SALAAM kutoka jikoni

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
1,488
908
Ndugu Watanzania, wana JF.. na wapenzi wazalendo woote wa nchi yangu.. sitakuwepo jamvini kwa kitambo kidogo, ila napenda threads yangu Isomeke.. CCM haiko tayari kuona nchi inachukuliwa na Upinzani kwa vyovyote Vile, hilo mlielewe. Katika Vikao Vyote vya ndani, CCM imejizatiti kuhakikisha Liwalo na Liwe lakini haitawezekana wala haipo akilini kwao kwamba kitakuwa chama cha upinzani.

Sisi tuliomo humu tumetumiwa sana kuwaneemesha "wazee", na wanasema waziwazi CCM haijaanza kuua watu Jana. Hivyo hakuna cha kushangaa.. watu watauawa kwa maslahi ya Nchi.

Katikati ya wiki lililopita Kulikuwa na Kikao kikubwa cha Viongozi waandamizi na wale wakongwe waliokuwa hazina ya CCM. Kikao Hicho mahsusi kilihusika na kujadili hasa matamshi ya viongozi wastaafu kushiriki kutoa matamko makali kwa serikali hivyo kukidhoofisha chama. Baadhi ya wazee wa "siku" kwenye kikao Hicho wakadai kwamba kama CCM ikiondolewa basi na wao maisha yao yatakuwa magumu kwa sababu watoto wao na wajukuu zao wameshamiliki maeneo muhimu ya Majiji na Miji na ndio warithi wa Tanzania kisiasa na kiuchumi.

Kikao Hicho kikapendekeza kwamba kwa kuwa kuna wazee bado wana heshimika kwenye jamii ya watanzania basi wajitokeze kwenye vyombo vya habari na kutoa matamshi makali juu ya vyama vya Upinzani vyenye upinzani makini hasa Chadema kwa upande wa bara na Cuf kwa upande wa visiwani, na moja kwa moja chama kitasponsor kadhia hiyo..

Kikao Hicho ambacho wajumbe hawakuruhusiwa kabisa kuingia na kitu chochote kama notebook, laptop au mobile.. wengine tulipenyapenya na Iphone na kubahatika kurekodi sehemu ya mazungumzo.. na ilikuwa nia yangu kumwaga mchuzi mezani kwa kuweka Audio strings JF ya sehemu ya mazungumzo hayo, ili kila kitu kiwe open.

Bahati mbaya wakati wa kutoka kukawa na sachsach na wajumbe wanne wakakutwa waliingia na cm. baada ya kuhojiwa na vijana wa Usalama.. walirejeshewa cm zao. Hvyo nikiweka strings ya Audio ntawachongea wale jamaa. Huku ndani, wana CCM wengi hawakipendi Chama, wengi wamo tu kwa sababu wanaogopa wakitoka watauawa.. wanasena No way you can Go out of CCM safely .. kama Kuna gereza la Kutisha.. CCM ni zaidi ya gereza..

Hata Huyo Nape.. CCM haipendi kabisa ila amewekwa kama spika ya wazee. na hela wanampa kweli kweli ndo maana ni kama kachanganyikiwa vile.. muda mwingi anautumia kwa kulewa chakari.. nadhani anapoteza mawazo.. kama kuna mtu wa kumwokoa ni Nape.. hana raha kabisaa.. hata ukikutana naye mwangalie usoni..

Ana huzuni sana huyo mkaka.. ni kama anajuta that time lipopata nafasi ya kujiondoa CCM kwa nini hakujiondoa.. sasa hawezi tena, anatumwa kama mtoto, anafanya kila anachoambia afanye.. inamuuma sana..

Mungu Ibariki Tanzania
 
mimi namhurumia mdogo wangu nape alipokuwa kabnisani alikuwa mwimbaji mzuri sana wa injili alipoasi kanisa ndo akaanza kula bakora za mungu.
ila sitaacha kumwombea kwa sababu najua mungu ni wahuruma na siku moja atamhurumia huyu kijana na kumtoa kwenye makucha ya huyu adui wa umma.
 
