Sakra-mauti ya ubepari, kifo cha ukomunist na ugaidi wa kweli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakra-mauti ya ubepari, kifo cha ukomunist na ugaidi wa kweli!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwalimu Jr., Sep 28, 2008.

 1. m

  mwalimu Jr. Member

  #1
  Sep 28, 2008
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  UKOMUNISTI AU UJAMAA ulipokuwa ukikata roho televisheni za dunia nzima zilikuwa zikishangilia lakini hii leo UBEPARI umo katika sakra-mauti na wanafiki wote wanaupamba kwa urongo wa kila aina huku wakiomba lifanyike kila jambo ili 'artificial respiration' katika chumba cha wagonjwa mahututi kiwezeshe ubepari kuendelea kuishi.

  Haiyumkiniki, kweli Wamarekani wanaweza kukwiba watakakokwiba lakini ubepari sio mfumo unaoweze kudumu kwa kuwa unaendelea kuwepo tu mpaka pale viongozi wa kibepari wanapojua kuwa wanaweza kuiba fedha yote iliyopo hazina na wao wakaendelea kujichana kama kawaida huku wananchi wa kawaida wakitumbukia kwenye kikaango cha mafuta ya kupikia.

  Haya sio niliyoyasema mimi bali ni Karl Marx ambaye alistahili kuwa mtetezi wa ubepari na sio mpiga vita ubepari.

  Hakuna UGAIDI mbaya kama ule wa VIONGOZI mliowachagua kugeuka wezi na mafisadi wa kutupwa. Kilichofanyika Marekani sio kingine ila ubia kati ya mabepari wa Republican party na wakurugenzi wa mabenki na taasisi za mikopo mikubwa mikubwa kuchota fedha kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Marekani 2008 na kisha kutaka kuwabebesha msalaba wakopaji wadogo wadogo.

  Dada Leah Bourne wa Marekani alishaandika kitabu kizuri tu kilichoitwa : The Inherent Instability of a Debt-Driven Economy' na wengi walimpuuza lakini yale yale aliyoyaandika ndiyo yanayoendelea hivi leo kama vile ni Mchezo wa kUigiza ambao ni 'live'!

  Tafakari mwenyewe hivi gaidi wa kweli ni Bepari anayetaka kulitoa hata jiwe damu au wachanganyikiwa wachache wa madhambi ya ubepari wanaokurupuka hapa na pale na kuua na kuwajeruhi hata damu yao wenyewe?
  Yanayotokea New York, London na kwingineko kwenye ubepari uchi uchi uliokomaa sio jingine ila ni jumuihso la kuanzishwa vita vya UGAIDI lililokuwa na lengo la kuruhusu VIONGOZI katika nchi za kibepari na vyama tawala kuwaibia WANANCHI wake kushoto na kulia kwa kisingizio cha kupiga vita ugaidi na kuanzisha uvamizi wa nchi kama Iraq na Afghanistan ili waibe bila kujulikana-toka kwenye mabenki yao na toka kwenye nchi wanazovamia.

  Septembe 11 haikuua watu waliofikia hata 10,000 lakini toka hapa Marekani na washirika wake wamewaua Waislamu wasiokuwa na hatia milioni 4 na bado wanaendelea kuua.
  Kiongozi mmoja wa Marekani aliwahi kuwaambia Wamarekani wenzake kwamba kama kuna kitu cha hatari na kuogopa sana ulimwenguni sio kitu kingine ila hofu. Akawataka waiogope hofu kuliko ukoma!

  Chini ya uongozi wa Bwana George Bush, hata hivyo, Marekani sio tu imeweza kuwatia hofu Wamarekani bsli pia viongozi mbalimbali Afrika wakiwemo wale wa Afrika Mashariki.

  Sote tunajua kuwa hofu au kisingizio chochote cha hofu kwa Afrika ni biashara nzuri kwa polisi wa Kiafrika kufanya biashara ya rushwa na kumalizia hasira zao za kulipwa mishahara kidunchu kwa watu masikini ha kama ilivyo Kenya kwa Waislamu ambao mfumo mzima wa nchi hiyo pamoja na kuchaguliwa kwa Raila Odinga kuwa Waziri Mkuu [ambaye Waislamu wengi walikuwa na imani naye ya kuibadili hali hiyo] umejengwa kuwadhalilisha na kuwahujumu Waislamu wa nchi hiyo.

  Hatuamini kuwa Wana Usalama wa Tanzania wanaweza kuwa na wivu, ubabe, uonevu na chuki dhidi ya Waislamu kama jamaa zao wa Kenya. Na kwa sababu Watanzania sio watu wenye akili fupin na kununulika kwa bei sawa na bure hatuamini kwamba watawapa polisi wanyanyasaji wa Kenya ushirikiano wowote wa kutafuta wachawi wa Ugaidi wakati mchawi mwenyewe ndio huyo huyo anayetoa kitu kidogo kwa viongozi wao ili wawakurupushe jamaa kila inapokaribia Agosti 8 ili waonekane wanafanyia kazi rushwa waliyopewa na Waibaji wakuu wa madini Kongo na wavurugaji wa amani nchini humo.

