Sala yangu kwa Mungu kwa ajili ya Nchi yangu Tanzania

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,158
2,000
Sala yangu kwa Nchi yangu Tanzania :

Mungu wa mbingu usiyeshindwa na kitu tunaomba mkono wako wa baraka utushukie utupe busara viongozi wetu watuongoze kwa hekima yako,wewe uliyesimamia Taifa la Israeli na kuwavusha katika bahari naomba utuvushe nasi katika kipindi hiki ambacho yamekuwa yakitokea mambo mengi ambayo yanaweza kufanya tusiwe na amani pia tukiwa tunaelekea katika uchaguzi Yesu sikia usituache tukakosa amani utuokoe,
Mungu simama wewe maana twajua kuwa kwa akili zetu hatutaweza,tunaomba akili na maarifa na kutambua viongozi wenye busara tunaomba kwa kupitia jina la mwanao Yesu mpendwa tukiamini kuwa utakuwa kiongozi maana umesema katika Yeremia 33:3 NIite nami nitaitika nitakuonyesha mambo makubwa magumu usioyajua,Zab:23

Amen.

Nawakaribisha wakuu nanyi muiombee Nchi yetu.
 
pleo

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
2,903
2,000
Samweli alikuwa na kazi ya kusali, Sauli ya kutumia upanga; kwakuwa sala imeshatangulia sasa ni wakati wa Sauli.
 
pleo

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
2,903
2,000
Pleo Tutakosa hata amani ya kupost thread humu

Yehova Shalom,

amani ya BWANA ikutangulie, ufunikwe na mbawa za masafira panapo gharika, BWANA na akutumie malaika wa kukuvusha panapo tufani.

Tuuzunguke mji huu mara ngapi ufisadi uanguke?
 
Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,158
2,000
Yehova Shalom,

amani ya BWANA ikutangulie, ufunikwe na mbawa za masafira panapo gharika, BWANA na akutumie malaika wa kukuvusha panapo tufani.

Tuuzunguke mji huu mara ngapi ufisadi uanguke?
Mi naona tuombe Mungu atuongoze wakati tunachagua viongozi
tuweze kuchagua wenye hekima
 
Chikaka Sumuni

JF-Expert Member
May 16, 2013
1,337
0
Sala yangu kwa Nchi yangu Tanzania :

Mungu wa mbingu usiyeshindwa na kitu tunaomba mkono wako wa baraka utushukie utupe busara viongozi wetu watuongoze kwa hekima yako,wewe uliyesimamia Taifa la Israeli na kuwavusha katika bahari naomba utuvushe nasi katika kipindi hiki ambacho yamekuwa yakitokea mambo mengi ambayo yanaweza kufanya tusiwe na amani pia tukiwa tunaelekea katika uchaguzi Yesu sikia usituache tukakosa amani utuokoe,
Mungu simama wewe maana twajua kuwa kwa akili zetu hatutaweza,tunaomba akili na maarifa na kutambua viongozi wenye busara tunaomba kwa kupitia jina la mwanao Yesu mpendwa tukiamini kuwa utakuwa kiongozi maana umesema katika Yeremia 33:3 NIite nami nitaitika nitakuonyesha mambo makubwa magumu usioyajua,Zab:23

Amen.

Nawakaribisha wakuu nanyi muiombee Nchi yetu.

Ni kweli usemacho, Nakuomba usome pia MKitabu cha Waamuzi sura ya 3:7-11, Kimsingi unaweza kusoma sura yoyote ya Kitabu cha Waamuzi utakuta mammbo yafuatayo

1. Wana wa Israel walitenda dhambi
2. Mungu aliwaacha
3. Mungu aliwaweka chini ya adui yao ili awaadhibu kisawasawa
4. Yule adui aliwaadhibu sawasawa
5. Walilia sana kutokana na adhabu kali waliyopewa
6. Katika kulia kwao wakamlilia mungu wao yaani wakaanza kujitambua na kutubu dhambi zao
7. Ndipo Mungu kwa kuona kilio cha na toba yao ni ya kweli ndipo alipowainulia Mwamuzi (Kiongozi) mwingine aliyewaondoa kwenye mateso yao.

Lakini pale waliporudia mafanikio na neema yao, walijisahau na kurudia kutenda dhambi tena na Mungu aliwaacha na mzunguko ukaendelea kama kawaida.

Kwa hili linaloendela laweza kuwa na tafasiri ya Kiroho pia, maandiko matakatifu yanayo majibu ya kila kitu katika maisha yetu ya kila siku....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom