Elections 2010 Sala ya kuiombea Tanzania baada ya uchaguzi

We can

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
678
47
Mungu uko wapi. Mbona Tanzania inaanza kupoteza mwelekeo kwa haraka? Watu wanapenda mali na madaraka na UPENDO baina yetu unafifia. Au ndo utimilifu wa maandiko Matakatifu kwamba siku za mwisho watu watapenda mali kuliko kukupenda wewe?

Shuka MUNGU, SHUKA HARAKA. Tusamehe Baba pale tulipokukosea. Tunajua kuwa sisi sote wana wa Tanzania ni watoto wa Adamu na Eva; lakini tumejigawa sasa kwa misingi mingi potofu kwa kisingizio cha Siasa tukitafuta Ufalme.

Tunajidanganya kuwa, kwa majeshi ya duniani tuna nguvu, kwa porojo majukwaaani tunaheshimika, kwa ulaghai tunasifiwa. Tumesahau kwamba tulizaliwa uchi na tutakuwa mavumbi muda mfupi ujao. Tena, twakubali kuwatesa wengine wa kizazi cha sasa na cha baadaye huku tukifumbia macho ukweli kwamba maisha yetu ni kama maua: yamea na kuchanua asubuhi na jioni yanyauka.

Mungu wa miungu, Mfalme wa wafalme, SHUKA BWANA. Bwana wa majeshi nyoosha mkono wako....Ibariki nchi yetu na viongozi wake watende wanayoyanena na wawe na HOFU yako ee Mwuumba, Amina.
 
Back
Top Bottom