Hii ni zaidi ya habari ya yule kada wa chadema, mwakyembe na mengineyo yanadhihirisha kabisa uliyoandika.Kwa nguvu hizo wanazotumia kupambana na upinzani si rahisi kutekeleza hata robo ya yale waliyowaahidi wananchi.Sasa naanza kuelewa ni kwa nini yule mgonjwa wa akili wamtera alisema atajiua ccm ikikosa ubunge Igunga.
 
Tunashukuru kwa taariarifa, tunakutakia mapumziko mema lakini siku utakaporudi tena humu jamvini usisahau kutujuza angalau kwa uchache majina ya wana magamba waliokuwa kwenye huo mkutano, na nini hasa kilichojiri wakati wa mkutano huo, na kama kweli wewe ni mpambanaji basi usihofu kutuwekea hiyo Audio ili wana JF tujiridhishe na kile ulichokisema. Karibu tena jamvini.
 
mimi namhurumia mdogo wangu nape alipokuwa kabnisani alikuwa mwimbaji mzuri sana wa injili alipoasi kanisa ndo akaanza kula bakora za mungu.
ila sitaacha kumwombea kwa sababu najua mungu ni wahuruma na siku moja atamhurumia huyu kijana na kumtoa kwenye makucha ya huyu adui wa umma.
Nape anatumika mkuu kama chambo,wanamtanguza huku nyuma wanamtafuna.
 
Salma2015 Umeongea mengi ya msingi... ila tu hapo hakuna geni... kama unavo sema kua uliweza ingia pale.... Hii post ingekua na zaidi na infor ambayo maybe ni productive.... otherwise...
 
salma 2015 nawasiwasi umekosa mgao umeamua kumwaga mboga, kila la kheri kama utarudi salama
 
mnh maama mbona mependa ulivomwaga mboga...................hebu nkatafute ugali kwa kada mwingine,ahsante
 
Hizi habari ni za kweli na nimefurahi mtiririko wake..Tumwombee Nape bado ana nafasi ya kujirudi na kuwa Kijana mwenye mwelekeo
 
asante kwa taarifa mkuu.mimi mwenyewe ccm nshaichoka.hapanilipo nasubili wa kulianzisha.vinginevyo ccm itatawala milele,haiwezi kuachia nchi kwa njia ya makalatasi.dawa ya muuaji ni kumuua na dawa ya moto ni moto.pickup ipo tayari.samahani mkuu,hivi wewe ndo yule wa jikoni nape anayemuogopa?mia
 
Ndugu Watanzania, wana JF.. na wapenzi wazalendo woote wa nchi yangu.. sitakuwepo jamvini kwa kitambo kidogo, ila napenda threads yangu Isomeke.. CCM haiko tayari kuona nchi inachukuliwa na Upinzani kwa vyovyote Vile, hilo mlielewe. Katika Vikao Vyote vya ndani, CCM imejizatiti kuhakikisha Liwalo na Liwe lakini haitawezekana wala haipo akilini kwao kwamba kitakuwa chama cha upinzani.

Sisi tuliomo humu tumetumiwa sana kuwaneemesha "wazee", na wanasema waziwazi CCM haijaanza kuua watu Jana. Hivyo hakuna cha kushangaa.. watu watauawa kwa maslahi ya Nchi.

Katikati ya wiki lililopita Kulikuwa na Kikao kikubwa cha Viongozi waandamizi na wale wakongwe waliokuwa hazina ya CCM. Kikao Hicho mahsusi kilihusika na kujadili hasa matamshi ya viongozi wastaafu kushiriki kutoa matamko makali kwa serikali hivyo kukidhoofisha chama. Baadhi ya wazee wa "siku" kwenye kikao Hicho wakadai kwamba kama CCM ikiondolewa basi na wao maisha yao yatakuwa magumu kwa sababu watoto wao na wajukuu zao wameshamiliki maeneo muhimu ya Majiji na Miji na ndio warithi wa Tanzania kisiasa na kiuchumi.

