Sakata za Richmond, EPA sasa kuhamia katika vikao vya CCM

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Posted Date::6/14/2008
Sakata za Richmond, EPA sasa kuhamia katika vikao vya CCM
*Wajumbe, wabunge kumwaga siri hadharani
*Yadaiwa lengo ni kuwazuia kushutumu, bungeni

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mwananchi

SUALA la kashfa ya Richmond na mabilioni yaliyochotwa katika Akaunti Maalum ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), linatarajiwa kutawala mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC-CCM) na waliotuhumiwa kwa kashfa hizo kujieleza mbele ya wajumbe wenzao na wabunge wa chama hicho.

Kikao hicho ambacho kitakuwa chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kitafanyika katika Ukumbi wa African Dreams mjini hapa.

Habari zilizopatikana mjini hapa zinadai kuwa, wabunge wa CCM waliomba kukutana na Rais Kikwete na awali kikao hicho kilikuwa kifanyike Alhamisi wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, lakini kikaahirishwa.

Kule White Sands tulikuwa tukutane na Kamati Kuu ya CCM, lakini kikao kikaahirishwa hadi tulipotaarifiwa kwa barua juzi, kilidokeza chanzo chetu cha habari.

Kiliongeza kuwa, lengo ni kutoa malalamiko yao jinsi suala la Richmond na watu waliohusika na kuchota fedha za EPA, linavyoshughulikiwa kwa sababu hatua haziridhishi.

Katika kikao cha Dar es Salaam kilichoahirishwa kuna kundi la wabunge lilikuwa limejipanga kuitetea Richmond kuwa haijawahi kulipwa hata shilingi, huku likitaka kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa Bunge, Samuel Sitta.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana zilidai kuwa, kundi hilo limesimamisha mpango wao kwa sababu, baadhi yao waliokuwa wamerubuniwa kuiunga mkono hoja hiyo wameanza kukataa kwa kile kinachoelezwa kuwa, wataonekana kioja mbele ya wapiga kura wao.

Taarifa za uhakika ambazo Mwananchi Jumapili imezipata zinaeleza kuwa, baadhi ya wabunge wanatarajia kutoa malalamiko yao kwa sababu hawaridhiki na hatua zinazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa Richmond na EPA.

''Barua ya mwaliko haijaeleza ajenda, lakini ninachofahamu utakuwa uwanja wa kila wabunge na wajumbe wa NEC watatoa yanayowakera, badala ya kwenda kuyazungumzia bungeni,'' kilidokeza chanzo chetu na kuongeza:

''Iwapo hatua zaidi hazitachulikuwa umma hautatuelewa, hatuwezi kuishia kuwa wamewajibishwa kwa kujiuzulu, huku kundi hilo likiingia msituni kwa ajili ya kupiga vita serikali hii, likiwa na malengo ya mwaka 2015 kuchukua Urais, hatuwezi kwenda,'' alisema.

Katika semina iliyofanyika jana kwa wajumbe wa NEC na kuhudhuriwa na Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndullu, inaelezwa iliwasilishwa taarifa ya hali ya uchumi, lakini Katibu wa Itikadi na Uenezi, Kapteni John Chiligati alikataa kutoa walichozungumzia.

Pia, Profesa Ndullu anatarajiwa kuhudhuria kikao cha leo kinachojumuisha wabunge na wajumbe wa NEC.

Februari mwaka huu Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa upatikanaji wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura, iliyopewa Kampuni ya Richmond Development LLC, ya Hauston Marekani, iliwasilisha ripoti yake bungeni na kusababisha mawaziri kadhaa kujiuzulu akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Kyela (CCM), alipendekeza kuwawajibisha wahusika wote, wakiwamo mawaziri na watendaji wa serikali kutokana na kushiriki kwao namna fulani katika kufanikisha mkataba huo.

Katika hatua nyingine, uchunguzi wa wizi wa fedha za EPA uliofanywa na Kampuni ya Ernest & Young unoanyesha kuwa makampuni 22 yalihusika katika kuchota jumla ya sh bilioni 133 kutoka katika mfuko huo.

Kampuni hizo zilizochota fedha hizo baadhi yake zinamilikiwa na wafanyabishra ambao ni wanachama wa CCM na viongozi wa chama hicho.
 
Hii sirikali sasa ni mufilisi kabisa!!!! Ufisadi uliofanyika EPA na Richmond unawahusu Watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao, hivyo vyote hivi vina kila sababu ya kujadiliwa hadharani katika bunge la Tanzania ili Watanzania waweze kufuatilia kwa karibu na kujua nini kinaendelea.

Sasa hii serikali jinsi ilivyo mufilisi inataka kuyapeleka majadiliano ya haya mambo mazito kuhusiana na ufisadi katika vikao vya siri vya chama cha mafisadi ili Watanzania tusijue nini kinachoendelea. Watanzania kamwe tusikubali na huu uamuzi wa kipuuzi na kifisadi ambao nia yake kubwa ni kuendelea kuwalinda mafisadi kwa kila hali na kuendelea kukilinda chama cha mafisadi ili kiendelee kubaki madarakani. Tuwashinikize kwa nguvu zetu zote ili kuhakikisha majadiliano kuhusiana na ufisadi wa EPA, Richmond, Kiwira na hata ripoti ya mikataba ya madini yote inajadiliwa hadharani bungeni.
:(:(:(
 
Heshima mbele mkuu,yaani mpaka sasa muungwana nchi hii imemshinda maana katika masuala ya EPA na RICHMOND ripoti zake zipo wazi kabisa zinaonyesha wezi na mafisadi kwahiyo ilitakiwa achukue hatua kali za kuwaadhibu yeye kama rais na kumaliza haya masula na sasa hivi tungekua tunazungumza mambo mengine ya kimaendeleo,lakini mpaka sasa hakuna kitu zaidi ya kuleta usanii tu.
 
dawa pekee ya CCM ni kuwaanika hadharani .Walipelekea hata Gavana kusema uongo juu ya kukua kwa Uchumi akija na point ya kijinga ya kusema our currency was getting strong against the dollar akasema ndiyo kipimo cha Uchumi kukuwa wakati Dollar ina shida kubwa Duniani .
 
Vikao, vikao, vikao, vikao.... Huku watuhumiwa wanaendelea kuficha ushahidi, sisi tunaendelea na vikao tu, hivi tumerogwa jamani?
 
Hii ni Nchi ya Domokrasia kaka mpitanjia, Swala la kulongwa mbona lipo wazi? huoni Dr. Mwakyembe amelogwa tena na Mbunge?
 
Demokrasia gani hiyo ya vikao kila siku? Mahakama si zipo kwa ajili ya kutoa haki? Kama kuna watuhumiwa wameiba mamilioni na ushahidi upo wapelekwe mahakanai. kama hakuna ushahidi watueleze ukweli tuendelee na mambo mengine kuliko kila siku kukaa vikao vya suala hilohilo mpaka tunashindwa kufanya mambo mengine ya maendeleo. Wananiudhi sana
 
Gavana anatekeleza ilani na sera ya chama .............kwenye sehemu ya fiscal policy....ndio maana ameombwa akaseme mchanganuo wake...katika chama chenye hatamuuu...................ni mtazamo wangu...
 
Back
Top Bottom