  Inafaa bila kujali tofauti zetu za rangi au dini au nyinginezo kujadili 'tatizo la matajiri kuhehushwa na hofu ya ugaidi kama kweli ni tatizo letu Afrika!'

  Binafsi yangu ninadhani tuna matatizo makubwa kama vile kuuawa maalbino, ubakaji tena na midubwana yenye ukimwi; watoto wetu kunyanyaswa, kuumizwa hata kuuawa wakati mwingine na mijitu isiyo na huruma wakati kuna polisi tunaowalipa mishahara; barabara mbovu na zisizopitika kwa urahisi; serikali za Kiafrika kutufanza masikini zaidi jana tulikuwa tuna magari leo tunapanda na kunyanyaswa kwenye taksi, matatu na daladala; umeme ghali tena kwa asilimia ndogo tu ya wananchi mijini; hatuoni biahsara yoyote ya maana kati ya nchi zetu; mashirika ya hifadhi, bima, mifuko mbalimbali na benki kuu kutuibia fedha zetu; watoto wa viongozi na matajiri kupewa nafasi zote nzuri za masomo na kazi wakati watoto wa walalahoi wananyanyaswa kwa mikopo ya fedha za wazazi wao wenyewe na kuwa na wakuu wa vyuo vikuu wanasesere waliowekwa na viongozi wa nchi kwa sababu wanazojua wao wenyewe; elimu na afya zimepanda bei kichaa; kwingine hatuna maji wengine hawana umeme; usafiri, vyakula na vitu kupanda bei mara kwa mara na kadhalika na kadhalika.

  Ninaamini Waafrika wa Afrika Mashariki tunastahili kuwa na hofu lakini sio ya kubomolewa kwa majengo ya balozi za Kimarekani kutokana na uzembe wao wenyewe. Watamtukanaje mamba wakati wako mgongoni mwake?

  Hofu yetu iwe juu ya matatizo yetu ya msingi-chakula, maji, usalama, afya, elimu, mawasiliano na mahitaji mengine ya msingi kwa watu wetu.
   
 2. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  MWALIMU JR,lest you forgot,KARL MARX was aware that capitalism had resources at its disposal to allow it to counter the effects of its internal contradictions.fundamentally scholars argue,marx might have been right about the crumbling of capitalism.Vividly he got it wrong was on the timescale by which capitalism would meet its nemisis.by the look of it communism if it ever was to take over,is a damn,damn long way away
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu heshima mbele sana,

  Article ni kali sana, ila sina uhakika kama nimekuelewa vizuri, are you saying kwamba ukomunisti ni bora kuliko ubepari, au? Mkuu huwezi kuelewa kua ukomunist ulipokuwa unakufa hakukuwa na anyhelp kwa sababu within it haujawahi kuwa na a built in system ya kuukoa, as opposed to ubepari, kwa sababu look what is happening in US,

  Kwa mfano, AIG ilikuwa njiani kuanguka, New York State yaani serikali ya mkoa wa NY, uka-inject dola billioni 87 na kuiokoa, huku state ikiiishia kumiliki share 80% ya shirika hilo from there on, na with a condition kwa AIG kurudisha hela hizo za serikali ya NY State in 24 months with a profit, sasa kweli unaweza kulinganisha ubepari na ukomunist ambao kuanguka kwa Russia tu, ukawa ndio mwisho wake hakukuwa na help wala artificial respiration ya kuukoa, China sasa hivi wanadanganya kuwa ni wakomunist wakati ukweli ni mabepari wanaowadanganya wananchi wao!

  Bado ubepari uko imara na ndio the only solution kwa matatizo ya uchumi duniani, the best system ni lazima iwe na njia za kujiokoa kama ubepari sasa hivi, kuteleza sio kuanguka mkuu, au?
   
 4. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mwalimu jr,
  Mimi sikuelewi kabisa.Ugomvi wako ni upi hasa???.Naiona hii mada imekaa kidini dini sana.Umenishangaza zaidi kwa kusema kuwa "WATU WALIOKUFA KWENYE 9/11 HAWAFIKI HATA 10,000" Haraaaaa!!!!! kumbe ukiua watu chini ya 10,000 ni sawasawa.Yaaani unatetea hao walioua watu chini zaidi ya 10,000.Wewe ulitaka wauawe wangapi ndo wa-react.Hapa kamwe usijadili idadi ya waliouawa bali jadili kiini hasa cha hao chini ya 10,000 kuuawa.

  Nakushauri pia usiwe muumini zaidi ya karl Max na kusahau wanamitazamo wengine.Kama wewe unamuona Karl Marx na mitazamo yake alikuwa sawa kuna mwingine anamuona Darwin,Socret,Plato,Arstotle,Webber,Hume,nk wako sawa zaidi kuliko huyo Karl Marx.Hiyo ni mitazamo tuu ya hao wakubwa na siyo tija kuwa kwa vile wao waliona hivyo basi na sisi tuone sawasawa kama wao.Unafikiri challenges za wakati wa Karl Marx ni zile zile za wakati huu????

  Kwa mimi mtu wa Darwinism naona sawasawa tu.Yote haya ni natural selection
   
 5. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2008
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
   
 6. a

  akili Member

  #6
  Sep 29, 2008
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TATIZO letu ni kuwa tumeacha kumuabudu aliyetuumba na sasa TUNAWAABUDU WAZUNGU kama wao waliweza kufanya walichofanya na kama kweli sisi ni binadamu na sio NYANI kwanini tushindwe basi angalau kuwaiga kama hatutakuwa na jipya.

  Na mashehe na mapadri wa dini hii mpya ya KUWAABUDU WAZUNGU sio wengine ila marais, mawaziri wetu wakuu, mawaziri, wabunge na viongozi wa vyama na serikali. Kila mmoja yuko mfukoni mwa mzungu huyu au yule na sasa wameingia Wachina, Warussia, Wakorea, Wahindi na Wajapani wanapigana vikumbo kujiuza kwa jamaa hawa kama vile 'machanguo'

  Lazima sisi vijana wa Afrika tukatae kuendelea kuwa na viongzi wa karne ya 19 wakati hii ni karne yetu na siyo wala ya 20 bali 21.

  Vikwazo vyote vinavyomzuia mtu kuwa Rais akiwa na miaka 35 lazima viondolowe. Vikwazo vyote dhidi ya kuwa na wagombea huru lazima viondolowe. Vikwazo vyote dhidi ya kuwa na Katiba mpya lazima viondolowe na vikwazo vyote dhidi ya kukua, kupanuka na kuota mizizi demokrasia lazima vitafutiwe ratu na masepetu viondolowe.


  Hawa jamaa zetu utafikiri ni sanamu au wanasesere eti. Mzungu akiwaambia hili haya wanafuata; akiwakata hili haya wanaacha; pitisheni sheria ya ugaidi, hiyo wanaipitisha; ondoeni unafuu kwenye huduma muhimu kwa wananchi ikiwemo elimu na afya wanafuata. Lakini ngoja wewe msomi wa Kiswahili uwaambie chochote wanakuona mpuuzi utadhani ushuzi wa mbuzi!

  Lakini ukweli ni kuwa ubepari kama ujamaa mahututi jamani. Lazima kuwe na siasa bora zaidi kuliko ujamaa na ubepari. Nayo ninaamini ni mchanganyiko wa yote mawili au ule mseto ambao wana-CCM Zanzibari wameapa hawatakaa wakubali upikwe achilia mbali kuula!
   
 7. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2008
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  MAJITA,the history of the twentieth century is impossible without reference to marx's ideas.the revolutions in russia and china were both,at least ostensibly marxist in character.hitler blinded by the hate of communism ordered the invasion of the soviet union,this invasion and the resultant defeat,saved this world from the clutches of fascism.if as a result of marx's philosophy communisim had triumphed over capitalism,you never know,perhaps we would have been living in a classless society,a sort of heaven on earth society.unfortunately GOD never gave us the power to peer into the future,hence it will always be what if communism had won the day
   
 8. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Binafsi naamini haiwezekani ukawa pure komunist or pure capitalist,you will always blend the two though one of which will color your face like US with capitalism and china with comunalism
   
 9. Manda

  Manda JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 2,075
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Capitalism is very natural; and real; while Communism is artificial (thinking)/utopia! Hebu twambie ni nchi gani haiko capitalist? or hai-practice capitalism? Wewe unamiliki gari au nyumba/land? then what do you call yourself? Man is naturally greedy and have to own (ownership) wealth; usichanganye capitalism na abuse of power/au sheria![/QUOTE]

  Am somehow a keen student of Marx. Karl Marx Philosophy is too much idealistic/utopian than realistic, that is why personally mara baada ya kusoma falsafa yake i come into realizing that Socialism/Communism was meant to die!, it was just a mnatter of time that thing to happen!

  US is going down due to its own arrogance!, Falsafa ya ubepari inaura nyingi, what we are obsreving now US ni kusnhindwa kwa namna yao ya Ubepari (i mean kwa jinsi walivyo utafsiri wao), tusi-rule out Ubepari inhali another form of capitalism which is employed by the Chinese na Indians is prospering!

  Inhali hawa wanahangaika ku-bail out financial market ku-rescue uchumi wao....on the other side of the very planet others are busy sending people into space!!!!, hapo ndio utujua what will be the global picture in the coming 20/30 years!!subiri!!
   
Loading...