Kikao Hicho kikapendekeza kwamba kwa kuwa kuna wazee bado wana heshimika kwenye jamii ya watanzania basi wajitokeze kwenye vyombo vya habari na kutoa matamshi makali juu ya vyama vya Upinzani vyenye upinzani makini hasa Chadema kwa upande wa bara na Cuf kwa upande wa visiwani, na moja kwa moja chama kitasponsor kadhia hiyo..

Kikao Hicho ambacho wajumbe hawakuruhusiwa kabisa kuingia na kitu chochote kama notebook, laptop au mobile.. wengine tulipenyapenya na Iphone na kubahatika kurekodi sehemu ya mazungumzo.. na ilikuwa nia yangu kumwaga mchuzi mezani kwa kuweka Audio strings JF ya sehemu ya mazungumzo hayo, ili kila kitu kiwe open.

Bahati mbaya wakati wa kutoka kukawa na sachsach na wajumbe wanne wakakutwa waliingia na cm. baada ya kuhojiwa na vijana wa Usalama.. walirejeshewa cm zao. Hvyo nikiweka strings ya Audio ntawachongea wale jamaa. Huku ndani, wana CCM wengi hawakipendi Chama, wengi wamo tu kwa sababu wanaogopa wakitoka watauawa.. wanasena No way you can Go out of CCM safely .. kama Kuna gereza la Kutisha.. CCM ni zaidi ya gereza..

Hata Huyo Nape.. CCM haipendi kabisa ila amewekwa kama spika ya wazee. na hela wanampa kweli kweli ndo maana ni kama kachanganyikiwa vile.. muda mwingi anautumia kwa kulewa chakari.. nadhani anapoteza mawazo.. kama kuna mtu wa kumwokoa ni Nape.. hana raha kabisaa.. hata ukikutana naye mwangalie usoni..

Ana huzuni sana huyo mkaka.. ni kama anajuta that time lipopata nafasi ya kujiondoa CCM kwa nini hakujiondoa.. sasa hawezi tena, anatumwa kama mtoto, anafanya kila anachoambia afanye.. inamuuma sana..

Mungu Ibariki Tanzania

ngoja niendelee kunusa kwanza nisije nikakubali haraka nikazodolewa nimekurupuka.

kitu kimoja najua tu ni kuwa vitu za jikoni huwa ni za ukweli.
 
Kwa taarifa yako Tanzania iliumbwa na Mungu na kuwapa Watanzania nchi nzuri. Kwa hiyo natamka leo tarehe 12 Oktoba 2011 yeyote anayedhani hawataondoka madarakani anaota mchana kweupe. KWA JINA KUU LA BWANA YESU WATAONDOKA MADARAKANI TU hata watafute msaada wa majini yote kuzimu watashindwa tu. Nawasilisha
 
Bahati mbaya wakati wa kutoka kukawa na sachsach na wajumbe wanne wakakutwa waliingia na cm. baada ya kuhojiwa na vijana wa Usalama.. walirejeshewa cm zao. Hvyo nikiweka strings ya Audio ntawachongea wale jamaa.
Mungu Ibariki Tanzania

Umefanya vizuri, usije ukawachongea wenzako; lakini je ungewataja kwa majina napo wangesema ni wale waliokutwa na simu ndio walioyataja? Napatwa na wasiwasi kidogo kuhusu ukweli wa taarifa hii
 
Asante sana kwa taarifa mkuu,da lakn c ungetuwekea sauti mkuu tusikie yaliyojiri zaidi?
 
Mh naona sasa inakuwa kama Mafia Mob hao Usalama wa Taifa kumbe ndio kazi yao kuilinda magamba?ipo siku watang'oka tu watake na wasitake alama za nyakati zipo ukutani ,hakuna marefu yasiyo na nchi,nani alikuwa kama Mubraka,saa yuko wapi
 
Back
Top Bottom