halali za kisiasa, tuna miaka 60 lakini bado tu masikini sana nk.

Ndugu Wananchi,
Hatuwezi kuendelea namna hii tukitaraji kuwa mambo yatabadilika yenyewe. Ni muhimu sana kufanya Tafakari ya Pamoja kama Taifa ili kujenga matumaini ya Taifa letu kutupeleka Miaka 60 ijayo. Nina ushauri.

Ninachokishauri si kipya, alikishauri mzee wetu, Rais wa Awamu ya Nne, ndugu Jakaya Kikwete wakati tulipoadhimisha miaka 50 ya Uhuru, kwamba ni furaha kuwa Taifa letu kutimiza miaka 50, lakini ni muhimu tujitafakari na kuja na njia mpya ya kwendea miaka 50 inayofuata, njia ya mzee Jakaya ilikuwa ni kuanzisha “Mchakato wa Katiba Mpya”. Tulitumia miaka mitatu kujadiliana kama Taifa juu ya Katiba yetu mpya iweje, ingawa mchakato ule hatukuumaliza lakini yapo mafunzo ambayo tumeyapitia kama Taifa, kwanza kwa kutoumaliza ule mchakato, na pili kwa kuuona umuhimu wa ule mchakato. Matokeo ya maono ya Watanzania kwa Miaka 50 inayokuja yaliwekwa katika Rasimu ya Katiba na hatimaye kwenye Katiba pendekezwa. Sio kila mtu aliyapenda yote yaliyokuwamo katika nyaraka hizi. Hilo haliwezekani kwani wakati wowote ule Nchi yetu angalau 40% ya Watu wake hupingana na 60% ya Watu wengine. Muhimu ni kupata mwafaka kwa kutilia umuhimu yale tunayokubaliana. Hatukupata muafaka wakati ule. Tukapita kwenye kipindi kigumu ambacho kinapaswa kuwa funzo kubwa ili tusirejee huko. Ni lazima turidhiane. Ni lazima tujenge Taifa ambalo kila Mwananchi anashiriki katika masuala ya Nchi bila ubaguzi. Ni lazima tutazame yepi yanatuunganisha tuyashike na yepi tuna mitazamo tofauti tujadili kwa lengo la kupata suluhisho. Kama upande wa Zanzibar wameweza kukaa na kuendesha Serikali kwa Pamoja kwanini ishindikane Tanzania Bara?

Ndugu Wananchi,
Nashauri kama Taifa tufanye mambo manne yafuatayo ili kurudisha umoja wetu kama Taifa:

1. Tufanye Mazungumzo ya Viongozi wa Vyama vya siasa ili kutafakari na kurekebisha makosa makubwa ya 2019 na 2020.
2. Kwamba Kiongozi mwenzetu wa Kisiasa, ndugu Freeman Mbowe aliyepo jela makosa yake ni ya kisiasa na suluhisho lake lazima liwe la kisiasa sio la kijinai. Nazisihi Mamlaka zinazohusika na Mashtaka kuwa ndugu Mbowe aachiwe Huru ili tuwe naye kwenye mazungumzo kati ya Rais na Vyama vya siasa mnamo tarehe 16 - 17 disemba 2021.
3. Mazungumzo ya Vyama vya Siasa yajikite kwenye kuangalia namna nzuri ya kuandika upya Sheria ya Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya siasa. Vile vile Sheria mbalimbali kandamizi zitazamwe upya na kurejewa.
4. Mwaka 2022 tunatimiza Miaka 30 tangu Nchi yetu irejee kwenye Mfumo wa vyama vingi vya Siasa. Ni muhimu sasa kuanza majadiliano na mazungumzo rasmi kitaifa kuhusu namna ya kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya.

Ndugu Wananchi,
Binafsi ningetamani miaka 60 ijayo, Taifa letu liendelee kuwa moja, lenye ushawishi kwenye ukanda huu na duniani kwa ujumla. Taifa lenye wananchi wanaojitambua, wenye maarifa, wasio masikini na wanaopendana. Bila Kuwa wamoja sasa hatutaweza kukaa pamoja na kujenga hilo ninalotamani kurithisha kwa vizazi vinavyokuja. Lakini ili kuwa wamoja ni lazima kuimarisha mifumo ya Haki ili kudumisha Amani. Tusiogope kujadiliana.

Ninawatakia tafakari njema, tunapoanza safari ya miaka 60 ijayo.

Asanteni sana kunisikiliza
Salute Sana Mkuu Yuda
Wewe ni Kichwa sana, sema tu unatembeaga na Price tag yako hadharani
 
Maoni mazuri ya kizalendo angalau unaonekana serikali mbadala kuliko wale chagadema wao Kila siku wanawaza ujinga tupu hongera zitto
 
Salute Sana Mkuu Yuda
Wewe ni Kichwa sana, sema tu unatembeaga na Price tag yako hadharani
Kwa comment kama hii, mwanasiasa kama huna ngozi ngumu, siasa zitakushinda, na kama una madaraka makubwa, basi utaishia kufunga watu jela au kuua watu kama sio kupoteza watu.
 
Kwa comment kama hii, Mwanasiasa kama huna ngozi ngumu, siasa zitakushinda, na kama una madaraka makubwa, basi utaishia kuua ama kupoteza watu.
Mkuu, Yuda ni Hazina Sana, na Yuko njema Sana upstairs
Sema ananunulika Kirahisi Sana, hata uanzishwaji wa Chama chake ulikuwa Mpango wa Kudhoofisha Upinzani baada ya watu Kumpa dau
 
Anyway, kila ntu ana haki ya kujieleza ila kusikilizwa ni hiari ya anayesikia. Siku wana siasa wakiacha usanii na kutuchezea akili labda.
 
Mkuu, Yuda ni Hazina Sana, na Yuko njema Sana upstairs
Sema ananunulika Kirahisi Sana, hata uanzishwaji wa Chama chake ulikuwa Mpango wa Kudhoofisha Upinzani baada ya watu Kumpa dau
Kwakweli siku hizi kapoteza kabisa mvuto na ushawishi wa kisiasa aliokuwa nao.

CCM inaharibu sana majina na future za kisiasa za wanasiasa wengi mfano Zitto, Halima Mdee na wengineo wengi.
 
Kwakweli siku hizi kapoteza kabisa mvuto na ushawishi wa kisiasa aliokuwa nao.

CCM inaharibu sana majina na future za wanasiasa wengine kama kina Zitto,Halima Mdee na wengineo wengi.
Mwendakuzimu alimpotezea Yuda ndio Maana alikuwa anamkosoa Sana, Kimsingi alikuwa ana wish Kununuliwa, sasa hivi Kaanza Kujipendekeza Kwa Mama
 
Mkuu, Yuda ni Hazina Sana, na Yuko njema Sana upstairs
Sema ananunulika Kirahisi Sana, hata uanzishwaji wa Chama chake ulikuwa Mpango wa Kudhoofisha Upinzani baada ya watu Kumpa dau
Unaweza kuleta ushahidi?
 
Leo tarehe 9 Disemba, sehemu moja ya Jamhuri yetu ya Muungano wa Tanzania, iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika, inatimiza umri wa miaka 60 tangu Uhuru wake. Ni siku muhimu mno kwa Taifa letu, kwa sababu ya umuhimu wake huo nimeamua nami kuzungumza nanyi moja kwa moja kwa njia hii kutafakari nanyi masuala machache ninayotaka tuyajadili kwa pamoja kama Taifa katika siku hii muhimu kwa Wananchi wa Tanzania Bara na Watanzania kwa ujumla.

Sio mataifa yote yameendelea kuwa pamoja baada ya kupata uhuru wao kutoka kwa wakoloni. Zipo baadhi ya nchi ndani ya Afrika ziliparaganyika miaka michache tu baada ya uhuru. Zipo nchi ambazo leo hii, ni muunganiko tu wa makabila na hazina sifa ya kuitwa mataifa; zipo pia nchi ambazo, tangu zilipopata uhuru hazijawahi kuonja ladha ya amani japo kwa miaka miwili mfululizo. Aidha, zipo nchi ambazo mapinduzi na umwagaji damu vimekuwa moja ya alama zao.

Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutuepusha na madhila ya aina hiyo, na kwa kutupatia viongozi waasisi waliokuwa na maono na uzalendo wa hali ya juu. Nitumie fursa hii kuwashukuru wazee wetu hao kwa kutuwekea msingi imara wa Taifa letu.

Tunapoadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika, tunayo kila sababu ya kuwashukuru wananchi wote wa Tanzania. Kila mmoja kwa nafasi yake ametoa mchango katika kujenga Taifa letu. Kipekee kabisa, nilishukuru na kulipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kwa kuendelea kuwa chombo imara na cha kutumainiwa katika ulinzi wa mipaka ya Taifa letu. JWTZ imeendelea kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kama ilivyokuwa dhamira ya kuanzishwa kwake.

Ndugu Wananchi
Kwa vyovyote vile, hii ni hatua kubwa sana na ni jambo la kujivunia kuwa sehemu ya wananchi wanaoshuhudia sehemu moja ya Taifa letu likiadhimisha miaka 60. Miaka 60 ni umri mkubwa kwa Taifa, huu ni umri wa mtu ambaye kwa mujibu wa Sheria zetu za utumishi wa umma, angetakiwa kuwa amestaafu, mzee mwenye busara zake, mwenye uzoefu, anayetenda kwa hekima, na anayerithisha watoto, wajukuu na jamii inayomzunguka yale mambo mema aliyoyapitia pamoja na kuwaonya wajiepushe na yale mabaya aliyoyapitia. Kwa hakika kuna mafanikio makubwa na ya kupigiwa mfano, vile vile kuna mafunzo mengi yanayotokana na yale ambayo hatujaweza kufanikisha. Ni lazima kujipongeza.

Pamoja na kujipongeza na kusherehekea miaka hii 60, kwa kujivunia mafanikio yetu kama Taifa, hatuna budi pia kuzitazama changamoto zetu mbalimbali. Wale tuliokuwa nao sawa Miaka ya 60 kama vile China, Vietnam, Korea na Malaysia Leo wapo mbali sana kimaendeleo. Kwa Mfano Nchi ya Vietnam, Mwaka 2003 tulikuwa nao Sawa kwa kipimo cha Wastani wa Pato la Mwananchi mmoja mmoja kwa USD 450, Leo Mwaka 2021 wametuzidi kwa takribani mara 3. Bado Uchumi wetu ni Duni sana na ni muhimu sana kwa TAIFA kujiuliza maswali magumu, KWANINI HATUPIGI HATUA KWA KASI KUBWA KAMA WENZETU.

Changamoto mbaya zaidi ni zile ambazo zipo ndani ya uwezo wetu, hasa zile zinazovunja umoja wetu wa Kitaifa. Kwa hakika hatuko wamoja, kuna manungúniko mengi, hasa ya kisiasa na hata kiuchumi. Tuna miaka 60 ya Uhuru lakini bado hatuna uhuru na ustaarabu wa kuchagua Viongozi wetu kwa haki; tukiitisha uchaguzi ni lazima tuuane; Tuna miaka 60 lakini hatuvumiliani kisiasa, tunashutumiana na hata kufungana, tunazuiana kufanya shughuli halali za kisiasa, tuna miaka 60 lakini bado tu masikini sana nk.

Ndugu Wananchi,
Hatuwezi kuendelea namna hii tukitaraji kuwa mambo yatabadilika yenyewe. Ni muhimu sana kufanya Tafakari ya Pamoja kama Taifa ili kujenga matumaini ya Taifa letu kutupeleka Miaka 60 ijayo. Nina ushauri.

