Sala ya siku 3, je kama nchi tuna nini? Tunaomba huku hakuna juhudi za kupambana na corona? Wenzetu wanasali au wanawekeza kwenye afya?

SALA
Tunaposimama mbele za Mungu, tunapaswa kuwa na imani thabiti. Imani kuhusu utendaji wa Mungu na Neema zake.

Mwenyezi Mungu ametuumba kwa upekee sana. Ametupa AKILI na UTASHI, ili tuwe tofauti na wanyama. Neno linasema Tuenende kwa AKILI, kwamba kutumia AKILI sio dhambi.

Mwenyezi Mungu anatumia AKILI alizotupa kuonesha uweza wake na nguvu zake. Kwamba, anatenda kazi zake kupitia sisi viumbe wake. Ni kama anavyotumia UZAZI kuendeleza kazi yake ya UUMBAJI ndio maana tunakemea utoaji mimba.

Sasa tunaingia magotini....

Je, tunaingia magotini kwa kuwa tuna HOFU?
Je, ni kwa kuwa ni 'maagizo' kwamba tusali?
Je, ni kumshirikisha Mungu wakati tunatumia AKILI alizotujalia ili atende kazi?
Je, tunasali kwa kuwa hatutaki tena kuwajibika?
Je, tunatumia sala kama njia ya kuficha uzembe?

Kila mmoja anajua kwa nini aingie magotini.

LAKINI

Nikumbushe, Yesu alisali, na ALITIMIZA WAJIBU.
Aliwapa watu chakula, japokuwa angeweza kutowapa chakula na kuwapulizia nguvu ya Roho Mtakatifu wawe wameshiba. Yesu ALIJIFICHA walipotaka kumpiga mawe... Hakujiachia hapo na kusema MUNGU ANAWEZA..

Wana wa Israeli walipewa mana, na walipaswa KUTOKA NJE ya nyumba zao kwenda kuzichukua...Hawakuketi kusubiri mana zijilete ndani ya nyumba zao. Ndio kusema, walipaswa waoneshe jitihada kupokea msaada wa Mungu.

Sisi WATANZANIA TUNAFANYA NINI?

Pamoja na kuliweka taifa katika maombi ambayo HAYAPASWI KUWA YA SIKU 3, bali maombi ya daima, tunatakiwa kuonesha juhudi katika kukabiliana na tatizo lililopo.

Kila siku unapotoka nyumbani kwako kuingia mtaani, jua kwamba unahatarisha maisha ya wengine. Jua kwamba unamweka muhudumu wa afya katika hatari ya kupoteza maisha.

Tujikumbushe haya kila tupigapo hatua huko mtaani: LEO NAKWENDA KUWAPELEKA WATU KADHAA KARANTINI. LEO NAKWENDA KUJIONGEZEA NAFASI YA KUWEKWA KARANTINI...

SERIKALI.

Pamoja na kuitia jina la BWANA, tujue kwamba juhudi zinahitajika. Kuhakikisha watu wanapata mask, huduma ya maji kwa bei nafuu, na WAHUDUMU wetu wapewe vifaa. Watu wapimwe, na taarifa zitoke.

Huwaambii watu wasali huku hata chai hawawezi kuimudu, au hawawezi kumudu kununua mask na vitakasa...

SALA na JUHUDI, SALA na AKILI, SALA na UKWELI.

