Sakata la wizi wa tiket;tff kuna kamchezo gani humo ndani?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sakata la wizi wa tiket;tff kuna kamchezo gani humo ndani??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 24, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,147
  Likes Received: 5,576
  Trophy Points: 280
  Watanzania wamekuwas na hamu sana na shauku kubwa kujua jinzi gani kumbe wakati wachezaji wakiumia uwanjani kutafuta point tatu huku kuna baadhi ya wafanyakazi wa timu wakishirikiana na viongozi wa TFF kujaribu kuhujumu pesa za viingilio kwa kutengeneza tkt feki;sakata la majuzi limenishtua sana kama si k kunihuzunisha jamani hasa kwa wale vijana wanaonyonywa;;;embu fikiria dogo amekutwa na vitabu 5,kila kimoj kikiisha kinatoa laki saba....hiyo ni kwa mechi ya kijinga kama yanga na moro..jiulize simba na yanga wanakula ngapi wahuni hawa wakishirikiana na viongozi wa TFF..tunaomba SERIKALI iingilie kati wahusika wote wapewe adhabu kali \\na kuwa mfano kwa wapuuzi wengine wanaochezea maisha ya wale vijana /wazee uwanjani..inaumiza sana...tena sana jamani

  Mkurugenzi wa Fedha wa Shirikisho la soka nchini (TFF), Daniel Msangi (35) pamoja na Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Interpress Ltd, Laurence Mally (36), wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Temeke, wakikabiliwa na shitaka la kughushi tiketi zenye thamani ya Sh. 700,000 na kuiba.

  Licha ya mtuhumiwa Msangi kutajwa kwenye hati ya mahakama kama Mkurugenzi wa Fedha, lakini kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela, Msangi ni Kaimu Mtunza Stoo, na kwamba Mkurugenzi wa Fedha wa TFF ni Ahmed Naeka.

  Washitakiwa hao walisomewa shitaka lao jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Heleni Riwa, ambapo upande wa mashitaka uliongozwa na Mrakibu wa Polisi, Bassil Pandisha.

  Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama kuwa katika kesi hiyo, watuhumiwa hao wameunganishwa pamoja na Mohamed Salumu ambaye alikuwa anafanya biashara kuuza tiketi hizo 'feki', ambaye tayari alishasomewa shitaka lake mwishoni mwa wiki iliyopita.

  Pandisha alidai kuwa washitakiwa wote watatu walikamatwa kwa pamoja Machi 15 mwaka huu katika maeneo ya Uwanja wa Uhuru uliopo katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

  Mwendesha mashitaka alidai kuwa washitakiwa hao walikutwa na tiketi 'feki' za mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom baina ya Yanga na Moro United iliyofanyika Machi 15 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

  Alidai kuwa washitakiwa hao walikutwa na tiketi feki zenye namba kuanzia 3001 hadi namba 3100 zenye thamani ya Sh.700,000 mali ya TFF.

  Washitakiwa hao walikana shitaka lao na kupatiwa dhamana mpaka kesi hiyo itakapotajwa tena katika mahakama hiyo Machi 31 mwaka huu.

  Wakati huo huo, taarifa nyingine zilizotufikia jioni jana zilisema kuwa kiongozi mmoja wa Yanga naye amekatwa na Polisi kuhusiana na kashfa hiyo ya tiketi bandia za mechi baina ya Yanga na Moro United.

  Alipotafutwa msemaji wa Yanga, Louis Sendeu, alikiri kuzisikia taarifa hizo lakini alisema hawezi kuthibitisha kwa sababu bado hazijawa rasmi.

  "Taarifa kamili itatolewa kesho (leo), lakini kwa sasa sina taarifa rasmi," alisema Sendeu.
   
Loading...