Habari wana jf, nimekua nikifaidi ya baraza hili nikia kwa nje muda mrefu, sasa nimeamua niingie ndani kwani utamu wa ngoma si kuangalia wengine bali kuingia nakucheza. MASHAKABWA
karibu tena ingia, si kwa tabu ni raha tu Ulizozoweya, ni kwa irabu na konsonanti ndo tutaongeya, si ndimi au fimbo za kuchapiya, utamuwe si wa kuhisabiya na hamuye hitokwishiya, karibu kaka, karibu mdogo, karibu muungwana, karibu na hapo ndo pa kuanziya, we ingiya ,ingiya, uwe mmoja wa kondooo! ingiya uweze jioneya, ingiya uje tusaidiya, ingiya uje kuchangiya.
Asanteni wenyeji wangu first lady 1, Dreamliner ,Bwanashamba,Edgartz na mswahilian mtaaluma wa kiswahili kwa shairi dogo nimejihisi mwenyeji tayari siku njema kwenu
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.