kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,069
- 264
SAKATA la wizi wa mamilioni ya fedha, linalowakabili wahasibu wawili wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha(AICC), limechukua sura mpya baada ya uongozi wa kituo hicho, kuamua kuwaondoa katika ofisi hiyo, kupisha uchunguzi wa kina unaofanyika, sanjari na kuwaandikia barua ya kuwataka watoe maelezo, kila mmoja kwa nafasi yake jinsi alivyohusika na wizi huo.
Watuhumiwa hao Haji Shabani (43) na Adela Kimaro (52), wanadaiwa kutafuna na kusababisha upotevu wa jumla ya sh 15,689,000 ambazo zilitokana na makusanyo ya wapangaji na ofisi za kituo hicho.
Wahasibu hao wawili walikamatwa na polisi, kisha kufunguliwa mashtaka ya wizi wa fedha, baada ya kuwepo taarifa za upotevu wa kiasi hicho cha fedha, tukio ambalo limedaiwa kutokea Novemba 8, mwaka huu, majira ya saa 4 asubuhi ndani ya ofisi ya Mhasibu Mkuu wa AICC.
Taarifa zaidi zimedai, Haji amehamishiwa ofisi ya kukusanya na kushughulikia mashuala ya bili, huku Adena yeye akihamishiwa ofisi ya kukusanya madeni, hata hivyo uhamisho huo unadaiwa kufanywa haraka ili kupisha upelelezi unaofanywa na uongozi wa kituo hicho kwa kushirikiana na polisi.