Bibi Happy J
MAOMBI MAALUM YA SIKU TATU YA KITAIFA
KWA AJILI YA UGONJWA WA COVID-19
SIKU YA KWANZA (17.4.2020)
Utangulizi
“Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili tusiangamizwe?” (Yon.3:6-10).
Habari ya Ugonjwa wa COVID-19 imemfikia Rais John Pombe Magufuli. Amepiga mbiu kwa Watanzania wote, kama alivyofanya mfalme wa Ninawi. Wito mkuu wa maombi haya ni TOBA na KUMLILIA Mungu kwa ajili ya KUIPONYA Nchi yetu ili TUSIANGAMIZWE. Kwa hiyo, tuombee mambo yafuatayo:
SHUKURANI
1. Mshukuru Mungu kwa ajili ya Rais kuona haja ya maombi ya kitaifa.Soma kwa sauti Zaburi yote ya 33.
2. Mshukuru Mungu kwa ajili ya kupata nafasi ya kufanya maombi haya.
3. Mshukuru Mungu kwa ulinzi wa Nchi yetu hadi sasa.
TOBA
1. Tubu kwa ajili ya dunia iliyopota na kumuacha Mungu(Zab.53). Soma kwa sauti Zaburi yote ya 51 kwa niaba ya dunia nzima.
2. Tubu kwa ajili ya kutokusikiliza mausia ya Neno la Mungu linalohubiriwa kila siku. Soma kwa sauti Daniel sura ya 9 yote.
3. Omboleza kwa ajili ya yanayotupata sisi kama wanadamu. Soma kwa sauti Maombolezo sura yote ya 5.
4. Muombe Mungu kwa damu ya Agano Jipya ya Yesu Kristo akumbuke rehema zake kwa watu wake(Hab.3:2)
MAOMBI
1. Omba Mungu akumbuke maombi ya Raisi wetu na kuiponya Nchi yetu na uharibifu wowote kiafya, kiulinzi na kiuchumi (Isa. 38:6).
2. Ombea uponyaji kwa wagonjwa wa COVID-19(Mt.8:17).
3. Kataa nguvu za kaburi na roho ya mauti juu yao. Soma kwa sauti Hosea.13:14 na 1Kor.15:55-57.
4. Omba ulinzi kwa wasiougua na omba kwamba ugonjwa usiendelee kusambaa kwa watu wengine. Soma kwa sauti Zaburi yote ya 91.
5. Futa maneno yaliyosemwa na watu kuwa Afrika itashuhudia maiti zikizagaa mitaani kwa sababu ya COVID-19. Tuma malaika mharibu akaue maneno hayo katika ulimwengu wa roho (Isa.54:16, 17).
6. Ombea ulinzi wa Damu ya Yesu juu ya watalaam wa afya. Pia Mungu awape hekima na upendo wa kuwahudumia wagonjwa(Isa. 11:2,3)
MWISHO
1. Mshukuru Mungu kwa kukupa nafasi ya kuungana na watakatifu wengine duniani kufanya maombi haya maalum.
2. Muombe Mungu ashughulike na mahitaji yako binafsi. Atakabali sadaka yako hii ya maombi(Zab.20:1-4)
AMINA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati yao waliowekeza kwenye afya ni nani aliyefanikiwa kuishinda korona?.
mimi naona bora magufuli aliyeweka matumaini yake kwa MUNGU.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Binafsi yangu MAGUFULI YUPO SAHIHI KATIKA HILI..
mimi naamini sana katika MUNGU muweza wa yote.
Wala sina wasiwasi TUTASHINDA tukimtegemea yeye..
Magufuli ameonesha kuwaamini viongozi wa dini . naamini hawatamuangusha.
TUSEME TU UKWELI SAYANSI KWA SASA IMESHINDWA

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Zero brain peke yao ndio wanaweza kuamini katika maombi while hawajachukua hatua yoyote.
SALA
Tunaposimama mbele za Mungu, tunapaswa kuwa na imani thabiti. Imani kuhusu utendaji wa Mungu na Neema zake.

Mwenyezi Mungu ametuumba kwa upekee sana. Ametupa AKILI na UTASHI, ili tuwe tofauti na wanyama. Neno linasema Tuenende kwa AKILI, kwamba kutumia AKILI sio dhambi.

Mwenyezi Mungu anatumia AKILI alizotupa kuonesha uweza wake na nguvu zake. Kwamba, anatenda kazi zake kupitia sisi viumbe wake. Ni kama anavyotumia UZAZI kuendeleza kazi yake ya UUMBAJI ndio maana tunakemea utoaji mimba.

Sasa tunaingia magotini....

Je, tunaingia magotini kwa kuwa tuna HOFU?
Je, ni kwa kuwa ni 'maagizo' kwamba tusali?
Je, ni kumshirikisha Mungu wakati tunatumia AKILI alizotujalia ili atende kazi?
Je, tunasali kwa kuwa hatutaki tena kuwajibika?
Je, tunatumia sala kama njia ya kuficha uzembe?

Kila mmoja anajua kwa nini aingie magotini.

LAKINI

Nikumbushe, Yesu alisali, na ALITIMIZA WAJIBU.
Aliwapa watu chakula, japokuwa angeweza kutowapa chakula na kuwapulizia nguvu ya Roho Mtakatifu wawe wameshiba. Yesu ALIJIFICHA walipotaka kumpiga mawe... Hakujiachia hapo na kusema MUNGU ANAWEZA..

Wana wa Israeli walipewa mana, na walipaswa KUTOKA NJE ya nyumba zao kwenda kuzichukua...Hawakuketi kusubiri mana zijilete ndani ya nyumba zao. Ndio kusema, walipaswa waoneshe jitihada kupokea msaada wa Mungu.

Sisi WATANZANIA TUNAFANYA NINI?

Pamoja na kuliweka taifa katika maombi ambayo HAYAPASWI KUWA YA SIKU 3, bali maombi ya daima, tunatakiwa kuonesha juhudi katika kukabiliana na tatizo lililopo.

Kila siku unapotoka nyumbani kwako kuingia mtaani, jua kwamba unahatarisha maisha ya wengine. Jua kwamba unamweka muhudumu wa afya katika hatari ya kupoteza maisha.

Tujikumbushe haya kila tupigapo hatua huko mtaani: LEO NAKWENDA KUWAPELEKA WATU KADHAA KARANTINI. LEO NAKWENDA KUJIONGEZEA NAFASI YA KUWEKWA KARANTINI...

SERIKALI.

Pamoja na kuitia jina la BWANA, tujue kwamba juhudi zinahitajika. Kuhakikisha watu wanapata mask, huduma ya maji kwa bei nafuu, na WAHUDUMU wetu wapewe vifaa. Watu wapimwe, na taarifa zitoke.

Huwaambii watu wasali huku hata chai hawawezi kuimudu, au hawawezi kumudu kununua mask na vitakasa...

SALA na JUHUDI, SALA na AKILI, SALA na UKWELI.

Bibi Happy J
 
Nawaza ni katika point gani inabidi ufikie na kukubaliana kuwa hili ni janga kubwa na HATULIWEZI!
Na baada ya hapo wenye kuendelea na maombi waendelee na wanaoamini vyote (sayansi na Mungu) wachukue nafasi yao. Hapa nina maana kuwa sisi tukae pembeni na tuombe msaada (labda kutoka jumuia ya kimataifa na WHO) ndio waingie field!
 
Nyie Mbona kigali mmefungiwa mnakufa njaa tu na maambukizi yanaongezeka

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini tambua kuwa Rwanda wanafanya testing, sisi hatufanyi. Kwa kuwa hatufanyi, hatujui hata idadi ya walioambukizwa. Tunasuburi mtu aumwe ndiyo apimwe au ahisiwe kuwa ameambukizwa, ndiyo apimwe.

Rwanda wanafanya testing. Wanawagundua walioambukizwa hata kabla ya kuanza kuumwa. Kwa takwimu zilizopo, mpaka sasa hakuna raia wa Rwanda aliyepoteza maisha kwa Covid 19.
 
1587107656402.png

Maji ya kutiririka ni kutoka kwenye vidonga na vidumu
 
Nilifikiri wewe ni Mtu wa kiroho kumbe hujui kitu unaleta siasa siasa kwenye mambo ya Mungu.
Hujasoma Mfalme Daudi alipoteseka na njaa miaka mitatu mfululizo alimtafuta Bwana na akamwambia chanzo cha tatizo la njaa na namna ya kulimaliza.Maombi aliyoagiza Rais yanaweza toa solution nzuri zaidi ya kumaliza tatizo siyo copy na paste za Wazungu ili kupata msaada wao.
2Samweli 21:1...
 
SALA
Tunaposimama mbele za Mungu, tunapaswa kuwa na imani thabiti. Imani kuhusu utendaji wa Mungu na Neema zake.

Mwenyezi Mungu ametuumba kwa upekee sana. Ametupa AKILI na UTASHI, ili tuwe tofauti na wanyama. Neno linasema Tuenende kwa AKILI, kwamba kutumia AKILI sio dhambi.

Mwenyezi Mungu anatumia AKILI alizotupa kuonesha uweza wake na nguvu zake. Kwamba, anatenda kazi zake kupitia sisi viumbe wake. Ni kama anavyotumia UZAZI kuendeleza kazi yake ya UUMBAJI ndio maana tunakemea utoaji mimba.

Sasa tunaingia magotini....

Je, tunaingia magotini kwa kuwa tuna HOFU?
Je, ni kwa kuwa ni 'maagizo' kwamba tusali?
Je, ni kumshirikisha Mungu wakati tunatumia AKILI alizotujalia ili atende kazi?
Je, tunasali kwa kuwa hatutaki tena kuwajibika?
Je, tunatumia sala kama njia ya kuficha uzembe?

Kila mmoja anajua kwa nini aingie magotini.

LAKINI

Nikumbushe, Yesu alisali, na ALITIMIZA WAJIBU.
Aliwapa watu chakula, japokuwa angeweza kutowapa chakula na kuwapulizia nguvu ya Roho Mtakatifu wawe wameshiba. Yesu ALIJIFICHA walipotaka kumpiga mawe... Hakujiachia hapo na kusema MUNGU ANAWEZA..

Wana wa Israeli walipewa mana, na walipaswa KUTOKA NJE ya nyumba zao kwenda kuzichukua...Hawakuketi kusubiri mana zijilete ndani ya nyumba zao. Ndio kusema, walipaswa waoneshe jitihada kupokea msaada wa Mungu.

Sisi WATANZANIA TUNAFANYA NINI?

Pamoja na kuliweka taifa katika maombi ambayo HAYAPASWI KUWA YA SIKU 3, bali maombi ya daima, tunatakiwa kuonesha juhudi katika kukabiliana na tatizo lililopo.

Kila siku unapotoka nyumbani kwako kuingia mtaani, jua kwamba unahatarisha maisha ya wengine. Jua kwamba unamweka muhudumu wa afya katika hatari ya kupoteza maisha.

Tujikumbushe haya kila tupigapo hatua huko mtaani: LEO NAKWENDA KUWAPELEKA WATU KADHAA KARANTINI. LEO NAKWENDA KUJIONGEZEA NAFASI YA KUWEKWA KARANTINI...

SERIKALI.

Pamoja na kuitia jina la BWANA, tujue kwamba juhudi zinahitajika. Kuhakikisha watu wanapata mask, huduma ya maji kwa bei nafuu, na WAHUDUMU wetu wapewe vifaa. Watu wapimwe, na taarifa zitoke.

Huwaambii watu wasali huku hata chai hawawezi kuimudu, au hawawezi kumudu kununua mask na vitakasa...

SALA na JUHUDI, SALA na AKILI, SALA na UKWELI.

©Bibi Happy J
ushauri kwa SIRIKALE ya MEKO
PESA zinzotolewa na wenyeuwezo ikiwa ni misaada kwa ajili ya CORONA aka ''KOLONA'' naomba zitumike kununua BARAKODA na zigawanywe bure kwa wananchi wote ili tuweze kujikinga.
 
mi naona mzee baba kama kichwa chake hakipo sawa yaani alivyotuaminisha mwanzo yeye na dada Bashite sasa wanaruka kimanga
 
SALA
Tunaposimama mbele za Mungu, tunapaswa kuwa na imani thabiti. Imani kuhusu utendaji wa Mungu na Neema zake.

Mwenyezi Mungu ametuumba kwa upekee sana. Ametupa AKILI na UTASHI, ili tuwe tofauti na wanyama. Neno linasema Tuenende kwa AKILI, kwamba kutumia AKILI sio dhambi.

Mwenyezi Mungu anatumia AKILI alizotupa kuonesha uweza wake na nguvu zake. Kwamba, anatenda kazi zake kupitia sisi viumbe wake. Ni kama anavyotumia UZAZI kuendeleza kazi yake ya UUMBAJI ndio maana tunakemea utoaji mimba.

Sasa tunaingia magotini....

Je, tunaingia magotini kwa kuwa tuna HOFU?
Je, ni kwa kuwa ni 'maagizo' kwamba tusali?
Je, ni kumshirikisha Mungu wakati tunatumia AKILI alizotujalia ili atende kazi?
Je, tunasali kwa kuwa hatutaki tena kuwajibika?
Je, tunatumia sala kama njia ya kuficha uzembe?

Kila mmoja anajua kwa nini aingie magotini.

LAKINI

Nikumbushe, Yesu alisali, na ALITIMIZA WAJIBU.
Aliwapa watu chakula, japokuwa angeweza kutowapa chakula na kuwapulizia nguvu ya Roho Mtakatifu wawe wameshiba. Yesu ALIJIFICHA walipotaka kumpiga mawe... Hakujiachia hapo na kusema MUNGU ANAWEZA..

Wana wa Israeli walipewa mana, na walipaswa KUTOKA NJE ya nyumba zao kwenda kuzichukua...Hawakuketi kusubiri mana zijilete ndani ya nyumba zao. Ndio kusema, walipaswa waoneshe jitihada kupokea msaada wa Mungu.

Sisi WATANZANIA TUNAFANYA NINI?

Pamoja na kuliweka taifa katika maombi ambayo HAYAPASWI KUWA YA SIKU 3, bali maombi ya daima, tunatakiwa kuonesha juhudi katika kukabiliana na tatizo lililopo.

Kila siku unapotoka nyumbani kwako kuingia mtaani, jua kwamba unahatarisha maisha ya wengine. Jua kwamba unamweka muhudumu wa afya katika hatari ya kupoteza maisha.

Tujikumbushe haya kila tupigapo hatua huko mtaani: LEO NAKWENDA KUWAPELEKA WATU KADHAA KARANTINI. LEO NAKWENDA KUJIONGEZEA NAFASI YA KUWEKWA KARANTINI...

SERIKALI.

Pamoja na kuitia jina la BWANA, tujue kwamba juhudi zinahitajika. Kuhakikisha watu wanapata mask, huduma ya maji kwa bei nafuu, na WAHUDUMU wetu wapewe vifaa. Watu wapimwe, na taarifa zitoke.

Huwaambii watu wasali huku hata chai hawawezi kuimudu, au hawawezi kumudu kununua mask na vitakasa...

SALA na JUHUDI, SALA na AKILI, SALA na UKWELI.

©Bibi Happy J
Mungu huyu huyu tunaye hubiriwa kwenye Biblia na Qouran? HAPANA hawezi kusikia sala zilizohamasishwa na JIWE. Kuna wananchi walitaka kumuombea Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi na kikundi cha BASHITE na kwa amri ya Jiwe, walikamatwa au walikatazwa, sasa Mungu wetu aliye hai anaanzaje kumsikia mtu mwovu kama Jiwe?

Mungu wetu aliye hai anaanzaje kumsikia mtu aliyewabomolea nyumba wakazi wa Kimara- Kibaha bila fidia wakati wale wa Mwanza hawabomolewi kwa kuwa ni Wasukuma wenzie?.

Mungu wetu aliye hai aanaanzaje kumsikia mtu aliyetengeneza kikosi cha kuua wakosoaji kikiwa chini ya Bashite na kimewapoteza akina Ben SaaNane, Azory Gwanda na Simon Kanguye?

Watanzania lazima tuwe serious tutumie akili zetu na siyo akili za kuelekezwa na huyu Jiwe. Sioni kama Mungu anaweza kumsikia kwa hayo machache tu ingawa najua kuna mengi aliyoyafanya ya kukatili watu na kuwapeleka rumande bila hatia kwa miaka zaidi ya 3 sasa. Mungu tunaye muamini kupitia BIBLIA na QUORAN hawezi kutusikia kwa kuhamasishwa na JIWE. JIWE ana madhambi mengi sana na MUNGU HAPENDEZWI
 
Back
Top Bottom