Ninachokishauri si kipya, alikishauri mzee wetu, Rais wa Awamu ya Nne, ndugu Jakaya Kikwete wakati tulipoadhimisha miaka 50 ya Uhuru, kwamba ni furaha kuwa Taifa letu kutimiza miaka 50, lakini ni muhimu tujitafakari na kuja na njia mpya ya kwendea miaka 50 inayofuata, njia ya mzee Jakaya ilikuwa ni kuanzisha “Mchakato wa Katiba Mpya”. Tulitumia miaka mitatu kujadiliana kama Taifa juu ya Katiba yetu mpya iweje, ingawa mchakato ule hatukuumaliza lakini yapo mafunzo ambayo tumeyapitia kama Taifa, kwanza kwa kutoumaliza ule mchakato, na pili kwa kuuona umuhimu wa ule mchakato. Matokeo ya maono ya Watanzania kwa Miaka 50 inayokuja yaliwekwa katika Rasimu ya Katiba na hatimaye kwenye Katiba pendekezwa. Sio kila mtu aliyapenda yote yaliyokuwamo katika nyaraka hizi. Hilo haliwezekani kwani wakati wowote ule Nchi yetu angalau 40% ya Watu wake hupingana na 60% ya Watu wengine. Muhimu ni kupata mwafaka kwa kutilia umuhimu yale tunayokubaliana. Hatukupata muafaka wakati ule. Tukapita kwenye kipindi kigumu ambacho kinapaswa kuwa funzo kubwa ili tusirejee huko. Ni lazima turidhiane. Ni lazima tujenge Taifa ambalo kila Mwananchi anashiriki katika masuala ya Nchi bila ubaguzi. Ni lazima tutazame yepi yanatuunganisha tuyashike na yepi tuna mitazamo tofauti tujadili kwa lengo la kupata suluhisho. Kama upande wa Zanzibar wameweza kukaa na kuendesha Serikali kwa Pamoja kwanini ishindikane Tanzania Bara?

Ndugu Wananchi,
Nashauri kama Taifa tufanye mambo manne yafuatayo ili kurudisha umoja wetu kama Taifa:

1. Tufanye Mazungumzo ya Viongozi wa Vyama vya siasa ili kutafakari na kurekebisha makosa makubwa ya 2019 na 2020.
2. Kwamba Kiongozi mwenzetu wa Kisiasa, ndugu Freeman Mbowe aliyepo jela makosa yake ni ya kisiasa na suluhisho lake lazima liwe la kisiasa sio la kijinai. Nazisihi Mamlaka zinazohusika na Mashtaka kuwa ndugu Mbowe aachiwe Huru ili tuwe naye kwenye mazungumzo kati ya Rais na Vyama vya siasa mnamo tarehe 16 - 17 disemba 2021.
3. Mazungumzo ya Vyama vya Siasa yajikite kwenye kuangalia namna nzuri ya kuandika upya Sheria ya Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya siasa. Vile vile Sheria mbalimbali kandamizi zitazamwe upya na kurejewa.
4. Mwaka 2022 tunatimiza Miaka 30 tangu Nchi yetu irejee kwenye Mfumo wa vyama vingi vya Siasa. Ni muhimu sasa kuanza majadiliano na mazungumzo rasmi kitaifa kuhusu namna ya kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya.

Ndugu Wananchi,
Binafsi ningetamani miaka 60 ijayo, Taifa letu liendelee kuwa moja, lenye ushawishi kwenye ukanda huu na duniani kwa ujumla. Taifa lenye wananchi wanaojitambua, wenye maarifa, wasio masikini na wanaopendana. Bila Kuwa wamoja sasa hatutaweza kukaa pamoja na kujenga hilo ninalotamani kurithisha kwa vizazi vinavyokuja. Lakini ili kuwa wamoja ni lazima kuimarisha mifumo ya Haki ili kudumisha Amani. Tusiogope kujadiliana.

Ninawatakia tafakari njema, tunapoanza safari ya miaka 60 ijayo.

Asanteni sana kunisikiliza

Zitto bana!

Introduction ya nguvu lakini conclusion dhaifu. Hata hivyo sishangai sana maana wanasiasa wote kwao kila tatizo solution lake ni "mwafaka wa kisiasa" wa viongozi. Kwamba leo hii Vietnam wapo vizuri kiuchumi kutuliko sisi solution yake = mwafaka wa kisiasa. Kwamba leo hii bado kuna watanzania maskini solution yake = Mbowe aachiwe huru.

Anyway....
 
Umepotosha kwamba JWTZ limeendelea kuwa jeshi la wananchi. Ukweli ni kinyume chake jeshi limekuwa kibaraka wa CCM na watawala. Kama tunataka kweli miaka 60 tuwe huko unakukusema. Lazima tuuseme ukweli wote bila chuki, haya Wala huba.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom