Uchaguzi 2020 Salaam kwa Watanzania wote Kupitia JamiiForums - Tunaomba kura zenu za Ndio mumpe Tundu Lissu

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,942
3,819
Wanajamiiforums, fikisheni salamu hizi kwa kila Mtanzania mpiga kura bila ya kujali itikadi ya chama chake kwani kama ni CCM huenda akaiona haki na yeye akatamani kutenda haki. Haki ambayo inahubiriwa na Tundu Lissu ,ya kuwa Mashehe wote wakiislamu walioko magerezani bila ya hatia yeyote anahakikisha anawaachia huru, mara moja.

Ni neema ilioje kwa ambae si Muislamu kutoa kauli hiyo hadharani jambo ambalo Mashehe kanzu na vilemba wa BAKWATA wameshindwa hata angalau kuwataja, Kwa Muislamu na mpenda amani bora Lisu kuliko hawa mashehe ubwabwa wa Bakwata wanatutia aibu waislamu.

Kura za Ndio kwa Mtakatifu Tundu Lissu.

Wajulishe na waTanzania wapenda amani ujumbe huu kupitia JF unawafikia na kuamshana CCM itakakoelekea inanjinjiwa huko huko mara hii haelekei mtu kibla... kichinjio changu nimekificha ila kila siku nakitazama kama kipo, maana Chakubanga na Abushiri ni wachawi.
 
Japo umetumia neno Mtakatifu sijui kwanini.

Familia yangu imejipanga vilivyo kuelekeza kura zao kwa Tundu Antipas Lissu. Hawatakaa wasahau sebuleni yetu ilijawa na simanzi na vilio siku ya Trh 07/09/2017 jioni tuliporudi nyumbani tukiwa tunajulishana masaibu yaliyompata Lissu...Kila mmoja aligeukia upande wake akifuta machozi kwa ukatili aliofanyiwa Lissu. Kwa nini avamiwe na kupigwa risasi kwenye eneo lenye ulinzi mkali, amewakosea nini? Maswali ni mengi ila Mungu ni Mkubwa kumzuilia na Mauti.

Tutampa kura zetu !!
 
Kura ni siri ya Mtu hazipigwi na Familia, Zinapigwa na Mtu mmoja mmoja. Kura yangu nitampa JPM, Wengine katika familia yangu nawaomba waangalie nani wanayemtaka wampe kura, japo nitafurahi wakimpa JPM Huyu ndio mbeba maono ya nchi.
 
Kura ni siri ya Mtu hazipigwi na Familia, Zinapigwa na Mtu mmoja mmoja. Kura yangu nitampa JPM, Wengine katika familia yangu nawaomba waangalie nani wanamtaka wampe kura, japo nitafurahi wakimpa JPM Huyu ndio mbeba maono ya nchi.
Wewe ni mtumishi wa umma?
 
Nitampigia kura Tundu Lissu, Ninashawishi ndugu zangu wampigie kura Tundu Lissu. Ninampigia kampeni Lissu kwa nguvu zangu zote na nitahakikisha anapata ushindi wa kishindo mwaka huu.

Kwa maslahi mapana ya Tanzania na vizazi vyetu vijavyo , tuna kila sababu ya kumchagua Tundu Lissu kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania mwaka huu! Kama unajali maendeleo yako na future ya watoto wako na uzao wako una kila sababu ya kumpigia kura Tundu Antiphas Lissu mwaka huu!
 
Bado unahitajika ushawishi wa nguvu wa mtu kwa mtu na kuzidi kuuelezea ukweli kuwa CCM imeshachoka ahadi zao za ajabu ajabu ni zile zile,wanapita kuwahadaa wananchi.

Maendeleo mapya kwa WaTanzania yatapatikana kwa kuwepo kwa Chama kipya katika uongozi,Watanzania kwa ujumla wao wakikatae chama Tawala na waamue kuweka Chama kiongozi.

Viongozi wa CCM sasa wanakaribia kusujudiana waangalieni kwa vizuri mtaona ni kwa jinsi gani viongozi wa CCM na wanataka na wananchi nao wawasujudie.

Shime wananchi kwa umoja wetu UTAWALA wa CCM lazima upigwe na chini kiuhalali kabisa tuweke chama kiongozi.

Huu ni mwanzo mwema kwa WaTanzania kuacha kuburutwa na vyama vya siasa,kila chama kitakachoingia kuongoza ,viongozi wake ni lazima wawe na adabu na heshima,

Heshimu ili uheshimiwe ,CCM imewavunjia heshima Waislamu walio wengi mpaka sasa ndugu zetu wa Kikiristo waziwazi wanawatetea ndugu zao katika uraia.

Nimeona ni muujiza kabisa Mgombea wa dini ya Kikiirsto anasimama wazi wazi akiwatetea Mashehe na sio sehemu moja kila anapopita, hawasahau.

Huyu ni kiongozi ambae WaTanzania wameletewa na mwenyezi Mungu,wanatakiwa wasibabaike kabisa na ahadi zisizokwisha za CCM.
CCM basi imetosha miaka 54 ni wakati wa kustaafu,chama kongwe limechakaa akili za CCM kama chama haziwezi kuendesha tena nchi ni kuvuruga na kulinda wababe ..kulindana....

hakuna ulazima si kwenye katiba ya nchi wala ya CCM kuwa lazima Raisi atimize miyaka kumi,wananchi na tetesi nchi zima zinasema sasa CCM imetosha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom