Salaam kwa mh. James Mbatia kutoka majimbo ya NCCR Mageuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Salaam kwa mh. James Mbatia kutoka majimbo ya NCCR Mageuzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rugumye, Apr 5, 2011.

 1. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MHESHIMIWA JAMES MBATIA WANANCHI TUMECHOKA KUONA UNAKUWA MKEREKETWA WA CHAMA CHA MAPINDUZI.
  Mheshimiwa mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia sisi wananchi wa Mkoa wa Kigoma unatukatisha tamaa, Kumbuka wananchi wa mkoa wa Kigoma ni wanamapinduzi wa kweli. Ni miongoni mwa mikoa ya kwanza kuamini vyama vya upinzani tangu mfumo wa vyama vingi ulipoingia hapa nchini, kumbuka Dr Walid Kabour na Mheshimiwa Zito waliaminiwa miaka mingi. Pia katika uchaguzi wa mwaka jana karibu majimbo yote ya mkoa wa Kigoma yachukuliwe na vyama vya upinzani. Kati ya majimbo 8 ya mkoa huu majimbo 5 yalichukuliwa na vyama vya CHADEMA na NCCR mageuzi. Majimbo 3 yaliyobaki ambayo ni Kigoma Mjini, Kasulu mashariki na Kibondo ndiyo pekee yalichukuliwa na CCM. Hata hivyo katika majimbo hayo 3 mawili yalichakachuliwa hasa la Kigoma Mjini kwa mheshimiwa Peter Serukamba, kule Kasulu Mashariki CCM ilishinda kwa kura 1.
  Mhesimiwa Mbatia tunasikitika sana kuona ukiungana na Chama cha wananchi CUF Prof Limbumba, kufunga ndoa na Chama cha Mapinduzi (CCM) chama ambacho sisi wana Kigoma tumekiweka pembeni kikajifunze. Tunashindwa kuelewa kuwa umetudharau watu wa Kigoma au umenunuliwa na CCM. Tunapenda kutoa onyo kwako kuwa kitendo unachofanya hakitufurahishi watu wa Kigoma hata kidogo. Kumbuka chama cha NCCR mageuzi kimepata ushindi katika majimbo mkoani kigoma tu, hivyo unahitajika kutoa shukrani kwa kuonyesha kuwa wewe ni mpinzani wa kweli. Kitendo cha kuungana na CUF kukitetea chama cha mapinduzi kinatukera sana. Kumbuka ruzuku inayopata NCCR Mageuzi inatokana na ushindi wa chama hicho mkoani Kigoma, tunapenda ruzuku hiyo itumike kuongeza upinzani na si kudhoofisha upinzani. Kumbuka NCCR Mageuzi hukukijenga wewe mkoani Kigoma, haya ni matunda ya Mhemiwa Daniel Nsanzugwanko na wengine. Mheshimiwa Nsanzugwanko inasadikika kushinda mwaka 1995 lakini akachakachuliwa baada ya hapo akajisalimisha CCM. Lakini kwa bahati nzuri wananchi walikuwa wameshachoka na CCM wakabaki na msimamo uleule wa upinzani. Mheshimiwa Mbatia ni kwa bahati tu Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA hakijajiuza kwa wananchi katika wilaya za Kasulu na Kibondo usingeweza kupata majimbo haya.
  Tunakuomba uache mara moja kuungana na CUF kukitetea chama cha CCM kwa pesa za ruzuku kupitia majimbo yetu. Tungeferahi kisikia kuwa NCCR mageuzi kuungana na CUF kuipinga CCM . kama hutasikia maoni yetu uchaguzi ujao usijindanganye kupata ushindi tena. Lakini pia Tunampongeza Mh. Dr NsengÂ’ondo Mvungi kwa kuonyesha kutokuwa mkereketwa wa CCM. Tunaaamini utauchukua ujumbe huu kwa uzito stahili na kijirekebisha. Aksante.
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Poleni Wabunge wa NCCR Mageuzi kwani mitazamo yenu na ya mwenyekiti wenu ni sawa na ncha mbili za sumaku. Mwambieni bora awe anakaa kimya kuliko kukimbilia kwenye media kutoa matamko yanayombomoa yeye na chama chake
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Huyu mbatia kafanyaje tena hebu tupeni habari kamili bana..
   
 4. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mawazo yake kuhusu KATIBA MPYA tofauti na wapinzani wote
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mbatia is a frustrated man kuanzia familia, biashara na hata ana inner personal conflict na jinsi alivyo... ana masumbuko makubwa sana. Unaweza kuthibitisha kwa kuangali nguvu anayotumia kuexpress kitu huku macho na paji la uso likimshataki moja kwa moja

  Ila nashangaa sana NCCR yenye vichwa vizuri kama Mvungi wanamuachaje yule bwana awaaibishe kila wakati??

  It is high time akina kafulila ku-step in na kumwambia huyo sh**a akae kimya anawaaibisha
   
 6. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbatia anazunguka mikoani akitukana vyama vya upinzani km chadema na kuisifia CCM. alikuwa kigoma, Zanzibar na nk. siyo mpinzani wa kweli.
   
 7. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  huyu mbatia ni ccm aliye upinzani huyu
   
 8. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  At first naanza kujua siasa na mfuatiliaji wa siasa i waz real impressed and motivated with Mbatia, ilifika wakati nikawa najiita Mbatia mdogo but as Days goes on nasikitika kuona jinsi anavyojenga hoja zake, ule uwezo wake wa kujenga hoja umepotelea wapi tena?mashiko aliyokuwa nayo yameenda wapi?kwanini hajiamnini kusimama mwenyewe mpk aungane na CUF wakati hapo awali alikuwa na uwezo wa kuitisha mikutano pekee yake na tilkuwa tunajaa na kumsikiliza lakini leo akizungumza watu wanahudhuria wachache kweli kweli.

  Kama kweli ni mwanasiasa mwenye mashiko na uchungu wa maoinduzi ya kweli lazima arudi nyuma na kutafakari kwanini hali hii sasa?lazima ajiulize inakuaje M/Kiti wa Chama ngazi ya taifa unagombea ubunge uankosa je unaweza kuendelea kuongoza taifa?kama wachache hawakutaki iwaje ujiite M/Kiti wa taifa?
   
 9. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  yeye na lipumba wamelipwa kuishambulia CDM,mimi siwahofii kabisa sababu hawana impact yoyote kwenye siasa za leo,..ili wasikike inabidi waitaje cdm kila wanapoongea,..nina uhakika,watz wote wana uhakika na hata lipumba na mbatia wana uhakika hakuna mmoja wao anaweza kutokea kuwa rais wa nchi hii,..never..sababu hawana jipya wamechuja,.bora hata lipumba alikuwa na kamvuto kidogo zamani kuliko huyo mbatia,.lipumba anaogopa hata kugombea ubunge maana anaweza kukosa
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,655
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Mbatia na CUF wameamua kuingia ubia kusamabaratisha upinzani nchini. Kweli masikini hana kiapo, nikikumbuka jinsi Mbatia alivyoihujumu CUF kwa kuwawekea pingamizi wagombea wa CUF kule visiwani hadi ukaasisiwa msamiati wa kura za maruhani,leo hii CUF hiyo hiyo inamnadi Mbatia huko visiwani kuwa ni mpiganaji mwenzao ni jambo la kusikitisha.
   
 11. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio anaweza kukosa, bali atakosa
   
Loading...