Sala ya Myahudi Yasababisha Kizaazaa Kwenye Meli

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,072
1,250
Mtalii wa Israel alisababisha mtafaruku mkubwa kwenye meli nchini New Zealand na na kupelekea baadhi ya watu wafikirie kujirusha baharini kwa hofu ya bomu wakati Muisrael huyo alipoamua kutoa zana zake za kusalia na kusali kwa sauti ndani ya meli.
Tukio hilo lilitokea jana jumapili katika mji wa Picton nchini New Zealand wakati mtalii huyo wa Israel alipotoa viboksi viwili vyeusi na kujifunga mkononi na usoni kabla ya kuanza kusali kwa sauti katika lugha ambayo hakuna mtu katika meli hiyo aliyeielewa.

Polisi wa kikosi maalumu cha kupambana na ugaidi wakiwa na silaha waliivamia meli hiyo na kumweka chini ya ulinzi mtalii huyo wa Israel kabla ya kumshusha toka kwenye meli hiyo pamoja na jamaa zake alioambatana nao kwa mahojiano zaidi.

Kwa mujibu wa gazeti la Dominion Post, wafanyakazi wa meli hiyo iliyokuwa imebeba abiria 750 walishtuka kumuona mtalii huyo wa Israel akitoa viboksi viwili vyeusi toka kwenye begi lake na kujifunga mkononi na kwenye paji lake la uso.

Wafanyakazi hao walitoa taarifa polisi ambapo kikosi maalumu kikiwa na silaha nzito kilivamia meli hiyo na kumweka chini ya ulinzi mtalii huyo.

Akiliongea suala la mtalii huyo wa Israel kuwekwa chini ya ulinzi wakati akisali, afisa mmoja wa serikali ya New Zealand alisema kuwa tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya kutokana na hofu kubwa ya ugaidi iliyopo nchini humo.
 

Avocado

Member
Aug 23, 2010
97
0
Kweli dunia imekuwa haina amani,na ni vizuri kuchukua taadhari kila inapowezekana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom